BLINDNESS IN TECH : Wadau na Wawekezaji kwenye technology wanakimbilia kuboresha hardware processing power bila kujali "Software efficiency"

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,052
Hello bosses.

Kwenye technology yoyote ile kwa sasa kuna watu muhimu sana ambao wengi hawawafahamu bali wanaishia kuona maajabu yao tu, watu hao sio wengine bali ni COMPUTER PROGRAMMERS au SOFTWARE DEVELOPERS. Iwe unaangalia TV, una-surf mtandaoni, unacheza game au unafanya kitu chochote kinachohusisha technology basi hawa watu lazima wamehusika kukuletea hicho unachoona na kufurahia kwa namna moja ama nyingine. Hivyo tunakuja kuona field ya SOFTWARE DEVELOPMENT au COMPUTER PROGRAMMING ni muhimu sana kwa maendeleo ya technology hapa duniani.

Lakini cha kushangaza ni kwamba hivi karibuni hii field (Software development) imeingiliwa na wimbi la concepts nyingi sana ambayo ni useless na hii imesababishwa na wawekezaji wengi na wadau wa technology kufocus tu kwenye kuzalisha hardware bora na zenye processing speed & power kubwa bila kutilia maanani kina nani (Computer Programmers) wataweza kuzicommand hizo hardware efficiently ili zifanye kazi kwa ufanisi mkubwa.

Okay nitoe mfano, unakuta mtu ana PC ina uwezo mkubwa tu wa kufanya parallelism au multithreading (Kurun process nyingi kwa wakati mmoja) lakini software zinazotumika humo hazina hata chembe ya parallelism, hivyo kupelekea PC ku-crash au kushindwa kurun software husika. Kama software zikiandikwa kwa ku-utilize concept ya paralleism tunaweza kuona mabadiliko makubwa sana kwenye matumizi ya hizi gadgets na softwares zake. Kila siku utasikia mara core i5, core i7 etc..... (with many cores) lakini bado unarun program inakua slow, hio ni kama vile tuko kwenye barabara inayoruhusu line 3 za magari kwenda mbele na 3 nyingine kwenda opposite lakini sote tunataka tutumie line moja hivyo kutengeneza jam ni lazima, hio ndio sababu softwares nyingi zinakua nzito kurun kwenye PC coz zinalazimisha kutumia processing thread moja wakati processor inaruhusu multi-threading.

Kitu kingine hizi taasisi zinazofundisha watu kufanya programming baadhi bado ziko nyuma sana ukilinganisha na mahitaji, na nyingine ziko mbele sana lakini kwenye direction ambayo sio sahihi(they are running very fast but out of the tracks)

Sitoongelea sana kuhusu hizi ambazo zipo nyuma coz ni kitu kinachoonekana, lakini nitaongelea hizi zinazokimbia sana(but out of the tracks). Kwa wenye idea na coding nadhan wataelewa hapa, kuna hii language inaitwa JAVASCRIPT(JS). JS ni rahisi sana kutumia na kuandika hii imefanya taasisi nyingi na watu binafsi kuinvest muda mwingi na resources kutengeneza javascript frameworks kwa almost kila kitu, huu ni uduwanzi kwa sababu tunazidisha u-softness na kufanya watu kuwa na brains ambazo ni tegemezi sana. Ukiangalia frameworks zinatengenezwa kwenye kitu ambacho bado sio efficient(Ni kama kuongeza ghorofa juu ya paa la nyumba ambayo haina msingi imara). Watu wanatumia umbrella ya "fast-prototyping" na "making everyone a programmer" kufanya vitu ambavyo vinaua kabisa hii field. Just imagine mtu anafight hadi javascript iweze kuandika USB drivers, i-program microcontrollers etc.... Kwa wataalam wanaweza jibu hapa "Hutoweza kumlinganisha mtu anaetumia JS frameworks kucode microcontroller na yule aliekua anatumia ASSEMBLY au C/C++ kiuwezo wa kufikiri na umakini katika kazi.

Sisemi kwamba frameworks zisitumike lakini shida inakuja pale unapokuta programmers wanadhani wanaelewa zaidi frameworks(Kiukweli hawazielewi) wakati hawaielewi kiundani lugha mama iliotumika kutengeneza hizo frameworks. Hii imejionesha wazi kwenye JAVASCRIPT coz wengi wanajikuta wanaelewa kutumia JS frameworks na libraries lkn hawaielewi kiundani Javascript kama Javascript. Kama baadhi ya programmers wanasema "JAVASCRIPT IS THE MOST MISUNDERSTOOD LANGUAGE EVER"

Ukiangalia mfano mwingine mission ya kwanza ya NASA ilitumia computer yenye 256 MB of RAM lakini kwa sasa ni vigumu sana kupata programmer ambae atatengeneza software yenye uwezo mkubwa na i-run kwenye PC yenye hio memory bila kukcrash.

SO, TUKIWA NA PROGRAMMERS AMBAO WANAWEZA KU-UTILIZE VIZURI COMPUTING RESOURCES ZILIZOPO KWA SASA KWA KUANDIKA EFFICIENT ALGOS NA KUTUMIA PROCESSING OPPORTUNITIES ZILIZOPO SIKUHIZI HASA HASA MULTI-THREADING ITASAIDIA SANA KUBORESHA TECHNOLOGY ZETU TULIZONAZO ILI IWE RAHISI KWA END USERS KUZITUMIA. KUKIWA NA MAKAMPUNI NA VYUO VINAVYOLENGA KUTENGENEZA PRO-PROGRAMMERS WENGI AMBAO WANAELEWA NINI WANA-CODE ITASAIDIA SANA KUTATUA HILI.

Peace......
kali linux
 
Hello bosses.

Kwenye technology yoyote ile kwa sasa kuna watu muhimu sana ambao wengi hawawafahamu bali wanaishia kuona maajabu yao tu, watu hao sio wengine bali ni COMPUTER PROGRAMMERS au SOFTWARE DEVELOPERS. Iwe unaangalia TV, una-surf mtandaoni, unacheza game au unafanya kitu chochote kinachohusisha technology basi hawa watu lazima wamehusika kukuletea hicho unachoona na kufurahia kwa namna moja ama nyingine. Hivyo tunakuja kuona field ya SOFTWARE DEVELOPMENT au COMPUTER PROGRAMMING ni muhimu sana kwa maendeleo ya technology hapa duniani.
True mkuu, japo saivi kwenye fani ya uhandisi wa program za computer tumevamiwa
Lakini cha kushangaza ni kwamba hivi karibuni hii field (Software development) imeingiliwa na wimbi la concepts nyingi sana ambayo ni useless na hii imesababishwa na wawekezaji wengi na wadau wa technology kufocus tu kwenye kuzalisha hardware bora na zenye processing speed & power kubwa bila kutilia maanani kina nani (Computer Programmers) wataweza kuzicommand hizo hardware efficiently ili zifanye kazi kwa ufanisi mkubwa.
mara nyngi mkuu hardware kama processor ikiwa inafanyiwa maboresho ni kilingana na demand na requrement za software, niliona telsa wamaupgrade processor yao kulingana na impovement ya softaware self-driving. au unakuta device ipo specified labda hii ni kwa matumizi flan labda hii ni kwa ajili ya games au device hii ni kwa ajili ya VR .
Okay nitoe mfano, unakuta mtu ana PC ina uwezo mkubwa tu wa kufanyaparallelism au multithreading (Kurun process nyingi kwa wakati mmoja) lakini software zinazotumika humo hazina hata chembe ya parallelism, hivyo kupelekea PC ku-crash au kushindwa kurun software husika. Kama software zikiandikwa kwa ku-utilize concept ya paralleism tunaweza kuona mabadiliko makubwa sana kwenye matumizi ya hizi gadgets na softwares zake. Kila siku utasikia mara core i5, core i7 etc..... (with many cores) lakini bado unarun program inakua slow, hio ni kama vile tuko kwenye barabara inayoruhusu line 3 za magari kwenda mbele na 3 nyingine kwenda opposite lakini sote tunataka tutumie line moja hivyo kutengeneza jam ni lazima, hio ndio sababu softwares nyingi zinakua nzito kurun kwenye PC coz zinalazimisha kutumia processing thread moja wakati processor inaruhusu multi-threading.
dha, mkuu wewe ni sumbufu sana inaonekana una tumia mda wingi kwenye computer, concept ya parallelism & multithreading/concurrent ni moja vya vitu mtu ukiwa unategeneza website au app huwezi vijua hapa unakuja umuhimu wa C, C++ na ndugu yao Java. sometime developer wenyewe tunashidwa ku take advantage ya improvement ya hardware
Kitu kingine hizi taasisi zinazofundisha watu kufanya programming baadhi bado ziko nyuma sana ukilinganisha na mahitaji, na nyingine ziko mbele sana lakini kwenye direction ambayo sio sahihi(they are running very fast but out of the tracks)
mpaka karne hii baadhi ya institution hazifundishi python darasan
Sitoongelea sana kuhusu hizi ambazo zipo nyuma coz ni kitu kinachoonekana, lakini nitaongelea hizi zinazokimbia sana(but out of the tracks). Kwa wenye idea na coding nadhan wataelewa hapa, kuna hii language inaitwa JAVASCRIPT(JS). JS ni rahisi sana kutumia na kuandika hii imefanya taasisi nyingi na watu binafsi kuinvest muda mwingi na resources kutengeneza javascript frameworks kwa almost kila kitu, huu ni uduwanzi kwa sababu tunazidisha u-softness na kufanya watu kuwa na brains ambazo ni tegemezi sana. Ukiangalia frameworks zinatengenezwa kwenye kitu ambacho bado sio efficient(Ni kama kuongeza ghorofa juu ya paa la nyumba ambayo haina msingi imara). Watu wanatumia umbrella ya "fast-prototyping" na "making everyone a programmer" kufanya vitu ambavyo vinaua kabisa hii field. Just imagine mtu anafight hadi javascript iweze kuandika USB drivers, i-program microcontrollers etc.... Kwa wataalam wanaweza jibu hapa "Hutoweza kumlinganisha mtu anaetumia JS frameworks kucode microcontroller na yule aliekua anatumia ASSEMBLY au C/C++ kiuwezo wa kufikiri na umakini katika kazi.
JS naitumia lkn basi tu sina option
Sisemi kwamba frameworks zisitumike lakini shida inakuja pale unapokuta programmers wanadhani wanaelewa zaidi frameworks(Kiukweli hawazielewi) wakati hawaielewi kiundani lugha mama iliotumika kutengeneza hizo frameworks. Hii imejionesha wazi kwenye JAVASCRIPT coz wengi wanajikuta wanaelewa kutumia JS frameworks na libraries lkn hawaielewi kiundani Javascript kama Javascript. Kama baadhi ya programmers wanasema "JAVASCRIPT IS THE MOST MISUNDERSTOOD LANGUAGE EVER"

Ukiangalia mfano mwingine mission ya kwanza ya NASA ilitumia computer yenye 256 MB of RAM lakini kwa sasa ni vigumu sana kupata programmer ambae atatengeneza software yenye uwezo mkubwa na i-run kwenye PC yenye hio memory bila kukcrash.

SO, TUKIWA NA PROGRAMMERS AMBAO WANAWEZA KU-UTILIZE VIZURI COMPUTING RESOURCES ZILIZOPO KWA SASA KWA KUANDIKA EFFICIENT ALGOS NA KUTUMIA PROCESSING OPPORTUNITIES ZILIZOPO SIKUHIZI HASA HASA MULTI-THREADING ITASAIDIA SANA KUBORESHA TECHNOLOGY ZETU TULIZONAZO ILI IWE RAHISI KWA END USERS KUZITUMIA. KUKIWA NA MAKAMPUNI NA VYUO VINAVYOLENGA KUTENGENEZA PRO-PROGRAMMERS WENGI AMBAO WANAELEWA NINI WANA-CODE ITASAIDIA SANA KUTATUA HILI.

Peace......
kali linux
 
Niliacha programming tokea mwaka 2015 au 2014 sina kumbukumhmbu vizuri ila ni majaira hayo. Sababu kubwa iliyonipelekea kuacha.. nilikuwa nyuma ya technology ( ulimwengu unakwenda haraka sana, tofauti na tanzania inavyo kwenda ).

Framework ni nzuri sana kama mtu ume master.. ila shida wengi hizi framework wanazitazama kwa macho tofauti na matokea wengi wanatumia hizi na endproduct zinakuwa mbaya mbaya.. huku bado wamerahishiwa..

Hapa kwetu tanzania hizo Assembly language ni maeneo machache sana zinatumika na kama unafaka kuzitumia basi ujiajiri.. huko mbele hizi fresh.. wanaendana na speed ya tech.. nilijifunza assembly kwasababu tu nilikuwa nafanya reverse engineering na some hacking kwenye low level.. ila nikaona ungese ungese tu nikaacha.. sasa hivi nalima nyanya na matikiti ma programmers kibao huja kunikopa hela 😃😃😃😃
 
dha, mkuu wewe ni sumbufu sana inaonekana una tumia mda wingi kwenye computer, concept ya parallelism & multithreading/concurrent ni moja vya vitu mtu ukiwa unategeneza website au app huwezi vijua hapa unakuja umuhimu wa C, C++ na ndugu yao Java. sometime developer wenyewe tunashidwa ku take advantage ya improvement ya hardware
Umeona sasa madhara ya frameworks hayo, exactly what I said

Parallelism kwenye web unaweza ukaitumia, kwenye Javascript ipo lkn ni core Javascript so kama unatumia jquery, angular na ndugu zake hutowahi kuigusa. Kuna kitu kinaitwa promises kwenye Javascript (Async and Wait) fatilia hizo zinaweza kukupa mwanga wa concurrency kwenye web development.

Pia umeongelea kuhusu tesla, yeah tesla wanajitahidi na ndio maana kila kukicha wana mafanikio. Wameona hilo gap kwenye industry. Ndo maana ukiangalia ECU (Engine control Unit) au Computer zinazotumika kwenye magari za Tesla zina nembo kabisa ya tesla hadi kwenye microcontroller coz wanatengeneza kila kitu kwa kuwa wameona kuchukua vya wengine ni craps tupu. Cheki mfano Toyota wanachukua ECU kutoka kwa Denso lkn headache yake mafundi magari umeme wanaielewa.

Kuna report ya engineers wa Toyota ilitolewa na Engineer wao mmoja hivi baada ya kusambalatisha gari ya Tesla kuona zile ECU zake zilivyo na technical structure nzima lkn huyo Engineer aliconclude kwa kusema "WE CANNOT DO IT, TESLA IS 6 YEARS AHEAD OF US"
Soma hapa hio article kutoka Nikkei

So Tesla ni kati ya makampuni machache yalioona hilo, aidha wanatengeneza efficient software zitakazoendana na limitation za hardware au wanatengeneza hardware zitakazo beba vzr software zao(Technical trade-offs) na ndio maana wanafanikiwa kila kukicha na stock yao inaenda juu kila kukicha.
 
Nje ya mada.
Mkuu nataka nijifunze kali linux kwa ajili ya black hat hacking...unarecommend resources gani?
inatumia kama muda gani (approx)?
 
Nje ya mada.
Mkuu nataka nijifunze kali linux kwa ajili ya black hat hacking...unarecommend resources gani?
inatumia kama muda gani (approx)?
kali.org kuna kilakitu hapo, hadi mitihani na certificates
 
Lengo la framework ni zuri tu kuturahisishia ufanyaji wa kazi lakini tatizo ni pale programmer anaanza kujifunza framework kabla ya language yenyewe anaishia kukariri tu bila kujua core ya lugha husika,
Hata hivyo programming katika nchi yetu bado tuko nyuma sana watu hawapati deals wanaishia kulima matikitiki tu baada ya kuwekeza miaka zaidi ya mitano kujifunza programming
 
Back
Top Bottom