Bob Mtekama: FBI wa Malawi aliyekamata raia wetu huko Malawi

Sokoro waito

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
2,201
2,598
Utaifa Kwanza, TANZANIA moja yenye Ushindi.

Wadau hiyo ndiyo salamu yangu hapo juu.

Tujuzane machache kuhusu jirani yetu Malawi hasa katika ule mji wa MZUZU ambapo inasemekana raia wetu wamekamatwa wiki iliyopita na kuzuiliwa nchini humo, haijalishi ni kweli au la! Lakini tujuzane haya machache kuhusu huyu jamaa anaitwa Bob Mtekama na ule Mji wa Mzuzu.

BOB MTEKAMA.

Huyu jamaa ni askari polisi wa malawi ambaye kwa jina lingine anaitwa Bob Hamisi Stambuli Mtekama, umri wake haujathibitika ana miaka mingapi lakini huenda akawa ana miaka 30 hadi 45.

Ni askari wa usalama nchini MALAWI lakini pia hivi karibuni ametajwa na vyombo vya habari vya Malawi kama askari aliyehusika na ukamataji wa Wapelelezi wa Tanzania huko karibu na mgodi wa uranium ulioko Kayerekera wilayani Karonga kaskazini mwa Malawi katika jiji la MZUZU.

Hatahivyo askari huyu haegemei upande wowote wa kisiasa,

ndiyo maana alipokuwa mkuu wa polisi kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai (CID) mkoa wa kusini nchini Malawi alikataa kwenda kukamata wakosaji wa kisiasa dhidi ya wanasiasa wa chama tawala.(ukitaka picha yake nenda ZNZ UNIVERSITY)

ELIMU NA UTALAAMU WAKE:

Vyanzo vichache vinaonyesha kuwa askari huyu amesomea degree au stashahada ya sheria ya makosa ya Jinai katika chuo kikuu cha Zanzibar,

hatahivyo pia ni POLISI PEKEE nchini Malawi mwenye elimu ya sayansi ya itumikayo kwenye makosa ya jinai na madai (forensic science).

Elimu hiyo ya forensic science ameisomea katika chuo kikuu cha Malawi kwenye chuo kidogo cha udaktari, chini ya mwalimu wake mkuu Proffessor George Liomba na Dr. Charles Dzamalala.

Kwa upande wa taaluma, yeye ni mtaalamu wa alama za vidole (fingerprint) na pia ni yeye pekee aliye mtaalamu wa mwandiko(handwriting expert) katika jeshi la polisi nchini Malawi.

MAHUSIANO YAKE NA FBI.

Taarifa nyeti zinaonyesha Bob Mtekama amebobea pia kwenye Upelelezi ambao amefundishwa na FBI nchini Marekani.

Hatahivyo lazima tujiulize je alifundishwa na FBI kuwa Double agent wao(kwa ajili ya Malawi na kwa ajili ya Marekani)? Au alifundishwa na FBI kwa ajili ya Malawi tu?

Lazima tuwe makini na huyu jamaa!!

kwani pia alihamishwa kikazi kutoka mkoa wa kusini mwa Malawi akapelekwa Central Malawi na sasa yuko anafanya kazi kama Mkurugenzi wa CID (Criminal Investigation Department) nchini Malawi akiwa anafanya kazi huko mkoa wa kaskazini ya Malawi!!
Ambapo ndipo penye mgogoro wa mpaka kati yetu na Malawi.

Huenda aliletwa hapo kaskazini kwa kazi maalumu ya usalama wa mpakani.

HISTORIA YAKE YA KAZI:

Huyu jamaa anaitwa afisa wa polisi Mtalaamu kwa umaridadi wake wa kupambana na wahalifu wa makosa ya Jinai nchini Malawi,

ndiyo maana wakati alipokuwa anateuliwa kuwa mkurugenzi wa CID maneno haya hapa chini yalisemwa;

“The IG has made a landmark appointment on Mtekama as he will bring sanity to the CID department. He is a well disciplined and extensively trained and dedicated police officer with a methodological know how on how to curb crime and criminals having been a CID office for a long time.”

Hatahivyo alifahamika sana kama mkamataji hodari wa wahalifu wakati alipokuwa mkuu wa kitengo cha CID katika mkoa wa kusini mwa Malawi.

Inasemekana kuwa alihusika kuwakamata Majambazi wa kutumia silaha kwenye maeneo maarufu ya THYOLO and CHICHIRI waliotuhumiwa kuvamia Benki ya Taifa ya Malawi mwezi wa sita 2012 huko Malawi

pia alihusika katika ukamataji wa watuhumiwa wa wizi wa kijambazi wa Mishahara ya Wizara ya Elimu ya Malawi.

Bob Mtekama pia alihusika kwenye operation maalumu iliyowahusisha maafisa wengine wa kipolisi kama vile detective George Mnjale, detective Mkwate ambao kwa pamoja waliwakamata kwa ustadi wauaji waliokubuhu wa CHIRADZULU (Chiradzulu serial killers’ criminals.)

GEREZA LA MZUZU. (MZUZU PRISON)

Mzuzu ni mji ambao ni makao makuu ya mkoa wa kaskazini mwa Malawi.

Vyombo vya habari vya Malawi vinasema mji huu ni maarufu kwa kilimo na mifugo, hatahivyo taarifa ya hivi karibuni iliyoripotiwa na vyombo vya Malawi kuwa kuna wapelelezi wa nchi yetu wamekamatwa huko Malawi na kupelekwa rumande kwenye Gereza la Mzuzu ambalo lipo kwenye mji wa MZUZU.

HISTORIA YA GEREZA LA MZUZU.

Maelezo yanaonyesha kuwa gereza hili lilijengwa na mwingereza mnamo miaka ya 1950 hadi 1960 kwa ajili ya wafungwa 200 lakini kwa sasa inaonekana kuwa lina wafungwa zaidi ya 500,

hali inayopelekea mrundikano mkubwa wa wafungwa na mahabusu.

Hatahivyo miaka ya hivi karibuni zimejengwa selo mbili katika gereza hilo ila zilishindikana kutumika kwasababu ya kukosa uzio (fence).

Kutokana na sababu hiyo Prophet Bushiri na Mzuzu Lions Club walijitolea kujenga huo uzio kwa kutoa vifaa na pesa taslimu.

Kwahiyo Gereza hili bado linafurika kwa wafungwa na mahabusu, ambapo wengine hulala wakiwa wamekaa sebuleni au kwenye vyumba vya selo.

RAMANI YA UJENZI WA GEREZA LA MZUZU. (ARCHITECH MAP OF MZUZU PRISON)

Nimetafuta sana ramani iliyotumika kujenga gereza hili lililojengwa na taifa la Uingereza ila sijaipata lakini inaweza kupatikana kwa kupitia mfungwa/mahabusu mojawapo aliyewahi kufungwa hapo Mzuzu(sidhani kama huko Songea au Katavi atakosa mtu aliyewahi kufungwa au kuwekwa mahabusu katika gereza hili).

JIOGRAFIA YA GEREZA LA MZUZU.

Gereza hili lipo katika mji wa Mzuzu, mji huu uko kaskazini mwa Malawi ambapo ndipo kuna gereza hilo la Mzuzu.

Njia 2 za kufika Mji wa Mzuzu.

Mahali hapo panafikika kwa bus, treni au ndege ama helikopta. Usafiri wa gari ni km 46.6 unasafiri kwa muda wa dakika 56 hadi kufika hapo kama umepita njia ya Nkhata Bay mpaka mji wa Mzuzu.

Usafiri wa ndege in km 35 kwa muda wa dakika mbili tu kwahiyo kwenda na kurudi ni dakika 4 tu mpaka Nkhata Bay ambapo hapo Nkhata Bay kuna usafiri wa Maji hadi Mbamba Bay Tanzania.

Mzuzu GPS coordinates.
Latitude/ Longitude:
-11.45807, 34.015131 *
-11° 27' 29.0514", 34° 0' 54.471" **

Nkhata Bay GPS coordinates
Latitude/ Longitude:
-11.6085556, 34.29494090000003 *
-11° 36' 30.8016", 34° 17' 41.7876" **

(WGS84):
* Decimal
** Degrees, minutes, seconds

Njia ya pili ni ya kupita majini kutoka Manda ya Tanzania mpaka Chilumba pwani ya Malawi ambayo ipo karibu na Nyika National PARK

AMBAPO kutoka Nyika National Park hadi mzuzu kwa gari kuna umbali wa km156km kwa mwendo wa masaa 2 na dakika 46,

njia hii ni ya mzunguko sana hatahivyo kule karibu na mbuga sidhani kama kuna usalama wa kupita vyema hasa kutokana na wanyama wakali au askari pori.

ZIPO njia nyingine za kufika huko lakini sitazitaja hata kidogo.

ULINZI WA GEREZA LA MZUZU.

Gereza hili lina perimeter fence na ulinzi wa kawaida tu wa polisi wa Malawi japokuwa kuna military base kwenye mji huo wa Mzuzu.

Hatahivyo huu mji wa Mzuzu unakabiliwa na tatizo la kutokuwa na taa za kutosha za kumlika usiku.

Nilipokuwa mdogo nilifundishwa na wazazi wangu kuipenda nchi yangu haswaaaaaaa!

Nimefanya hivi kwa mapenzi ya nchi yangu na sio vinginevyo.

Mwisho.

Inayofuata hapa chini ni link yenye Picha ya mji wa Mzuzu.

C:\Users\TUMAC\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg

www.panorama.mzuzu
C:\Users\TUMAC\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image004.gif
 
Kama vipi tukavamie hilo gereza kinuke tujue moja!
Wazo lako halifai

Wapelelezi wa usa kibao wamekamatwa Iran ,North Korea na wamefungwa ila hakuna mashambulizi waliyofanya licha ya kuwa taifa kubwa

1.Negotiation za kidiplomasia mfano juzi serikali ya Obama ilikubali kuwalipa Ransom money Iran na wale mateka wakaachiwa japo alikataa ila watu wanaamini hvyo kuwa Ransom money ndio imesababisha wale mateka kuachiwa huru.

2.kubadilishana wafungwa

3.kulipa pesa "fidia'

4.nk nk nk

Mkuu hayo mawazo yako uliyotoa hufai hata kuwa mwenyekiti wa mtaa
 
Wazo la kijinga

Wapelelezi wa usa kibao wamekamatwa Iran ,North Korea na wamefungwa ila hakuna mashambulizi waliyofanya licha ya kuwa taifa kubwa

1.Negotiation za kidiplomasia mfano juzi serikali ya Obama ilikubali kuwalipa Ransom money Iran na wale mateka wakaachiwa japo alikataa ila watu wanaamini hvyo

2.kubadilishana wafungwa

3.kulipa pesa "fidia'

4.nk nk nk

Mkuu hayo mawazo yako uliyotoa hufai hata kuwa mwenyekiti wa mtaa
Nafaa kuwa mwenyekiti wa chama chetu ccm
 
Ufafanuzi kuhusu taarifa za kukamatwa kwa Watanzania wanaodaiwa ni majasusi nchini Malawi

Baadhi ya Vyombo vya habari vya hapa nchini hivi karibuni vilitoa taarifa kuwa, Watanzania 8 wanaodaiwa kuwa ni majasusi wa Serikali ya Tanzania wamekamatwa nchini Malawi kwa tuhuma za kuingia kwenye mgodi wa urani wa Kayerekera uliopo nchini Malawi kinyume cha sheria.
Taarifa hiyo kwa mara ya kwanza ilitolewa na chombo cha habari cha Malawi ambacho kilidai kuwa watu hao wametumwa na Serikali ya Tanzania ili kuchunguza kama Serikali ya Malawi inatengeneza silaha za nyuklia kwa kutumia madini ya urani ya kutoka mgodi huo.

Kufuatia taarifa hizo, Wizara kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi ulifuatilia ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Baada ya kufuatilia ilibainika kuwa ni kweli Watanzania 8 kutoka taasisi ya CARITAS iliyo chini ya Kanisa Katoliki Songea mkoani Ruvuma walikamatwa na vyombo vya usalama katika Wilaya ya Karonga ambayo inapakana na Wilaya ya Kyela. Watanzania hao mara moja walifunguliwa kesi kwa kutuhumiwa kufanya kosa la jinai la kuingia eneo la mgodi bila kibali (criminal trespass).

Ubalozi uliwasiliana na Taasisi ya CARITAS kutaka kufahamu madhumuni ya watu hao kufanya ziara nchini Malawi. Ubalozi ulielezwa kuwa ziara hiyo ilikuwa ni ya mafunzo ambapo walitaka kufahamu juu ya madhara yatokanayo na machimbo ya madini ya urani. Watanzania hao kwa sasa wapo katika gereza kuu la Mzuzu hadi kesi yao itakapotajwa tena tarehe 04 Januari 2017.

Ubalozi unaendelea kufanya mawasiliano na Kanisa Katoliki Songea ili kupata maelezo zaidi kuhusu ziara ya watu hao kwa madhumuni ya kuyawasilisha mamlaka husika ili watuhumiwa waweze kutolewa.
Aidha, Wizara kupitia Ubalozi umebaini kuwa CARITAS iliruhusu watu hao kufanya ziara nchini Malawi bila kupata kibali kutoka mamlaka husika na bila kutoa taarifa Ofisi ya Ubalozi kuhusu ziara hiyo.

Aidha, kipindi cha kufanya ziara hiyo nchini Malawi hakikuwa muafaka kwa kuwa watumishi wa Serikali ya Malawi wanakuwa katika likizo ya mwaka kuanzia tarehe 22 Desemba hadi 03 Januari 2017. Hii inakwamisha juhudi za kuwafuatilia watu hao ikiwa ni pamoja na kukwama kwa maombi ya kibali cha kuwatembelea watu hao tarehe 28 Desemba 2016.

Wizara inatoa wito kwa mara nyingine kwa taasisi za dini, vyuo vya elimu na watu binafsi kuomba vibali na kufuata sheria za nchi nyingine wanapofanya ziara za mafunzo au ziara nyinginezo ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na ofisi za Balozi zetu kwa madhumuni ya kufahamishwa taratibu zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kufanya ziara husika ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Wizara, kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi unaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa suala hilo linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 29 Desemba 2016.
 
hapo umetibua mkuu...tayr wameona uzaifu wao na sasa watajipanga
 
Back
Top Bottom