Bobi Wine asema Polisi waliiba nyaraka za uteuzi wake wa Urais

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mwanasiasa na mwanamuziki wa Uganda, Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ameiambia BBC kuwa nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya uteuzi wake wa kugombea urais zimepotea katika ofisi yake baada ya uvamizi wa ofisi hiyo wa vikosi vya usalama siku ya Jumatano mchana.

Moja ya masharti ya wagombea ni kuwasilisha sahihi za wafuasi wao 100 waliojisajili kupiga kura kutoka katika walau theluthi mbili ya wilaya za Uganda.Bobi Wine anasema timu yake ilikuwa tayari imekusanya sahihi milioni sita lakini hizi sasa zimepotea.

“Serikali ya Museveni inajaribu kunizuwia kuteuliwa kama mgombea wa urais. Kuanzia kuhoji nyaraka zangu, kuhoji umri wangu- na sasa wanafanya kila juhudi kukwamisha uteuzi wangu na ninaamini kuwa ndio maana walichukua saini .”

"Hatutakata tamaa, tumekwisha ripoti mara mojakwa matawi yetukuhakikisha wanaanza kukusanya saini mara mojana tunatumaini kufikia Ijumaa tutakuwa na saini zinazohitajika ,” alisema.

Mbunge huyo alikuwa akizungumza na BBC baada ya kutoroka kutoka katika ofisi yake wakati makumi kadhaa ya askari na polisi walipowasili kufanya msako.

Pia alisema milioni 23 Waganda milioni ($6,200 ) zilichukuliwa. Anasema pesa hizi zilichangishwa kusaidia kulipia garama za uchaguzi kwa ajili ya wanachama wanaotaka kugombea ubunge.

Polisi hawakujibu wito wa BBC wa kuzungumzia madai yaBobi Wine. Awali walikana kuwa uvamizi wa ulichocjewa kisiasa.

Tume ya uchaguzi iliwapatia wagombea siku ya Ijumaa kuwa muda wa mwisho wa kuwasilisha fomu zao za uteuzi..

Msemaji wa tume anasema hawezi kuzungumzia juu ya madai ya Bobi Wine ya kutoweka kwa nyaraka lakini anasema muda wa mwisho unaweza uongezwa kwa mgombea iwapo wataifahamisha tume rasmi.
 
Duh! nitakuwa mie ndio sijaelewa
Kweli waganda mumeendelea
Hapana maana umeuliza swali lakuchekesha, hata Tanzania wagombea wanapewa fomu ambazo wanakusanya watu wanajaza taarifa zao na kuzisaini na zinarudishwa kwenye tume kama hard copy.
 
Hapana maana umeuliza swali lakuchekesha, hata Tanzania wagombea wanapewa fomu ambazo wanakusanya watu wanajaza taarifa zao na kuzisaini na zinarudishwa kwenye tume kama
Na mie nimesemea hizo hizo kuwa ushahidi kwa hiyo tume na hao polisi wanaokataa kufanya hivyo
Ukiwa na copy wanapingaje?
 
Duh! nitakuwa mie ndio sijaelewa
Kweli waganda mumeendelea
Hapana maana umeuliza swali lakuchekesha, hata Tanzania wagombea wanapewa fomu ambazo wanakusanya watu wanajaza taarifa zao na kuzisaini na zinarudishwa kwenye tume kama hard copy.
Na mie nimesemea hizo hizo kuwa ushahidi kwa hiyo tume na hao polisi wanaokataa kufanya hivyo
Ukiwa na copy wanapingaje?
Lengo lao ni kwamba asigombee hawakawii kuendelea kuda OG
 
Back
Top Bottom