Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa bado wapo Wizarani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa bado wapo Wizarani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUMBIRI, Feb 13, 2012.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakati tukiendelea kupokea na kung'amua vitendo mbalimbali vya ufisadi vilivyofanywa na Mapacha wawili wa Wizara ya Afya (Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa), habari nilizozinyaka leo kutoka kwa watumishi watatu na baadae nikadhibitishiwa na Mkuu wa Idara mmoja ambae yupo Wizara ya Afya, zinasema Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali waliosimamishwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bado wapo kazini na hata leo wamekuwepo Ofisini.

  Habari zinasema kuwa wamekuwa katika heka heka za kuweka sawa nyaraka zao vizuri hasa zile zinahusu Manunuzi. Concern yetu hapa ni kwamba imekuwaje Pinda ameweza kuwadanganya Madaktari kuwa mahasimu wao wakuu Bi Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa amewasimamisha kazi tangu mchana wa Alhamisi ya tarehe 09/02/2010 wakati bado wameendelea kwenda ofisini hadi leo?

  Hofu inayoibuka hapa ni kwamba kama wataendelea kwenda ofisini wakati tayari wamesimamishwa kazi na Waziri Mkuu katangaza kuwa wanachunguzwa na vyombo vya dola, Je hawawezi kutumia mwanya huu kupika au/na kupoteza nyaraka za serikali ambazo zingesaidia katika ushahidi? Na je Waziri Mkuu Mizengo Pinda, anamdanganya nani kwamba Blandana Nyoni na Deo Mtasiwa wamesimamshwa wakati bado wanaenda ofisini tena kwa kutumia V8 za serikali?
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Serikali ya kisanii hii no one is serious!
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  makubwa!
  Jairo kaibukia Wizara ya afya
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,499
  Likes Received: 19,914
  Trophy Points: 280
  serikali ya vilaza hii ..unafikiri Pinda hajui.anajua sana ..chezo hili
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Pinda anapenda sana kudhalilika...Very soon atadhalilishwa tena na tabia yake ya kuwa mbwa asiye na meno.
  Naamini madaktari wanayaona na kuratibu mambo yote ya kizembe haya!
   
 6. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Jairo?
   
 7. Mtafiti1

  Mtafiti1 JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiwa mtoto, kumbuka ni mara ngapi uliwahi kumsemea baba kwa mama ukitegemea baba atamchapa mama?
  Mtasubiri sana maana lao ni moja!
   
 8. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mambo ya serikali ni endelevu, hata mtu akisimamishwa kazi ofisi lazima ifanyekazi hivyo kama wanakwenda ni kwenda kukabidhi ofisi kwa wengine watakaochukua nafasi zao!!
   
 9. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  hutaki?
  mzimu basi!
   
 10. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pinda hatarini tena. Spongy la ccm lazidi kunyonya uchafu na kuurudisha. Tutafika kweli!
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hivi watanzania mulimwamini Pinda,,huyo mbaba mbona ni mwongo sana kuliko kawaida ndivyo alivyo viongozi wa CCM hawana jema wanachotaka ni nchi iingie kwenye machafuko
   
 12. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama bado wako kazini basi hiyo ni kinyume na makubaliano na madaktari. Nashauri madaktari waendeleze mgomo wao waliositisha.
   
 13. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Serikali hii, kila jambo hufanywa kwa kigugumizi!! Ukiamua kumchunguza mtu kwa ufisadi wakati anaendelea kufika ofisini tarajia ushahidi kuchakachuliwa!!
   
 14. m

  mhondo JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Labda bado hawajapokea/hawajapewa barua za kusimamishwa. Serikali inafanya kazi kupitia nyaraka sasa kama imetangazwa kwenye Tv tu na hawajapewa barua ni halali kwao kwenda kazini.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Feb 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwani Waziri Mkuu alisema wamesimamishwa kuanzia lini?
   
 16. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  you are very wrong...ukisimamishwa kazi kupisha uchunguzi hutakiwi kuonekana ofisini kwako wala ndani ya eneo la kazi. hi inatokana na kuogopa kuficha baadhi ya nyaraka muhimu ambazo zingeweza kuharakisha uchunguzi
   
 17. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Jamani acheni utani mtanifanya kesho nichane passport ya nchii nikawe mkimbizi somalia.
   
 18. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu TUMBIRI hiyo tarehe 9/2/2010 mbona sielewielewi vile?
   
 19. T

  Tinker Member

  #19
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]
   
 20. K

  Karata JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
   
Loading...