Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa bado wapo Wizarani

Wakati tukiendelea kupokea na kung'amua vitendo mbalimbali vya ufisadi vilivyofanywa na Mapacha wawili wa Wizara ya Afya (Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa), habari nilizozinyaka leo kutoka kwa watumishi watatu na baadae nikadhibitishiwa na Mkuu wa Idara mmoja ambae yupo Wizara ya Afya, zinasema Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali waliosimamishwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bado wapo kazini na hata leo wamekuwepo Ofisini.

Habari zinasema kuwa wamekuwa katika heka heka za kuweka sawa nyaraka zao vizuri hasa zile zinahusu Manunuzi. Concern yetu hapa ni kwamba imekuwaje Pinda ameweza kuwadanganya Madaktari kuwa mahasimu wao wakuu Bi Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa amewasimamisha kazi tangu mchana wa Alhamisi ya tarehe 09/02/2010 wakati bado wameendelea kwenda ofisini hadi leo?

Hofu inayoibuka hapa ni kwamba kama wataendelea kwenda ofisini wakati tayari wamesimamishwa kazi na Waziri Mkuu katangaza kuwa wanachunguzwa na vyombo vya dola, Je hawawezi kutumia mwanya huu kupika au/na kupoteza nyaraka za serikali ambazo zingesaidia katika ushahidi? Na je Waziri Mkuu Mizengo Pinda, anamdanganya nani kwamba Blandana Nyoni na Deo Mtasiwa wamesimamshwa wakati bado wanaenda ofisini tena kwa kutumia V8 za serikali?
[/QUOTE

Sasa ww ulitaka waende wapi? kwani unawafuatafuata walikufanya nn Mkuu? maana huu ni uzi wa pili sasa umefungua. Kwani ata wakienda Wizarani ww kina kuuma nn? kama nilivyokwambia katika ule uzi wako wa tuhuma za majungu kuwa wameshakugundua na dawa yako inachemka kwa ajili ya majungu ambayo umeyaanzisha, wametumwa waendelee na kazi ili kuja kuwatafuta wale wote waliosambaza majungu kutokea Wizarani (Inner circle), safari hii hamtaamishwa kupelekwa Milembe, nadhani kinachofuata unakijua. Sijui ulipoanza kazi pale Wizarani walikufanyia VETTING na kama ni ndio, unajua kitakachokupata. "Majungu si Mtaji"
Mbona unamtishia mwenzako, wewe ni muhusika nini, huyu bwana anatupa information juu utendaji kazi wa serikali yetu wewe unamzima kuna nini??? Na wewe unayezima wenzako ni nani???Kaa ukijua pamoja na harakati zako za kuzima wenzako, ukombozi uko njiani karibu saana watu watakombolewa tuu!!!!

Mi niliwashangaa sana mlipo shabikia nikawauliza Pinda ametoa wapi mamlaka ya kuwasimamisha kazi?
 
Hivi kwa nini Pinda anapenda kutupindua pindua kama mazuzu?kama hii ni kweli basi Pinda hafai na hatutaki kumsikiliza tena,aaaaagh!!!
 
Yaani anayemwamini Punda mimi namshangaa! Hilo baba hata halioni aibu kabisaaa! Juzi hapa limelia halina uwezo wa kumfukuza Jairo, leo eti linapata uwezo wa kuwafukuza hao wawili?! Nya...f!

mkuu asante kwa kuliona hilo.................
 
The fact that ameshatangazwa kwenye vyombo vya habari kwamba ameachishwa kazi hakuna jinsi ya kurudisha hii kauli. Ukiangalia shutuma zilizowekwa ni kwamba huyu mama alikuwa anashughulikia kila kitu pale wizarani na hii wizara ni kubwa na ina mambo mengi. Hii ina maana kwamba isingekuwa rahisi kuondoka mara moja inabidi aeleze kila kitu ameweka wapi ili huyo anayekuja kukaimu aelewa aanzie wapi.

Punguzeni pressure, it is just a matter of time ataondoka tu
 
Wakati tukiendelea kupokea na kung'amua vitendo mbalimbali vya ufisadi vilivyofanywa na Mapacha wawili wa Wizara ya Afya (Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa), habari nilizozinyaka leo kutoka kwa watumishi watatu na baadae nikadhibitishiwa na Mkuu wa Idara mmoja ambae yupo Wizara ya Afya, zinasema Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali waliosimamishwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bado wapo kazini na hata leo wamekuwepo Ofisini.

Habari zinasema kuwa wamekuwa katika heka heka za kuweka sawa nyaraka zao vizuri hasa zile zinahusu Manunuzi. Concern yetu hapa ni kwamba imekuwaje Pinda ameweza kuwadanganya Madaktari kuwa mahasimu wao wakuu Bi Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa amewasimamisha kazi tangu mchana wa Alhamisi ya tarehe 09/02/2010 wakati bado wameendelea kwenda ofisini hadi leo?

Hofu inayoibuka hapa ni kwamba kama wataendelea kwenda ofisini wakati tayari wamesimamishwa kazi na Waziri Mkuu katangaza kuwa wanachunguzwa na vyombo vya dola, Je hawawezi kutumia mwanya huu kupika au/na kupoteza nyaraka za serikali ambazo zingesaidia katika ushahidi? Na je Waziri Mkuu Mizengo Pinda, anamdanganya nani kwamba Blandana Nyoni na Deo Mtasiwa wamesimamshwa wakati bado wanaenda ofisini tena kwa kutumia V8 za serikali?

Nafikiri unapaswa kujua kuwa Blandina na Mtasiwa ni wateule wa Rais hivyo kuna taratibu zake za kufuata katika kuachia ofisi ikiwa pamoja na kusubiri jina la mteule atakayekabidhiwa ofisi na majukumu. Wao kama wao hawawezi kumwachia wamtakae bali lazima wasubiri amri toka kwa rais kupitia waziri husika.

Kuna mengi ya kukabidhiana sio tu ofisi kama ofisi. Ukibahatika kufikia level a kuwa mteule wa rais utalijua hilo. Na hata wakitaka kuacha kazi lazima waombe kibali kwa Rais ili atengue uteuzi wake kwao.

Kuwa na subra kwani sasa hawafanyi kitu kipya chochote wao wapo kusubiri nani akabidhiwe majukumu na madaraka.
 
Nyie wadanganyika ni vilaza kweli kweli mnategemea uchunguzi gani ufanyike: mpaka leo watuhumiwa wa Richmond kamati ya bunge ilipendekeza wachunguzwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao, je uchunguzi wao umekamilika na wamechukuliwa hatua gani?
 
Pinda hivi kwa nini hujaweka askari maofisi mwao wasiruhusiwe kufanya chochote zaidi ya kubeba personal belongings zao?

Pindaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa whhyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyy unadanganya??????????????

mmmhh sababu unajua hautafuti cheo tena

Kikwete hatua za waziri etc nae kimya

:sad:
 
Back
Top Bottom