Boarding Schools- Kunani??

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
356
Naamini wengi wa wana JF mtakua mko aware na mambo mengi nitakayoyaongelea hapa kwa kuwa mmeyaexperience huko mashuleni mliposoma. Cha kushangaza ni kwamba hakuna mtu anaetaka kuyaongelea - si viongozi wa serekali, si walimu, si wana JF, nahisi watu wanaona tu kuwa ni part and parcel ya process nzima ya elimu. Nitalenga zaidi kwenye mashule ya boarding ambako kama wengi- nilisota huko kwa miaka sita.

Suala nyeti kabisa ambalo naona linaendelea kuwa ignored na serekali na wakuu wa mashule ni “Health and Safety” .Nilitegemea kwamba baada ya maafa ya Shauritanga mwaka 1994 ambapo wanafunzi 41 walipoteza maisha yao labda kungekua na mabadiliko na new legislations za kutoa guidelines kwa wakuu wa mashule zingetungwa. Lakini hadi leo kuna wanafunzi bado wanafungiwa mabwenini mida ya usiku hasa kwenye shule za wasichana. Ni mabweni ya shule ipi yana Fire escape routes leo hii? Fire extinguishers utazikuta Staff rooms tu, mabwenini hakuna kitu. Chemli, mishumaa na koroboi ambavyo ni main recipes za fire disasters bado vinaendelea kutumika mabwenini mida ya usiku, hasa kwa shule za vijijini- ndio maana kila siku mashule yanaungua lakini no one is doing anything!

Utakuta shule iko kijijini sana na mbali kabisa na mji, haina kituo cha afya na mbaya zaidi haina hata baskeli achilia mbali gari- lakini cha kushangaza serekali inakubali kuisajili.Mwanafunzi akipata maradhi au injuries ambazo ni serious usiku its very likely kwamba atakufa! Kwanini kusingekua na minimum standards ambazo shule inatakiwa ku achieve kabla ya kupewa kibali? Sehemu nyingine wanafunzi wanatumia muda mwingi kusaka maji kuliko muda wanaotumia darasani, cha kushagaza ukiwa mchafu kwenye ukaguzi utamtambua mwalimu wa zamu!!

Bado karne hii wanafunzi wa shule nyingi za boarding wanatumia dekio la ‘tambara’, hakuna cha gloves wala mop! Wakati nipo kidato cha pili, corridor ya darasa langu ilikua karibu sana na ’assembly’ ground na naweza sema labda wanafunzi zaidi ya mia 300 walikua wakiitumia corridor hiyo kwenda ‘mstarini’ lakini kila siku there must be a 14 or 15 years old poor boy crawling on his knees to get it cleaned and it used to be worse kipindi cha mvua, dongo la Moshi huwa linapenda kudandia soli! Sasa hebu jiulize hao wanafunzi wengine wanaopita hapo wamekanyaga nini na viatu vyao? Hapo kuna vinyesi , mikojo, and all sort of horrible creatures na huyo dogo ana ndoo na tambara lake tu na kusipodekiwa atakiona cha mtema kuni. How much does it cost to buy a mop and a bucket kwa kila darasa? Huko vyooni ndo usiseme kabisa, kunahitajika cleaning chemicals-lakini naona this will be asking for much. Mbaya zaidi choo kikiziba,kwa kuwa hakuna alternative watu wanajazia humohumo tu- By the way adha ya choo nilikutana nayo hata nilipokuwa mlimani UDSM- vyoo vile vya kukaa viliwekwa kipindi hicho ambacho wanafunzi walikua wachache,chumba kimoja-mtu mmoja na sio sasa chumba kimoja watu nane, as a result hakuna mtu anaekaa kwenye toilet seat siku hizi, watu wanapanda kwenye seats (natamani ningekuchorea hapa!)

Sikujua kama bullying ni tatizo hadi nilipokuja ulaya coz nilikua na mimi nina mtazamo wa wengi kwamba its part and parcel ya hizo shule za boarding. Utanyanyasika ukiwa form one then ukifika form two kibao kina change na wewe unaanza kuwatesa ’njuka, ndama’ wanaofuatia . I must say, I was a strong lad na I got away with it but ukweli ni kwamba mambo wanayofanyiwa form one huko mabwenini- they are horribly shocking! Na kibaya zaidi they are scared to report them kwa walimu. Dogo mmoja alitumwa akamletee maji ya kunywa mbabe mmoja, alipokataa mbabe yule akatoka kimyakimya na baada ya muda akarudi na kigeleni cha lita tano kikiwa kimejaa maji-“Si umekataa kunipa maji? niimekuletea wewe mheshmiwa na uyanywe”,aling’aka mbabe huyo huku akimtizama kwa usongo, dogo aliyanywa hadi ikabidi wababe wengine waingilie kati kumuokoa otherwise angepasuka tumbo! Ilikua ni kawaida kuamshwa usiku wa manane na kulazimishwa kuimba wimbo wa taifa.Ilifikia kipindi hadi wazazi walikua wakihamisha watoto wao kwenye baadhi ya mashule. Naamini wakuu wa mashule wanaweza kuwa taratibu nzuri zaidi za kukabiliana na tatizo hili na na hili linahitaji maelekezo toka wizarani?

Itakua dhambi nisipoongelea issue nyeti hapa- MSOSI coz najua hiki ni kilio cha wengi. Migomo mingapi imekua triggered na suala la chakula mashuleni? Ukiliingia darasani mwalimu anahubiri kuhusu balanced diet lakini unapoingia dinning hall unagundua kuwa mwalimu alikua akiongelea ndoto tu. Ninaamini kabisa kwamba mkuu wa shule yang alikua anapata fungu linalotosha kutulisha vizuri (and were not actually asking for anything rather than variety na sio hiyo balanced diet coz naona bado ni ndoto huko mashuleni!) Hivi kweli ni haki kulishwa ugali na maharage kwa term nzima (usiku na mchana) na maharage yenyewe yameungwa kwa chumvi tu, wadudu kibao!and you can tell mnunuzi alipoenda sokoni alichagua yale ya bei rahisi kabisa. Hapo asubuhi breakfast ni uji usiokuwa na sukari wala mafuta (popularly known as sumu, sifongo). I also learned about a huge conflict of interest coz Headmaster mwenyewe ndo alikua supplier wa misosi, kuni alikua anakata miti ya hapohapo shuleni na alikua akitumia lori la shule kwenye ma deal yake yote hayo. Utaona tu kwamba yeye alikua anamaximise profit bila kujali maslahi ya wanafunzi na kwa kuwa shule ilikua huko kijijini na tulikua tunamuogopa (kama sio kuogopa kufukuzwa shule!)- he simply got away with it!

Nilisoma shule za boys only lakini Im well aware of matatizo wanayoyapa dada zetu kwenye mashule ya wasichana tu au mchanganyiko, kubwa zaidi likiwa ni sexual harassment and abuse toka kwa walimu na most of the time wanakuwa hawana choice zaidi ya kukubaliana na matakwa ya walimu. Wakatae? Utapewa miadhabu kibao au kuishia kuwa suspended au kufukuzwa kabisa, na usitarajie kufaulu somo la huyo mwalimu kabisaaa!

Sijui kama waziri wa elimu anachunguliaga humu, lakini nawaombeni wana JF wenzangu muweke personal experiences zenu hapa ili tuwasaidie wadogo zetu na watoto wetu, things can be done, things can still be improved- I believe so.

Wasalaam,
Kana Ka Nsungu
 
Back
Top Bottom