Board ya mikopo kukata 8% za mishahara ya wadaiwa

OTL

Member
Nov 22, 2012
39
3
Board ya mikopo wanakata 8% ya mshahara kama lejesho la deni kwa walionufaika na mikopo,
ninachokiona mimi wanafunzi wananufaika kwa kiwango tofauti, kuna wenye asilimia mia adi sifuri, na kuna wanaosoma miaka 3 adi 4.
Mkopo nijuavyo mwenye deni kubwa ndio analipa kiasi kikubwa, kwa kuweka 8% kwa wote ninaona kama sio fair, ukizingatia na mishahara ni tofauti.

Sijui wana jf mnaonaje wezangu
 
Kama deni lako dogo si utamaliza mapema kwani tatizo lipo wapi?on top of that 8% bado ni resonable amount.
 
Board ya mikopo wanakata 8% ya mshahara kama lejesho la deni kwa walionufaika na mikopo,
ninachokiona mm wanafunzi wananufaika kwa kiwango tofauti, kuna wenye asilimia mia adi sifuri, na kuna wanaosoma miaka 3 adi 4,
mkopo nijuavyo mwenye deni kubwa ndio analipa kiasi kikubwa kwa kuweka 8% kwa wote ninaona kama sio faer, ukizingatia na mishahara ni tofauti.
sijui wana jf mnaonaje wezangu
mbona kidogo sana 8% mimi nashauri iwe 50% ya mshaara iliishe mapema
 
huu ni mkopo so ulipwe kulingana na nn umekopa sio kukatwa tu, ni resoanable amount lakini kumbuka hii watakukata miaka mingapi, na mshahara ukiongezeka na wenyewe inaongezeka, kuna wazuri wakuweka record za mtu alichotoa. maana unaenda hata pale nssf unakuta huna ata sent tano na umechangia mwaka sasa ni bora ikawa fixed amount then unajua baada ya miaka mingapi deni litaisha.
 
Pamoja na mleta mada kutoweka vielelezo vya kufanya hiyo taarifa isiwe ya kutunga, bado nina machache ya kuchangia.

1. Kwanza hiyo 'mikopo' ni jasho la walipa kodi, hivyo ni haki ya wanafunzi kunufaika nayo, kwani elimu hiyo ni kwa manufaa ya umma kwa njia moja au nyingine.

2. Kama lengo la kukata 8% ni kutunisha mfuko ili kupanua wigo wa watakaonufaika na huo mfuko, kwa hilo ni sahihi sana.

3. Hofu yangu ni pale mfuko unapotumika kuwalipia watoto wa wakubwa kwa 100% wakati watoto wa walala hoi wakipigwa danadana. Ikumbukwe wakubwa hao hao walisomeshwa bure na leo wanataka watoto wao wasomeshwe bure na serikali wakati wameficha mamilioni ambayo yangeweza kuwalipia watoto wao .
 
Kama wanakata 8% hiyo ni ndogo saana. Nashauri wangekata 12% au 15% ili vijana wengi zaidi waweze kusoma kwa hii mikopo.
 
hawa jamaa si walisema wanafungulia kesi wale wote ambao watakuwa wame default kulipa na waliweka na dead line kabisa, sasa mbona sijaskia tena kama wameshawapeleka mahakamani?
 
Hawa jamaa mbona hata kumbukumbu zao si sahihi? WWarekebishe kwanza kumbukumbu zao ndiyo tutoe michango yetu ya namna ya kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi.
 
Mfano kwa mwenye gross ya tshs 500000 anatakiwa kulipa 40,000 kwa mwezi parefu
kwani kabla ya iyo 8% walikuwa wanalipa ngapi?
 
Board ya mikopo wanakata 8% ya mshahara kama lejesho la deni kwa walionufaika na mikopo,
ninachokiona mimi wanafunzi wananufaika kwa kiwango tofauti, kuna wenye asilimia mia adi sifuri, na kuna wanaosoma miaka 3 adi 4.
Mkopo nijuavyo mwenye deni kubwa ndio analipa kiasi kikubwa, kwa kuweka 8% kwa wote ninaona kama sio fair, ukizingatia na mishahara ni tofauti.

Sijui wana jf mnaonaje wezangu
Mi naona ni sawa tu kwani unamaliza deni kwa haraka na kuendelea na mipango mengine ya maisha.
 
hawa jamaa si walisema wanafungulia kesi wale wote ambao watakuwa wame default kulipa na waliweka na dead line kabisa, sasa mbona sijaskia tena kama wameshawapeleka mahakamani?

ilionekana idadi kubwa ya watoto wa vigogo ndio waliojaa kwenye listi ikaachwa! halafu inatakiwa kila mtu aliyesoma na ana kazi awe anakatwa maana hawa waliosoma zamani bure wao wana excuse gani ya kusoma bure?
 
jamaa wapo makini, waliochelewa wote 10% adhabu, majembe ndo wanafanya hiyo kazi .
 
Board ya mikopo wanakata 8% ya mshahara kama lejesho la deni kwa walionufaika na mikopo,
ninachokiona mimi wanafunzi wananufaika kwa kiwango tofauti, kuna wenye asilimia mia adi sifuri, na kuna wanaosoma miaka 3 adi 4.
Mkopo nijuavyo mwenye deni kubwa ndio analipa kiasi kikubwa, kwa kuweka 8% kwa wote ninaona kama sio fair, ukizingatia na mishahara ni tofauti.

Sijui wana jf mnaonaje wezangu

Kwa mtu ambaye anakatwa this percent atakuwa anaelewa maumivu yake,kiukweli sio fair kuweka fixed rate kuwa 8% wakati salary za watu zinatofautiana sana.Wangeweka rate tofauti depending na salary ya mhusika kwa vile unakuta mtu ana zaidi ya mkopo mmoja which means anazidi kuongezewa burden zaidi.Nakubaliana na hoja yako mia.
 
Wamechelwa sana...sijui walikuwa wanafanya nini wengine tunakaribia kustaafu kabisa na kufanya kazi zetu binafsi!
 
Basic salary - (income tax +pension contribution + tuge +high student lb +nat health insurance fund +parastatals rent)= 0

hahahaaa, pole sana mkuu ndo tz hii
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom