Bobi Wine ameshtakiwa akidaiwa kuwa na nia ya kumkera Rais Yoweri Museveni

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Mwanamuziki ambaye pia ni Mwanasiasa, Robert Kyagulanyi maarufu ‘Bobi Wine’ ameshtakiwa akidaiwa kuwa na nia ya kumkera, kumshtua au kumkejeli Rais Yoweri Museveni

Shtaka hilo linahusianishwa na tukio la Agosti 2018 ambapo Bobi Wine alishutumiwa kuongoza maandamano sehemu ambayo gari la Rais Museveni lilipigwa mawe na Waandamanaji

Bobi Wine ambaye ni Mbunge wa Kyadondo Mashariki tayari anakabiliwa na shtaka la uhaini na anaweza kufungwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia

Pamoja na kufunguliwa shtaka la uhaini Agosti 23, 2018 katika Mahakama ya Kijeshi baada ya kushikiliwa kwa muda mrefu huku akiteswa, ameendelea kuikosoa vikali Serikali ya Rais Museveni

Katika hatua nyingine, Mbunge huyo ametangaza pia kuwa atawania Urais wa Uganda dhidi ya Rais Museveni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021.

======

Ugandan musician-turned-politician Bobi Wine has been charged with a new count of intending to annoy, alarm or ridicule the president.

This is in connection to the August 2018 incident where he was accused of leading a protest where President Yoweri Museveni’s motorcade was stoned by protesters.

Wine, whose real name is Robert Kyagulanyi, is also facing a charge of treason and could be jailed for life if convicted.

The MP was charged with treason on August 23, 2018 in a military court after days of detention and severe torture.

Despite the brutal encounter with Ugandan government, Bobi Wine remains critical of the Museveni’s administration.

He has since declared his bid to contest for the Presidential seat against Museveni in the 2021 election.



Source: Citizen TV
 
BOBI WINE ASHTAKIWA KWA TUHUMA ZA KUMKEJELI RAIS MUSEVENI UGANDA
Posted by Tatu24 | Aug 7, 2019

Bobi Wine ashtakiwa kwa tuhuma za kumkejeli Rais Museveni Uganda
Msanii wa muziki nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu maarufu la Bobi Wine ameshtakiwa nchini humo kwa tuhuma za kumkera na kumkejeli Rais wa taifa hilo, Yoweri Museveni.

Mashtaka hayo, Yanajumuishwa na tukio la Agosti mwaka Jana, Ambapo Bobi Wine alishutumiwa kuongoza maandamano sehemu ambayo gari la Rais Museveni lilipigwa mawe na Wafuasi wa Bobi Wine.

Mbunge huyo wa Jimbo la Kyadondo Mashariki, Tayari anakabiliwa na shtaka la uhaini na anaweza kufungwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.

Mapema mwezi Julai mwaka huu, Bobi Wine alitangaza kuwa atawania Urais wa Uganda dhidi ya Rais Museveni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021.
 
Wameona Bobi Wine ana wafuasi wengi wanahaha.

Afrika viongozi sijui wana nini aisee!
 
Kampala (AFP) - A Ugandan court on Tuesday charged pop star turned leading opposition figure Bobi Wine with "annoying" President Yoweri Museveni, his lawyer told AFP.

The singer, whose real name is Robert Kyagulanyi, appeared in court on a prior treason charge after he and other opposition politicians allegedly stoned Museveni's convoy during a campaign rally in August last year.

"He was charged with annoying the president" in relation to the same case, his lawyer Asuman Basalirwa told AFP.

Wine, who entered parliament in 2017, has emerged as a leading critic of Museveni -- who has been in power for over three decades -- and has faced multiple detentions while authorities have frustrated his efforts to perform.

He announced last month that he would take on Museveni in 2021 national elections.

"This government of President Museveni is in panic mode. At first it was treason and now it is annoying President Museveni. Who on earth can't be annoyed?" Wine told AFP.

"It is a ridiculous charge and am ready to challenge it in court," he said.

The new accusation against Wine comes just days after prominent activist Stella Nyanzi was sentenced to 18 months in prison over her vulgar posts on social media against Museveni -- which she sees as a way to get her message across.
 
Si achukue mbinu za mwenzake?
Mwenzake alitaka kumaliza mtu pale area D.
Yeye anashindwa nini kukopi na kupaste?

Kw sababu hawa hawatakuja kufa . Hata Mobutu yupo hadi leo anaishi.
 
Kufungwa “MAISHA” sababu ya kumtukana Rais?

Hizi nchi ni shithole kabisa!

Kuna tofauti gani na adhabu ya kuua?

Maana anaeua anafungwa maisha,ni heri mtu amuue Museveni kabisa ili afungwe maisha kihalali!

Hizi nchi ni shitholes beyond me!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Si achukue mbinu za mwenzake?
Mwenzake alitaka kumaliza mtu pale area D.
Yeye anashindwa nini kukopi na kupaste?
Kw sababu hawa hawatakuja kufa . Hata Mobutu yupo hadi leo anaishi.
Ile mbinu kaona mwenzake kafail sasa wameamua kuwafunga maisha wakagombee urais gerezani hata hapa kwetu wengi wataozea gerezani tu.
 
Nabashiri soon moto usiozimika kirahisi utaenda kulipuka uganda.

Museveni ataondolewa na nguvu ya umma. Ataua sana, atafunga sana wapinzani lakini hataweza kushindana na nguvu ya umma.
 
Kwa Africa ni heri umkosee Mungu Muumba atakusamehe.Kuliko kumkosea mkoloni mweusi.
 
Ndege wafananao.. East Africa yote (ukiondoa Kenya kidogo), viongozi wanafanana tabia.. Tofauti ndogo iko kwenye how & to what extent do they deal with wapinzani.. Role model wa mtawala mmoja yeye anawamaliza wapinzani wake popote walipo..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kufungwa “MAISHA” sababu ya kumtukana Rais?

Hizi nchi ni shithole kabisa!

Kuna tofauti gani na adhabu ya kuua?

Maana anaeua anafungwa maisha,ni heri mtu amuue Museveni kabisa ili afungwe maisha kihalali!

Hizi nchi ni shitholes beyond me!

Heri upore kimada wa dikteta kuliko kutaka kukalia kiti cha dikteta Hakuna Rangi utoacha.
 
Ndege wafananao.. East Africa yote (ukiondoa Kenya kidogo), viongozi wanafanana tabia.. Tofauti ndogo iko kwenye how & to what extent do they deal with wapinzani.. Role model wa mtawala mmoja yeye anawamaliza wapinzani wake popote walipo..

Wanashare Genetic thus ufanana kitabia
 
Wamedumu madarakani si kwamba wana intelligence imara ni Kwa sababu awajagusa maslai ya Mzungu wanaiba Congo wanauzia wazungu hata kama watauwa raia wao.Siku wakigusa maslai ya wazungu ndipo watavurushwa madarakani wanacheza na akili ya mabeberu.
 
Ukiona dikteta anapanda ndege kwenda kumtembelea dikteta mwenzake chunga sana hapo wanapeana maagizo hatari ya kuuwa RAIA wao,utekaji, mauaji,kesi za uhujumu uchumi, kumfilisiwa Kwa wapinzani wao lzm ziongezeke,wanapanda ndege kukwepa udukuzi wa maagizo mabaya.Maana Simu zote urekodiwa duniani nzima.
 
Waafrica wataendelea kuumia sana hadi watakapoamua kubadili mifumo, miundo ya uongozi huu wa( uraisi) kama ndo dhamana ya kuongoza watu umefail miaka 60 sasa ya Uhuru umeshindwa isaidia Africa isonge,zaidi ya viongozi kujinufaisha wao,kuzigeuza nchi ni Mashamba yao,kujinufaisha binafsi, kuwapora waafrica kuficha ulaya, kuwauwa waafrica, kuwateka,kuwafunga,kuwafilisi,waafrica wenzao.

Yatendekayo Africa yanasadikisha maneno ya General Bernard Montgomery ( 1947) "Hakuna mwafrika awezae kumletea maendeleo mwafrika mwenzake, hawa wanataka Uhuru wapeni Lkn hawatofika kokote wataishia kuchinjana, kuuwana,kufilisiana,kutekana ,kufanyiana madhila ya kila namna, kiongozi wa kiafrika amejaa hila asili ya uovu ,ubinafsi, kuabudiwa ndani mwake". Na yote yaliyonenwa ndio yangali hata sasa baada ya Uhuru.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom