Bloggers: Pengine inakera!!

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Wataalamu wanasema pengine kumwelewa tu alivyo si lazima umwone kwa sura, hata kwa sauti au maandishi yake waweza kujua tabia zake na yale anayoyapenda na kuyachukia.

Ongezoko la bloggers wa kitanzania linaonekana kukua kwa kasi sana na kwa takwwimu za haraka haraka wengi wao ni wana habari (waandishi, wapiga picha na watangazaji) katika vyombo mbalimbali vya habari ndio waliojikita katika kupasha habari kwa staili hii ya blogu. Kama inavyofafahmika, waandishi wa habari wanadhamana kubwa katika jamii na pengine wale wanaojua kwa hakika maadili ya kazi zao wamekuwa wakizingatia hata pale wanapotakiwa kuandika kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Ukijaribu kutafiti kupitia blogu nyingi sana na wenzetu wana habari unatona kuwa yale yanaoandikwa na baadhi yao ni kana kwamba wahusika huwa hawafikiri na japo wana haki ya kuandika kwa maana ya kwamba wao ndio wamiliki wa hizo blogu zao, lakini haileti maana kama hata kufikiri athari ya kile unachokiandika na lugha unayotumia inakuanika wewe binafsi na kutosaidia jamii ambayo ingejifunza kutokana na yale unayoandika.

Kwa mfano, katika moja ya blogu, mmiliki wa blogu hiyo anaandika haya hapa chini ambayo ni wazi kabisa ilikuwa ni sehemu ya kazi ambayo awali alifanya ofsini kwake na lakini badae anaamua kuianika tena kwenye kwa staili ya majungu kwenye blogu yake ili mradi tu blogu ionekane ina habari:

Kuna kipindi nilifanya interview na Hemed katika ala za roho a star Request ..
Nikamuuliza PHD Ya kuwa eti una ugomvi na Yusuph Mlela na yeye akajibu hawez kuwa na Beef na MTU ANAEJULIKANA CLUB BILICANAS,MAISHA NA KINONDONI ..
Na chicks anaotoka nao yeye hawawezi kutoka na mlela kwani yeye ni Next level na anajulikana across Africa na Mlela yeye sio levol yake ...
Hemed akaendelea kusema kuwa eti jamaa alikuwa kama ndugu yake na baada ya kuona hemed katoka kupitia Tusker Project fame na kuingia katika Movie Industry ndo hapo sasa Akaanza nuna na kuanza Kumchuniachunia ila the story inasema hawa jamaa wali share msichana,yaani msichana wa hemed alikuja kutoka na Mlela ndio chanzo cha Beef lao na Mpaka sasa Hawaelewani na ni full Masharobalo records lips hazina lipshine nilambe na ulimi lol ..
ila kusema ukweli hemed alikana hizi habari na kusema sio kweli ni kwamba yeye kamzidi mlela na kingine chicks zake hawawezi toka na mlela kwani hana hadhi hiyo doe .. nasema tena doe kazi ipo ..
ila mlela hes such a good boy trust me so sijui whats up will holla at him nisikie side yake ya Pili coz kusema ukweli .. Ni aibu wanaume kununiana na kujisifusifu ovyo
u guys shuld work together as a team bana ..nyie young blood kabisa what the heck khaaa...
eti mnaonaje ??wanaume wanaonuniana ??
Hivi karibuni kuna Binti anaitwa Radhy ali andika status kupitia facebook na kumponda hemed na kusema unajiita PHD and sifa kibao while yo stil livin witcha mama ..kama wewe ni the best si uishi mwenyewe
banaaa ..hemed una lakusema rafiki yangu?wewe kuishi na yo mama still??

http://www.diva255.com/2010/05/told-u-its-gossip-site-either-eti-mlela.html
Posted by Diva at 5:35 PM


Jamani kama twataka ufanisi, basi tukae chini, tufikiri, tujifunze toka kwa wenzetu ili tuweze kuboresha na si kukurupuka na kufanya kile ambacho pengine hakina mwelekeo wa kitaaluma wala kujenga jamii.
 
Nafikiri watanzania wengi hawajui maana ya ku-blog.Naona sehemu kubwa ya wamiliki wa blogs Tanzania wanatumia kuandika udaku au ku-copy taarifa toka kwenye vyombo vingine vya habari.Lakini ukiangalia blogs nyingi katika nchi zilizoendelea unaona contents zinakuwa juu ya mambo ambayo waanzilishi wa hizo blogs wanakuwa na utaalamu nayo.Kwa mfano unaweza kuona blogs juu ya urembo,teknohama na vitu vya namna.Zipo pia blogs za udaku hasa kwenye entertainment industry lakini hizi ziko specific kuandika juu ya hayo mambo lakini hapa Tanzania mtu anapoanzisha blogu yeye anaandika kila kinachokuja kwenye kichwa chake na anachoweza ku-copy toka kwenye blog nyingine.
 
mambo ya kuiga haya yana matatizo wafuate mfano wa blog ya michuzi.sio kwamba nampigia debe ila ankal yupo makini na kazi yake.Blog yake ipo mwake
 
Tatizo lingine shule nayo muhimu mtu anapo kosea ukimuelimisha tu kosa ooh unanionea wivu blog ni ayngu na mambo kibao sasa huyu unategemea nn atacho kuwa anatundika zaidi ya vitu anavyo ona yeye vinamfaa kwenye kichwa chake. Wanahitaji kuelimika, wakubali kuwa kuna changamoto kubwa mbele yao.
 
Tatizo lingine shule nayo muhimu mtu anapo kosea ukimuelimisha tu kosa ooh unanionea wivu blog ni ayngu na mambo kibao sasa huyu unategemea nn atacho kuwa anatundika zaidi ya vitu anavyo ona yeye vinamfaa kwenye kichwa chake. Wanahitaji kuelimika, wakubali kuwa kuna changamoto kubwa mbele yao.


Fidel, Nakubaliana kabisa na wewe.

Wakati Mwingine wataalamu wanatushauri kuwa siri ya mafanikio ni kukubali kukosolewa na kutumia mawazo ya wenzetu kujijenda na si kuendelea kusimamia yale ya kwetu tu, vinginevyo pasingekuwa na shule mapka ngazi ya u-Profesa na wala pasinge kuwa na taaluma mbalimbali kwani kila mtu anazo akili zake na angefanya vile anayoona yeye inafaa na sio jamii yake ionavyo juu yake .

Maisha siku zote ni sawa na kujatazama katika kioo, ukitaka kioo kikuambie wewe ni kwa vile kinavyokutizama, kitakuambia lakini ukikilazimisha kwa kujichekesha mbale yake, kujifutafuta nk. kamwe huwezi kupata jibu sahihi la jinsi ulivyo hata kama utajiangalia kwenye kioo mara mia kwa siku.

Sasa kama mtu anakukosoa na wewe unaendelea kusimamia misimamo yako hata kama unapotoka hiyo inadhihirisha upeo wako mdogo, udikteta wa mawazo, na kutojua nini unafanya na katika hali kama hiyo, hata kama uliwahi kuwa darasani ni wazi kuwa ulikuwa ukipitisha siku tu na darasa halijakusaidia.

Haiingii akilili mtu mzima ukashindwa kuubali ukweli, unaanzisha blogu, wewe ni mwanahabari ambaye kimsingi unapaswa kufikiri na kuandika ili uwape wanajamii habari za uhakika nk lakini unakuwa unaanza kuhamisha hamisha habari na mapicha toka katika blogu za wenzako na tovuti pasi hata kuahariri wala kuchuja chochote na kuzitundika kwenye blogu ya kwako na unasema hayo ni mawazo yake. Unaandika habari ukiwa umechanganya changanya lugha (hovyo hovyo) kiswahili, kiingereza, kichina nk...na pengine hata kufanyia mapitio ya kusahisha makosa ya uchapaji hutaki kufanya lakini bado unang'ang'ana na misimamo yako kuwa "blogu ya kwangu"..ikiwa ni ya kwako na hutaki wale wanaoitembelea wakukosoe, ya nini basi ukaiweka hewani na kusema unataka wadau wapitie na kutoa maoni??..

Tukumbuke kuwa si wakati wote yale tunayofanya yanatupatia umaarufu, kitu kama blogu na taarifa nyinginezo ambazo tunaziweka katika tovuti zinasomwa na mamilioni ya watu ulimwenguni na zitaendelea kuwepo hewani pengine hata baada ya kufa kwetu. Sasa ukiwa unaamua kuweka lolote tu unalofikiria hewani pasipo kujua athari zake inaweza kukugharimu na ukaonekana mbumbumbu mbele ya jamiii pasipo kujitambua!.

Tuchukue muda wa kujifunza na kukubali pia ukweli!!
 
Tatizo lingine shule nayo muhimu mtu anapo kosea ukimuelimisha tu kosa ooh unanionea wivu blog ni ayngu na mambo kibao sasa huyu unategemea nn atacho kuwa anatundika zaidi ya vitu anavyo ona yeye vinamfaa kwenye kichwa chake. Wanahitaji kuelimika, wakubali kuwa kuna changamoto kubwa mbele yao.


Nakushauri anzisha yako kuwaelimisha bloggers wa kibongo
 
Aisee, Shy umerudi? Karibu tena jamvini, sisi bado tunaendeleza mijadala. Umefanya vizuri kurudi lakini si vizuri ulivyondoka huku ukiapa kutorudi!

Hivi kumbe aliapa kuwa hatorudi tena JF? IT spesholist ana matatizo sana!
 
Kwangu mimi cha kuwashauri watu wengi wajaribu kwanza kuangalia kitu ambacho hamna nao wafanye hicho au waangalie ambavyo viko lakini havifanywi kwa ufanisi mfano mimi nilianzisha naombakazi.com baada ya kuona blogu Fulani kama hii iliyokuwa inaendeshwa toka Kenya nimeiboresha hii kuwa zaidi ya ile ya Kenya sasa kuna nafasi za kazi za dunia nzima haswa bara la afrika na ulaya sasa unaona nilivyoweza kumpiku huyu mwingine hata ukiangalia hapo kwenye follow utaona kila siku 3 watu 2 au 3 wanaongezeka kwenye follow na wanaofungua naomba kazi kwa siku wanazidi kuongezeka .

Lingine ni kuangalia pia hizo hizo za wenzetu lakini kuboresha zaidi kwa ajili ya watu wa kwetu na mazingira yetu hiyo itakuwa vizuri sana mfano utamaduni unaweza kuangalia blogu zingine kwenye utamaduni zinaandika nini nao huko nchi za watu unaweza nawe kuandika hivyo lakini kwa kutumia mifano na mambo mengine ya kwetu badala ya kuhangaika kuandika habari moja na maoni yanayofanana kila siku .

Halafu cha mwisho ni kuwe msomaji mzuri na kuchangia maoni au makala kwa wenzako usipofanya hivyo utakosa hata watu wa kusoma blogu zako au kuzifuatilia na utakuwa sio mbunifu wa vitu mbalimbali haswa vinavyohusu uandishi
 
Nakushauri anzisha yako kuwaelimisha bloggers wa kibongo

Hahahaha da mkuu kila mtu akianzisha ya kwake si itakuwa kero na sisi wengine sio maarufu nani atakae tembelea kwenye blog yako unaweza jikuta ni wewe na jamaa mmoja au wawili ndo mnatembelea na kuchangia maoni, kwa vile mm sina jina kama hao wengine hata nikianzisha kuwaelimisha itakuwa kazi bure cha muhimu wakubali tu kukoselewa pindi wanapo kosea hapo ndipo wanaweza ng'amua mawazo ya mtu na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
 
bloggers wanaandika kile wasomaji wao wanachotaka..............watanzania wengi tunapenda umbea na mabeef....ndo ukakuta blog zote zmejikita huko.

hawa mablogger hawatakoma mpaka atokee mtu awa sue .........
 
Blogs za maana ni chache sana, nyingi ni upuuzi mtupu na hazifai hata kutembelewa, watu wanadhani ni kazi rahisi kuanzisha Blog na kuifanya iheshimike kwenye jamii, wengi wanakurupuka tu kama hawa waliotolewa mfano.

Uanahabari ni fani ya watu jamani tena wanaendea shule, ni bora kuishia kusoma za wengine tu kuliko kuanzisha Blog na kufanya madudu.
 
Ndugu zangu tusijaribu kupotosha mada kwenye blogu sio lazima kuandika kile kitu wanachopenda ni kuandika kile ambacho mtu mwenyewe anapenda watu wajue au waweze kuchangia kwahiyo sio lazima watu wakipende

Kinachotakiwa tu ni kuwa na target Fulani na kuwe na umoja Fulani
 
I somehow agree to some points in here ila tatizo kubwa lakwetu sis wabongo ni chuki zisizo na msingi mi nadhani mtu kumuelimisha mtu si kitu kibaya ila utakuta kuna watu waingia kwenye mablog ya watu kutukana tu watu all the time je hii ni haki???

Hata kama blog inauhuru sidahni kama ni jambo zuri mtu kuwa anatukanwa au chochote anacho weka ni matusi tu. Tubadilike na pia tuelimishane kama wadau hapa mlivyo sema blog si mambo ya kucopy and paste.
 
Back
Top Bottom