Bmw Jitokeze Kujibu Tuhuma Zako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bmw Jitokeze Kujibu Tuhuma Zako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ipole, May 4, 2008.

 1. I

  Ipole JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kutokana na tuhuma nyingi amabazo zimekuwa zikielekezwa kwako nawewe kukaa kimya bila ya kujibu lolote inatutia mashaka wananchi wenzako.

  Madai ambayo yanatolewa juu yako ni mengi muno tumeambiwa kuwa umeitumia ikulu kufanya biashara lakini kama hiyo haitoshi, Tukambiwa kuwa una hisa kiwanda cha kiwira na baadaye tunambiwa kuwa ulimbeba karamagi kwa kumuongezea muda wa mkataba wa kampuni yake.

  Kwa maana hiyo basi bila shaka ulikuwa na maslahi katika kampuni hiyo. Juzi natoka arusha wakati tupita mombo ikazuka hoja yako, Na kijana mmoja akesema kwamba unayo Hoteli kubwa ya kitalii huko Lushoto.

  Na kwamba una mpango wa kujenga reli ya waya kwa ajili ya kuwachukua watalii kutoka kituo kitakachojengwa hapo mombo, na kuwapandisha watalii kwenye Hoteli yake iliyoopo huko Lushoto.

  Lakini pia kama hiyo haitoshi inasemekana mama mkapa alinunua jengo lililopo Ilala lililokuwa linamilikiwa na shirika la Posta kwa njia za panya.

  Na baadaye kuliuza kwa mfanya biashara wa Mwanza wakati huohuo kuna jengo lililokuwa linamilikiwa na iliyokuwa NBC, Lililoko katika njia panda ya Morogoro na Jamuhuri ambalo pia inasemekana linamilikiwa na mama Mkapa.

  Kwa maana hiyo basi ni wakati muafaka sasa kwa bwana BMW kuyaweka wazi mambo haya. naomba kuwasilisha
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  May 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  sasa aombwe atokeze mara ngapi ? serikali ndio yenye mamlaka ya kumtaka ajibu hizo tuhuma na sio wewe au yule , huyu sasa ni mwananchi huru kama wengine kama mikataba aliandika wakati akiwa serikalini kwahiyo serikali hiyo imeshapita muda wake na haina chake sasa hivi
   
 3. I

  Ipole JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anachotakiwa kueleza ni kukubali au kukataa ni kweli raia sas anapokaa kimya maanake yanayzungumzwa ni kweli
   
 4. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..shy,

  ..tumia busara kidogo. ulikuwa hauna haja ya kumtetea che-nkapa katika hili kwani yote aliyoyafanya yanafahamika na watu wanatoa dukuduku zao tu.

  ..utetezi wako usio na mipaka unawafanya watu wajiulize,"wewe una maslahi gani na hawa?"

  ..kwa taarifa,hata viongozi wa dini wametoa maoni yao kuwa huyu jamaa ajibu hizi tuhuma kwani kukaa kwake kimya kunawafanya watu wengi waamini kuwa ni za kweli[ingawa tunajua ni za kweli!].

  ..hizi issue zimekaa vibaya sana.utetezi mtupu[usio na hoja]hausaidii.

  ..wakati mwingine,ni busara kukaa kimya!
   
 5. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2008
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Watu hawaingii kwenye PAYROLL ya mafisadi kirahisi namna hii, Unajidanganya ukidhani unatudanganya. Bora ukawapigie magoti maana pesa za wizi bado wanazo, Ongeza bidii!!

  Toka lini $erikali imechukua hatua dhidi ya mafisadi bila ya whistleblowers kupiga kelele??!!
   
 6. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..my bet is,hatojitokeza kuzungumza! why?,atakuwa amefungulia floodgate la majadiliano katika vyombo vya habari juu yake!

  ..it'll be suicidal!
   
 7. n

  nat867 Member

  #7
  May 4, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nasikia Anna Mkapa Alinunua mtaa mzima huko moshi, na ilala nasikia hotel ya lamada.
  Hivi wanajisikiaje kuwa matajiri katikati ya maskini wanaoshindwa kumudu nusu na robo ya sukari?
  Gazeti la SANI la wiki hii limemchora katuni nzuri mkapa na mkewe wakiwa kitandani(theme:ububu).
   
 8. n

  nat867 Member

  #8
  May 4, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nasikia Anna Mkapa Alinunua mtaa mzima huko moshi, na ilala nasikia hotel ya lamada.
  Hivi wanajisikiaje kuwa matajiri katikati ya maskini wanaoshindwa kumudu nusu na robo ya sukari?
  Gazeti la SANI la wiki hii limemchora katuni nzuri mkapa na mkewe wakiwa kitandani(theme:ububu).
   
 9. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mkuu Shy

  Hivi kwa nini usirudishe hile picha ya zamani ya kidini uliyokuwa unatumia. Maana ilikuwa inakufanya unafikiria sana. Siku hizi umebadilika kweli hata nashidwa kuamini kama ni wewe. Au umeibiwa password zako nini.
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Si tunaambiwa serikali ni watu? Si tunaambiwa viongozi wa serikali ni vijakazi wetu, wanaotakiwa kutekeleza matakwa yetu? Sasa kama watu wengi wanataka Mkapa ajibu tuhuma mpaka unauliza "aombwe atokeze mara ngapi" then hiyo inaongezea nguvu case ya Mkapa kujibu.

  Hii top down approach (serikali iwe controlled na viongozi na sio wananchi) ndiyo imetufikisha hapa.Kwa sababu sehemu yoyote ukiwapa control watu wachache bila ya kuwawajibisha watu hao wata abuse control kwa manufaa yao binafsi.

  Kuna wimbo mmoja wa Fela Anikulapo Kuti unaitwa "Confusion Break Bone" anamsema rais wa Nigeria Shehu Shagari kwa kuiba mihela na kukaa kimya, anawashambulia wanajeshi na mahakama kwa kuiba na kukaa kimya.We need a million Felas to sing the grotesque and unethical misconducts of Benjamin Mkapa.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkapa kishageuka kuwa bubu asiyetaka kusema.
  Anafura tu huko nyumbani kwake na kugonga meza kwa hasira na kuongeza kilauri cha wiski!
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Masikini ya Mungu! Kuna mtu aliwahi kusema kuwa kwenye huu msafara pia tunao vibaraka wao mafisadi!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Serikali siyo yenye mamlaka ya kumtaka ajibu tuhuma dhidi yake, bali Watanzania waliomchagua ndio wana wajibu huo. Hata kama awamu yake imekwisha bado anastahili kujibu tuhuma zozote dhidi yake kwa yale aliyoyafanya akiwa madarakani.

  Kama serikali inanyamaza kimya ama kwa kumlinda fisadi Mkapa au kwa kuogopa kwamba 'nchi italipuka' basi Wananchi tuna kila sababu ya kupiga kelele kila kukicha ili Mkapa ajibu tuhuma hizo. Hatukumchagua ili atumie madaraka yake kujitajirisha kwa njia za kifisadi, bali tulimchagua ili alete maendeleo kwa Watanzania wote wanaoishi mijini na vijijini.
   
 14. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Mkuu wakiondoa immunity tuu..atatoka mwenyewe uko aliko na kujibu tuhuma....hakuna kisichowezekana chini ya jua... slowly we are getting there....ingawa speed ni ndogo sana lakini tutafika.
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,557
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Hivi hapa maswali hapa ni yapi?
  1)Anaombwa ajitokeze na kujibu tuhuma
  2)Anatakiwa ajitokeze kujibu tuhuma
  3)Tusubiri sheria ichukue mkondo wake.
  Maswali hayo hapo juu tunaweza kujiuliza. Watu wanataka ajitokeze lakini tunasahahu kuwa hizi ni tuhuma na hivyo inabidi awe makini kwenye statement zake.
  My take:
  Nafikiri hajui kuwa akanushe ama akubali ama aseme no comment..Matter fact he said nadda!
  Kusuasua huko kunatokana na ushahidi ambao ni mzito!
  Hana imani na baadhi ya wana CCM ambao ni wazi wamegawanyika huku waziri mkuu akiacha shughuli za kitaifa na kwenda kuzindua tawi la CCM huko chuo kikuu Tumaini in order to counter balance the "Mlimani effect"
  Hana imani na ndio maana hakwenda Butiama!
  Ana maadui wengi kutokana na ubabe aliokuwa nao na hivyo kusababisha mambo mengine ya ndani kwa ndani serikalini na chamani kwa ujumla aliyokuwa akiyafanya dhidi ya wenzake wakati wa scrambling for "Power and Money" na hivyo kutokea mgawanyiko ambao madhara yake ni sasa!(wanamtandao) etc.
  Kwamba sasa ubongo wao unawatuma kuwa chama ndio kiko hatarini na wala sio Taifa!
  Kwanini waziri mkuu aende akafungue tawi ilhali anahitajika kwa udi na uvumba sehemu lukuki nchini zenye matatizo ambayo hayajatatuliwa toka enzi na enzi?
   
 16. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Katika suala la Mkapa ni kula sahani moja na JK hili suala liko wazi. Huyu Mkapa anafanya uhuni tu hakuna aliyemtuma kufanya biashara.

  Uhuni wake hauna nafasi tena ktk Tanzania, nafikiri anatakiwa awe mfano hili dunia nzima ijue kuwa sasa watanzania hawana mchezo.

  Nafikiri alikuwa anajua miiko ya uongozi, tutamuomba JK amtangulize, si kwa sababu kuna mtu ana chuki binafsi naye hila ni sheria alizo hapa kuzifuata.

  Kushindwa kumfikisha mKapa mahamani ni failure ya JK kulinda katiba ya nchi.
   
 17. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2008
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Ajitokeze aseme nini? Hivi mtu akishikwa ugoni huwa unamwona anavyonywea kama kuku aliyemwagiwa maji pamoja na viroja vyake vyote. Huyu sasa ni wa kumfikisha mahakamani tu.
   
 18. M

  Mutu JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi si Kiwira inamesemekana itaanza kuchunguzwa na serikali.Sasa mnataka huyu bwana ajibu nini,kwani kukaa kimya ni jibu pia.Hata mahakamani unaambiwa una haki ya kukaa kimya au kuongea.

  Au unataka kusikia anavyokanusha?Cha msingi unatakiwa kusema tunataka serikali ikamilishe uchunguzi mapema na kama kuna chetu kirudishwe.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Kichunguzwe kipi tena kisichojulikana? :confused:
  Katika ile ripoti iliyoundwa na JK, kamati ya madini, hiyo Kiwira nayo imo humo katika ripoti. Cha ajabu ni kwamba pamoja na Mwenyekiti wa kamati hiyo kutamka kwamba ripoti imeshakamilika na wanasubiri kumkabidhi muungwana, muungwana anawapiga chennga za mwili mara yuko Uganda mara Ethiopia mara yuko Singida. Anayapa kipaumbele mambo ambayo hayastahili kipaumbele kwa sasa ukilinganisha na hili la mafisadi ambapo pia fisadi Mkapa na Yona walijimilikisha Kiwira Coal Mining katika mazingira ya kifisadi

  Kiwira irudishwe chini ya umiliki wa serikali na pesa zote walizolipwa na TANESCO hadi sasa ambapo wanatakiwa walipwe shilingi 146 milioni kwa siku zirudishwe TANESCO tena na riba na fisadi Mkapa na Yona wafunguliwe mashraka kwa kujimilikisha kinyemeka KCM.
   
 20. M

  Mutu JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Duh kazi ipo hapo ndugu!ila anaweza kufumba macho akapokea ripoti na kuwaambia mashwahiba wake jamani mambo ndio hivyo hadharani.Tatizo na yeye kama yumo kwa namna moja au nyingine.
   
Loading...