Blogs za Tanzania ziangaliwe kwa umakini mkubwa

Belight Technology

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
582
122
Sasa imeshakuwa kawaida kuona Blogs mbalimbali za hapa kwetu, Vichwa vyao vya Habari ni vya kuonekana wamefichua SIRI kwa kutafuta picha za uchi za watu na kuweka kwenye blogs zao ili kuongeza "Online Traffic" Sidhani kama inatusaidia sana na wakati tunazidi kudidimiza baadhi ya tamaduni zetu.

Mamlaka ya mawasiliano ipo, Wizara ya Habari ipo, na kila kukicha ndizo habari zao utasikia Picha za Fulani za Uchi hizi hapa... Ni nani aliyekutuma ukaonyeshe uchi wa watu hadharani? Habari za maana ziko nyingi ila nasikitishwa sana na hii kitu yani. Na kwa habari za maana mtu anamiliki blog kazi yake ni KuCopy toka vyombo vingine vya Habari na kuPaste kwake bila kufanya uchunguzi wowote au kupata taarifa kamili ilimradi kaona kwa mwandishi fulani. Ziko nyingi mpaka kero.

TUNALIPELEKA WAPI TAIFA HILI?

Hebu tujiulize.
1. Nini sababu ya wewe kumiliki blog? Je ina manufaa kwako na kwa Uma?
2. Blog yako imelenga nini? Habari, Matangazo, Biashara, au Utamaduni, Elimu au nin?
3. Vyanzo vyako vya Habari ni wapi?
4. Elimu ya yule anaepost Habari kwenye Blog ni ya kiwango gani? Anatambua Lugha ya kutumia kwa Umma?
5. Kitu gani cha kitofauti ambacho umekibuni katika blog yako ambacho kwingine hakuna?
6. Je unafuata vigezo na masharti ya habari ikiwemo sheria na taratibu zake?
 
Umeongea sahihi kaka,,inabidi kuwa na sensorship ya hizi blog,,halafu nyingi zimejaa tu mapicha ya akidada wakiwa uchi,,halafu saa zingine wanadanganya eti mwanafunzi wa chuo kikuu UDOM kapiga picha za uchi wakati amezitoa kwenye site za ngono huko nigeria...its too much.
 
Utoto tu, wakikua wataacha.
Ila kama hawajaandika kiswahili utajuaje ya tz, seva ipo urusi, hosta marekani.
 
dah... yani hawana tofauti na wanaouza viungo vya albino hawa.

Maana wanauza kwa picha za utupu za watu halafu hadi watoto siku hizi wakiwa fesibuku wanaona post zao wanazoshea, so madogo wanaenjoy tu halafu mnasema ooh mwanangu sijui nani kamfundisha tabia mbaya kumbe blogs.
 
kila muda utasikia picha za utupu zanaswa. Tena hawakawii kusema wanafunzi wa chuo kikuu wapiga picha za uchi
 
kuweka picha za uchi kwenye blogs sio tatizo hata kidogo. tujiulize:

1. kwa nini umtetee mwenye picha kwamba anadhalilishwa wakati hizo picha kazipiga na kuzitundika kwenye blog yeye mwenyewe?

2.kama kuna m2 anajihisi kadhalilishwa si aende mahakamani?

3. picha zinatundikwa wahusika wakiwa wanaongea kiswahili fasaha kabisa mtasemaje kwamba ni za wanaijeria? acheni hizo.

ANGALIZO: Nahisi mtoa hoja anaweza akawa mmoja wa watu wanaopiga picha za uchi. so, nadhani huenda ameguswa na wenye blogs kutundika picha za namna hiyo. tafakari.
 
"Blog za Tanzania" ni zipi?

Mtanzania anayeishi Marekani na kutumia Wordpress, lakini anayeandika habari za Tanzania kwenye blog yake, hii blog ni ya Tanzania?

Vipi anayeishi Tanzania na kutumia Wordpress?

Vipi Mmarekani anayeishi Marekani na kutumia Wordpress kuandika habari za Tanzania? Na anayeishi Tanzania? Au anayeishi Tanzania na kutumia servers za ISP wa Tanzania ku host blog?

Sheria inasemaje?
 
Mkuu,maswali yako kweli yana kiranga,mjibuji anapaswa kutuliza kiranga anapomjibu Kiranga!!

Nimeyapenda na nasubiri kuelimika!!!
 
tanzania ni nchi huru acha udikteta...kama kweli unakerwa na mabaya ya tanzania tuungane kukomesha ufisadi sio unaenda kukamata mateja kinondoni wakati wewe ndio unaingiza drugs

#kunjani kuti
 
Ila tuwe wakweli, tatizo pia watu wanapenda sana kuona hizi picha. We kama huendi huko wala hutajua kama zipo!!! Linakuwa tatizo kwa sababu tu siku hizi hata watoto wanajua mtandao ni nini na wanatumia, kwa hiyo zikiachiwa kwa kweli litakuwa tatizo kubwa sana kwa vijana wetu wa baadaye.
 
Naungana na kiranga katika swali lake lenye kiranga, mtoa hoja bila ya kuwa na kiranga akijibu swali hili lenye kiranga tutapata pa kuanzia bila kuonekana tuna kiranga kujaribu kufunga seva ya google au worldpress yenye clip ya mchezaji maarufu mwenye kiranga cha kuvujisha video yake ya utupu.
Mkuu,maswali yako kweli yana kiranga,mjibuji anapaswa kutuliza kiranga anapomjibu Kiranga!!

Nimeyapenda na nasubiri kuelimika!!!
 
Ndio maana blogu yetu ileee tangu asubuhi nikiingia naambiwa imeondolewa! ni fitna au ndio kakiuka maadili?
 
Mkuu,maswali yako kweli yana kiranga,mjibuji anapaswa kutuliza kiranga anapomjibu Kiranga!!

Nimeyapenda na nasubiri kuelimika!!!

Ni rahisi sana kuandika loosely "blog za Tanzania" bila kujua kwamba unapoongelea blogs unaongelea internet, ambayo haiheshimu mipaka ya nchi. Na nchi zetu hazina sheria zinazoendana na teknolojia.

Sasa kabla hatujazama sana kwenye majadiliano, ni muhimu tukubaliane hizi "blog za Tanzania" ni zipi?

Blog si magazeti useme unajua hili linachapwa Ilala na hili Sinza. Unaweza hata kupeleka polisi wafunge mnyororo getini.
 
"Blog za Tanzania" ni zipi?

Mtanzania anayeishi Marekani na kutumia Wordpress, lakini anayeandika habari za Tanzania kwenye blog yake, hii blog ni ya Tanzania?

Vipi anayeishi Tanzania na kutumia Wordpress?

Vipi Mmarekani anayeishi Marekani na kutumia Wordpress kuandika habari za Tanzania? Na anayeishi Tanzania? Au anayeishi Tanzania na kutumia servers za ISP wa Tanzania ku host blog?

Sheria inasemaje?

Babu taratibu hapa zinazungumziwa blog za Watanzania zinapost ujinga ujinga.

Ila kikubwa wenye matatizo ni hao wanaotembelea hizo blog uchwara maana hawalazimishwi.

Wewe unatembelea blog inaitwa udaku special bado unategemea la maana huko? Au unaingia blog ya Le Mutuz unategemea lipi la maana?

Kwa blog za Kitanzania Mjengwa blog ni mfano bora kabisa ukiacha katabia kake binafsi Maggid ka unafki.
 
Swali la msingi halijajibiwa.

Tukizungumzia "blog za Tanzania" inabidi tuelewe ni zipi.

Ni zile zinazokuwa hosted physically in Tanzania by Internet Service Providers walio Tanzania?

Au ni zile ambazo zina habari za Watanzania regardless ya zinapokuwa hosted?

Hili swali si la kifalsafa tu, lina practical implications.

Kwa mfano, tukisema "blog za Tanzania" ni zile zinazokuwa hosted na ISPs walio Tanzania, tunaweza kuweka sheria ya kuwabana ISPs watupe habari za nani kafanya nini. Watupe IP addresses na habari nyingine.

Sasa mtu yupo Virginia anatumia blog ya Google, tena ni Mmarekani mwenye asili ya Tanzania, kashachukua uraia huko hana mpango hata wa kuja likizo, na kipande cha kaburi kashanunua hukohuko,tutaanzaje anzaje kumuadibisha hata kama tukitaka?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom