Bob Amsterdam ni Mamluki; Watanzania tuweni macho sana

Kwahiyo makamanda siku hizi mna fashion mpya; kila kamanda ana mercenary wake?
Mbona meko ana mamluki wake kutoka Burundi husemi?? Na wewe pia ni mamluki wa meko kwa njia moja au nyingine na so far hujui unachotetea uko kushabikia zaidi

Go back to school
 
Mbona meko ana mamluki wake kutoka Burundi husemi?? Na wewe pia ni mamluki wa meko kwa njia moja au nyingine na so far hujui unachotetea uko kushabikia zaidi

Go back to school

Do you seriously want me to go back to school? Enjoy cover ya JF. Jukwaa zuri sana hili; linamwezesha hata ambaye hakusoma kumuambia msomi hajasoma! What else can you ask for?
 
Watanzania wenzangu, napenda kutoa angalizo muhimu sana. A political mercenary is a gun for hire!

Tufanyeni makosa mengine yote tunayoweza kufanya, lakini shime shime tusije tukaingia kwenye mtego wa kuruhusu matumizi ya mamluki kwenye chaguzi zetu!

Ni kawaida ya mamluki yeyote kukosa utiifu kwa nchi alikokodiwa kuendesha shughuli zake za mamluki. Yeye hasimamii maslahi ya nchi husika. Utiifu wa mamluki ni kwa mteja wake. Period.

Ukiingia kwenye mtego wa kuruhusu matumizi ya mamluki, umeingia kwenye shimo refu na lenye utelezi mbaya. Kumbuka, Robert Amsterdam sio political mercenary pekee aliyepo duniani. Wapo wengi.

Let’s assume nchi imeingia kwenye huu mtego na Bob Amsterdam amefanikiwa kumueka mteja wake madarakani. Huu sio mwisho wa ngoma ya aina hii. Ni ngoma ya watu wazima; inakesha! Huu utamaduni ukishajengeka, baadaye mwingine mwenye uchu wa madaraka, kama yule wa kwanza, naye atatafuta mamluki wake na before we know it, we’re back to the drawing board. Je, huu ndio utamaduni tunaotaka kuujenga? Tutakuwa nchi ya aina gani hiyo?

Utamaduni wa kukubali matumizi ya political mercenaries ni utamaduni unaopaswa kuogopwa kama ukoma. Tusije tukadhani mwaka jana U.S. Congress ilipochukua hatua ya kumuondoa madarakani Bwana Trump kwa makosa mawili, likiwemo la kuwatumia Urusi ili ashinde uchaguzi, ilifanya hivyo kujifurahisha. Wanatambua risk kubwa ya kuruhusu matumizi ya foreign powers kwenye chaguzi zao!
angekua upande wenu angekua mhisani,mshirika na rafiki lakini akiwa upande wa pili ni mamluki?
 
angekua upande wenu angekua mhisani,mshirika na rafiki lakini akiwa upande wa pili ni mamluki?

Sio kawaida kwa nchi yoyote kuwa na foreign actors kwenye chaguzi zake. Watu wasiokuwa waadilifu wanaifanya hii nchi kuwa shamba la bibi!
 
Una ushahidi gani kuhusu kupigwa risasi ulikua ni mpango wa CCM?

Ok hata kama CCM imehusika kwenye sakata la shambulizi hilo kama anavyodai Lissu, ndio aingie mkataba na mabeberu na makaburu kwa kuhamasisha maandamano yasiyokua na kikomo kitu ambacho kitaleta vurugu na kuondoa amani nchini, hatimaye nchi iuzwe kwa mabeberu na makaburu ??!! Mm naona Lissu sio mzalendo kabisaa na nchi yake.

Watanzania tuamke, kwa kukosa umoja na mshikamano tunajikaanga kwa kutumia mafuta yetu wenyewe.

Tukumbuke, mfumo wa vyama vingi umeletwa na wazungu huku Africa wakijua fika siku moja tutashindwa kuelewana na tutaishia kuuana wenyewe kwa wenyewe. Wakiona mnauana wenyewe kwa wenyewe mabeberu na makaburu yataingilia kati, yakishaingilia kati hayo majasusi mtafurahia show.

Kifupi hao mnaowaita wasaidizi watetezi wa haki wakishaingia madarakani chini ya kibaraka wao Tundu Lissu ndio mtaelewa wazungu hawafanyagi kazi ya bure isiyokua na maslahi.

Vyama vya upinzani na wafuasi wake igeni mfano huu:

USA na UK kuna upinzani mkali sana wa vyama vya kisiasa, vinaumana weee wakati wa uchaguzi mpaka,,, ila matokeo ya uchaguzi yakishatoka wanashikana mikono, wanaungana pamoja kufanya maendeleo.

Husikii nchi hizo wakiomba msaada kutoka nchi nyingine eti sababu hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa Rais.
Yaliyotokea huko Tanzania uliwahi yasikia yakitokea kwenye hizo nchi ulizofanyia refernce?
Pathetic
 
Robert Amsterdam Babu zake ndio waliowafanya Babu zetu watumwa, waliwaambia eti hawana uwezo wa kujitawala.

Sasa hao hao ndio wametuletea demokrasia na sasa wanataka tujitawale.

Huu upendo wa ghafla umetokea wapi?
Bora utawala wa wakoloni kuliko huo utawala wa ccm, siku wananchi wakiona kuna watu wanataka kuwatwanga lazima watawaunga mkono maadui zenu
 
Bora utawala wa wakoloni kuliko huo utawala wa ccm, siku wananchi wakiona kuna watu wanataka kuwatwanga lazima watawaunga mkono maadui zenu

Kama mali ya urithi isivyokuwa na uchungu, uhuru uliopiganiwa na babu zako nao hauna uchungu. Ndiyo maana unatamani utawala wa wakoloni.

Kama babu yako alikuwepo wakati wa utawala wa mkoloni na bado yuko hai, kampe huo msimamo wako kisha utupe mrejesho!
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom