Bloggers Michuzi, Milard Ayo na wenzenu wenye mawazo haya, rudini shule

KISHURO

Member
Feb 23, 2015
80
42
Kwa kawaida bloggers wengi duniani ikiwemo wamiliki wa JF utafuta mfumo mzuri wa ku copyright kazi zao hasa picha zao za kipekee. Sasa bloggers wa Tanzania wamekuja na mfumo mmoja wa kijinga sana. Nao ni kubandika LOGO kubwa katikati ya picha zao. Wao kwa uelewa wanadhani wanalinda kazi zao eti atakayecopy akaweka kwao itaonekana amekocopy hivyo atakuwa amewatangaza au wanaweza kumshtaki kwa kutumia kazi zao bila kutoa credit. Issue ya kijinga sana.

Hasara kubwa ya kuweka ma logo kama hayo ni kuwa hakuna njia bora na ya kudumu ya kutunza file/picha husika kama online. Kwa hiyo wanapoweka picha hizo online katika blog zao ni kwa faida ya wao wenyewe na vizazi vijavyo maana, katika PC au laptop ndani ya miaka minne hawawezi kuwa na picha husika.

Nawapongeza bloggers wanaweka logo zao kwa chini kama wafanyavyo AFP/REUTER nk au za kufifia kama JF.

Tazama hawa ndugu zetu;

MMGL1279.jpg
IMGL1218.jpg
MMGL0837.jpg
MMGL1056.jpg
 
Wanaharibu mpaka uhalisia wa picha, kwanini wasiweke hata transparent logos....! Wao wanataka mpaka wachafue picha......mfano hiyo picha ya jengo jipya la magamba mtu hasiyefahamu si anaweza kujua limewekewa bango la millardayo kumbe ni copyright sign
 
Ulimbukeni tu hamna lolote. Kwanza viblog vyenyewe ni free templates za WordPress, ulimbukeni wa hali ya juu kwa kujifanya wanajua.
 
Reuters iko poa sana na ya JF, ila hizo zingine wajirekebishe.
 
Back
Top Bottom