BND YAMFUNGA JELA MIAKA 8 KWA KUUZA SIRI ZAKE KWA CIA

Complex

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
4,118
4,765
Afisa wa zamani wa shirika la kijasusi la Ujerumani (BND) amekiri kuuza mamia ya nyaraka nyeti sana kwa shirika la kijasusi la Marekani (CIA). Pia alikiri kuwa alijaribu kufikia shirika la kijasusi la Urusi (FSB). Aliiambia mahakama kuwa kilichompelekea kufanya hivyo ni sababu alikosa morali kazini na alijihisi kutoonekana mwenye thamani ndani ya shirika hilo la BND.

Markus Reichel, 32, alihukumiwa na mahakama Munich kwa miaka nane jela siku ya Alhamisi akishtakiwa kwa kuuza zaidi ya nyaraka 200 za siri kwa CIA, na pia kujaribu kuuza nyaraka 3 kwa shirika la ujasusi la Urusi.

Reichel aliajiriwa katika Shirika la Ujasusi la ujerumani (BND) katika kitengo cha utawala kati ya mwaka 2008 na Julai 2014, ambako alifanya kazi katika mailroom. Kwa mujibu wa taarifa Markus alikuwa kibali kushughulika na nyaraka na taarifa za siri za juu kabisa.

Reichel alikiri yeye aliuza nyaraka na taarifa za ndani kwa CIA kwa malipo ya $ 107,000. Yeye aliiambia mahakama kwamba alijisikia ambaye hana thamani na wa kupuuzwa, na kwa hiyo alitaka maisha yake kubadilika.

"Hakuna mtu ndani ya BND aliyeniamini mimi kwa kitu chochote, Wakati kwa CIA ilikuwa tofauti," Reichel alisema. Pia wamarekani (CIA) walikuwa wananipa adventure.
Reichel alikuwa katika mshahara ngazi ya chini, alikuwa akilipwa $ 1,400 kwa mwezi. Na CIA hawakuwa wakimpa mshahara mkubwa sana, walikuwa wakimpa kati ya $ 12,000 na $ 22,000 kwa mwaka, ambapo makutano yao ya kupeana pesa hizo yalikuwa ni katika nchi ya Austria.

"Nilitaka kitu kipya, uzoefu na kitu chenye kusisimua," alinukuliwa akisema na shirika la utangazaji la AFP.
 

Attachments

  • upload_2016-3-18_19-5-53.png
    upload_2016-3-18_19-5-53.png
    328 bytes · Views: 43
Yaani hawa wajerumani vipi tena, yaani mtunza siri za juu kabisa wanamlipa kama 2m za kibongo. Anazidiwa mshahara hata na karani wa bandari wa hapa bongo. Ndio maana visimu vya wakubwa wao vinadukuliwa kiurahisi kabisa.
 
Good thing about white though might not be them all,they always speak their hearts out so its just up to you! He going to serve the time,but atleast he is okay with it.
 
Back
Top Bottom