BOB MAKANI na uhalisia wa JINA LAKE...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Bob Nyanga Makani,Mwenyekiti wa pili na Katibu Mkuu wa kwanza wa CHADEMA,amefariki dunia jana.Ninaomoyo mnyenyekevu kuwapa pole wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine na msiba huu mkubwa.Mungu awape ustahamilivu na ujasiri mkubwa.Bwana alitoa,Bwana ametwaa...jina lake LIHIMIDIWE! Amina.

Hayati Bob Nyanga Makani alikuwa wa kipekee.Pamoja na kuwa Mwanasheria(baadaye Wakili wa Mahakama Kuu tangu tarehe 4/4/1986 na kupewa Nambari 131 ya Uwakili),alikuwa ni Naibu Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania.Baadaye,kutokana na kutoridhishwa na utendaye Serikalini,Bob Nyanga Makani akishirikiana na wanamageuzi wengine chini ya Edwin Isaac Mtei,walianzisha CHADEMA mwaka 1992 naye kuwa Katibu Mkuu wa kwanza.

Neno 'Bob' humaanisha,pamoja na vitu vingine,kutikisa(hasa kichwa) kuanzia chini kwenda juu.Huonyesha usikivu wa kufuatilia na kukubaliana na jambo la msingi linaloelezwa.

'Nyanga' katika lugha ya Nyanja ya pale Zambia(ambayo hufanana na lugha nyingine za kibantu hapa kwetu) humaanisha pembe ya ndovu.Hii inaonyesha kuvuma na kuwa maarufu sana.Yeye pia alikuwa hivyo.

'Makani' kwa Kinyanja hichohicho,humaanisha upinzani wa kimaneno au kimatendo.Hapa sina haja ya kutoa maelezo marefu.Kila mtanzania anajua.Alikuwa mpinzani wa kweli.

Huyo ndiye Bob Nyanga Makani.Pumzika kwa amani Wakili Msomi na Mpambanaji 'Msikivu Mvumaji Mpinzani wa kweli'...
 
Jina lake ni Mohamed Makani. nakumbuka ana wadogo zake Issa, Marhum Mariam na mwingine Hassan.
 
Bob = Robert

Nyanga = Masomo magumu pale UDSM - Uhandisi

Makani = kiburi zaidi ya 'nhinda'.

Makani ni wingi wa nghani. ni aina fulani ya kiburi walichonacho watu wa kanda ya Ziwa ambacho ndo kinawatesa ccm mpaka kesho. kiburi hiki ni kibaya kwa sababu mtu mwenye kiburi cha aina hiyo huwa hataki tena kukubali unachomuambia hata umshawishi vipi. mtu mwenye nghani humpinga hata baba/mama yake ... kwa miaka mingi ccm imekuwa kama mzazi wa taifa hili, hasa enzi za Mwalimu Kambarage. watu wamekitii, wamekiheshimu, wakiamini kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi. enzi na enzi. lakini baada ya nyerere kufa, falsafa nzima ya ccm imekufa. limekuwa pango la walanguzi. wasanii. mchwa.

Time to show them the plural form of nghani, Makani! mwanzo mwisho mpaka mtang'oka.

R.I.P. Robert.
 
Spelling kidogo mkuu, ni Ng'hani siyo nghani. Neno Ng'hani kwa kisukuma halina uwingi, hivyo Makani siyo uwingi wa ng'hani hata kidogo. Na hilo neno/jina (Makani) halina maana ya kiburi hata kidogo!
 
BOB ni kifupisho cha jina ROBERT, sielewi kwa nini anafahamika kwa jina hilo ila jina lake ni MOHAMED BOB NYANGA MAKANI.
 
BOB ni kifupisho cha jina ROBERT, sielewi kwa nini anafahamika kwa jina hilo ila jina lake ni MOHAMED "BOB NYANGA" MAKANI.
 
Hivi mbona mnataka kuleta uhuni kwenye majina ya watu sijui kwa nini hamtaki kuliweka jina lake la Mohamed..
 
Bob = Robert

Nyanga = Masomo magumu pale UDSM - Uhandisi

Makani = kiburi zaidi ya 'nhinda'.

Makani ni wingi wa nghani. ni aina fulani ya kiburi walichonacho watu wa kanda ya Ziwa ambacho ndo kinawatesa ccm mpaka kesho. kiburi hiki ni kibaya kwa sababu mtu mwenye kiburi cha aina hiyo huwa hataki tena kukubali unachomuambia hata umshawishi vipi. mtu mwenye nghani humpinga hata baba/mama yake ... kwa miaka mingi ccm imekuwa kama mzazi wa taifa hili, hasa enzi za Mwalimu Kambarage. watu wamekitii, wamekiheshimu, wakiamini kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi. enzi na enzi. lakini baada ya nyerere kufa, falsafa nzima ya ccm imekufa. limekuwa pango la walanguzi. wasanii. mchwa.

Time to show them the plural form of nghani, Makani! mwanzo mwisho mpaka mtang'oka.

R.I.P. Robert.

Hivi wewe ni mtoto wa marehemu? Mbona unataka kupotosha majina ya watu...kwa hiyo Mohamed sio jina lake?
 
Back
Top Bottom