BOB MAKANI na uhalisia wa JINA LAKE...

Nyie wote ni wasukuma mikokoteni tu na siyo wa-Sukuma kama kabila. Kisukuma kina wingi wa kila neno ukitaka. Kisukuma kina lahaja za kikanda pia, Mwanza kuna lahaja zaidi ya 6, Shinyanga zaidi ya 4 na Tabora zaidi ya 4 pia. Sasa unabisha nini hapo Salum?

mwambie huyo. mi nimezaliwa alipozaliwa makani. kishapu hospital ijumaa tarehe 16. usiku.
 
Nilichojifunza hapa ni kuwa Mwanzilishi wa CHADEMA hakuwa mkristo, wala hakuwa mchaga. Hivyo kwa mtazamo wangu ni dhahiri kuwa hiki chama sio cha wachaga wala hakifungamani na wakristo kama Magamba walivyopotosha ukweli. Nadhani hiki chama kimempoteza mwana uhamsho mwanzilishi aliyekuwa na uchungu na maisha ya wananchi..RIP Baba wa taifa wa Chadema- MAKANI

Hat a muazilishi wa CUF hakua muislam lakini mwisho wasiku kikawa chaa.......jibu unalo
 
Bob Makani alikuwa mkristo, kama wakristo wengine wa Chadema. Kwenye Uislam hakuna mambo ya kuanika mwili kwa ajili ya "kuaga"
 
Na vipi yule binti yake Dr Julie Makani??
Hili ni suala tatanishi na nifundisho kwa uamusho kwamba uislam na ukristo wa watanzania umejichanganya sana katika jamii ni tofauti na jamii zingine kama za kisomali, kioman nk ambazo huwezi kuta dini zote mbili ndani ya familia moja

Huyu dada nilisikia story yake nisingependa niiweke humu, aliolewa na mtoto wa Iddi Simba kuna kitu kuhusu Dini yake alikifanya baadae kilimletea shida , ulizia vizuri ndugu yangu.
 
tumia akili yako vizuri mkuu. kwani Makani ni mwarabu? we vipi?

hayo majina ya uamsho hukohuko Bububu na Mwanakwerekwe.

Mbona amezikwa KIUAMSHO UAMSHO? mbona hilo hamlikatai? Jeneza limefunikwa na Khitma kasomewa , acheni mambo ya kubagua dini hapa, mwacheni mzee wa watu apumzike, ALLAH amuondolee adhabu ya Kaburi ampumzishe salama, INNA LILLAH WA INNA ILAIHI RAAJIUUN, kwa MWenye Ez Mungu na kwake tu ndio marejeo yetu .... Allah amrehem
 
Unawezaje kutafsiri majina ya mtu ukawacha jina lake la mwanzo? kwi kwi kwi teh teh teh!

Unaonaje wewe ukitafsiri hilo jina MOHAMED maana yake nini? Tusijiingize katika mgogoro wa kidini bila sababu ya maana?
Bahati mbaya Bazazi haamini jina linabeba IMANI yake (dini). Kwangu kuna majina ya Kiarabu (yananasibishwa na Uislamu) na majina ya Kizungu (yananasibishwa na Ukristo). Huu ni umbilikimo wa fikra ambao ni mbaya sana.

Plz Be a greater thinker! THINK LOUD & OUT OF THE BOX.

Bazazi ni Bazazi!
 
Bob Nyanga Makani,Mwenyekiti wa pili na Katibu Mkuu wa kwanza wa CHADEMA,amefariki dunia jana.Ninaomoyo mnyenyekevu kuwapa pole wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine na msiba huu mkubwa.Mungu awape ustahamilivu na ujasiri mkubwa.Bwana alitoa,Bwana ametwaa...jina lake LIHIMIDIWE! Amina.

Hayati Bob Nyanga Makani alikuwa wa kipekee.Pamoja na kuwa Mwanasheria(baadaye Wakili wa Mahakama Kuu tangu tarehe 4/4/1986 na kupewa Nambari 131 ya Uwakili),alikuwa ni Naibu Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania.Baadaye,kutokana na kutoridhishwa na utendaye Serikalini,Bob Nyanga Makani akishirikiana na wanamageuzi wengine chini ya Edwin Isaac Mtei,walianzisha CHADEMA mwaka 1992 naye kuwa Katibu Mkuu wa kwanza.

Neno 'Bob' humaanisha,pamoja na vitu vingine,kutikisa(hasa kichwa) kuanzia chini kwenda juu.Huonyesha usikivu wa kufuatilia na kukubaliana na jambo la msingi linaloelezwa.

'Nyanga' katika lugha ya Nyanja ya pale Zambia(ambayo hufanana na lugha nyingine za kibantu hapa kwetu) humaanisha pembe ya ndovu.Hii inaonyesha kuvuma na kuwa maarufu sana.Yeye pia alikuwa hivyo.

'Makani' kwa Kinyanja hichohicho,humaanisha upinzani wa kimaneno au kimatendo.Hapa sina haja ya kutoa maelezo marefu.Kila mtanzania anajua.Alikuwa mpinzani wa kweli.

Huyo ndiye Bob Nyanga Makani.Pumzika kwa amani Wakili Msomi na Mpambanaji 'Msikivu Mvumaji Mpinzani wa kweli'...


Good analysis.
 
Unaonaje wewe ukitafsiri hilo jina MOHAMED maana yake nini? Tusijiingize katika mgogoro wa kidini bila sababu ya maana?
Bahati mbaya Bazazi haamini jina linabeba IMANI yake (dini). Kwangu kuna majina ya Kiarabu (yananasibishwa na Uislamu) na majina ya Kizungu (yananasibishwa na Ukristo). Huu ni umbilikimo wa fikra ambao ni mbaya sana.

Plz Be a greater thinker! THINK LOUD & OUT OF THE BOX.

Bazazi ni Bazazi!

Mleta mada ndio anatakiwa atoe tafsiri, sio anaruka majina ya mtu. Mohammed.
 
Kifupi BOB ni jina lake la skuli na kiulaji. Lakin jina lake la asli alopewa na wazazi wake ni Mohammed.
Kumbukeni zamani kulikuwa na jila skuli (kama ukirudia darasa unabadili jina) na jina la kuzaliwa na kupewa na wazazi.

Inna Lillah wainna Illaihi Rajihunna.
 
Kwa Wamarekani Bob ni Robert. Mbona zile sifa zingine za huyu Mzee hazisemwi? Yeye na Jaji Waryoba wawezadhani ni ndugu!
 
Huyu dada nilisikia story yake nisingependa niiweke humu, aliolewa na mtoto wa Iddi Simba kuna kitu kuhusu Dini yake alikifanya baadae kilimletea shida , ulizia vizuri ndugu yangu.

Ameolewa na Said Iddi Mohammed Simba na kama utabaini aliyekuwa mshenga ni Eng Abdullah Saleem Al harthy ambaye alikuwa classmate wa Iddi Simba na rafiki mkubwa sana wa Bw Mohammed Makani. Mimi nilikuwepo kwenye harusi hiyo.
 
Ndugu yangu JF sio sehemu ya porojo kitu kama hujui kitu kaa kimya! Hivi mtoto wa marehemu Bob Makani, Mohamed Makani akisikia hii kauli sidhani kama atajisikia vizuri kweli.

Siku zote si mnasema Chadema ni chama cha kanisa katoliki? sasa Makani anakuwaje muislam? Mi siku zote najua Bob Makani ni Mkatoliki kutoka Kaskazini.
 
Back
Top Bottom