Blandina Nyoni ana siri nzito za vigogo Mafisadi, wakwepa kodi na wezi wa mali ya umma Tanzania

Unajua huyu mama sio kwamba anajua kitu kuhusu hawa viongoz anaowasema..bali kwavile anajua TZ hakuna msafi basi ameona akilopoka huo upuuzi wake kwa vile viongozi wetu wengi sio waadilifu basi wakiona ujumbe wake watapunguza makali ya kumfatilia...lakini bado hatakuwa msafi hata km kamati amabyo ikimchunguza itaongozwa na Lowassa hawezi kuwa msafi hata kidogo:juggle:
 
Source ni gazeti la rostam?crap alikua wapi siku zote?watajulikana tu later kwani yy kajulikanaje?hao watafuata yy atangulie jela tu
 
Hakika hii nchi ingekuwa na wananchi km wa Mara,,Arusha na Mbeya hakika hii serikali ingefanya kazi vizuri sana:lol:
 
Ninachoshukuru tu huyu Blandina Nyoni na Deo Mtasiwa wote ni wakristo maana wangekuwa waislamu leo mngesikia tamko la Bakwata kwamba waislamu wanaonewa.
 
ha ha ha.....dunia uwanja wa fujo, mwaga ugali namwaga mboga na maji ya kunawa na kunywa namwaga

Taarifa kutoka chanzo cha karibu na Blandina Nyoni zinasema Kuwa aliyekuwa Katibu mkuu wa wizara ya Afya amesema anasiri nzito ya vigogo mafisidi wote wa nchi hii waliokwapua fedha hazina kupitia miradi na project feki katika kipindi chote alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, amefunguka na kusema nchi hakuna kiongozi msafi kama kuchafuana tutachufuana wote na kama jela itajaa Viongozi wa juu wa serikali wasasa na wastaafu.

Taarifa zinasema amekasirishwa na Kauli za pinda na Mpambe wake Ghasia ambaye anakashifa za kutosha pale utumishi juu ya mishahara na project mabalimbali; Amewataka watanzania wakae mkao wa kupata waporaji wakubwa wa mali ya umma
 
Hizi ni porojo tu
Jambazi limtaje jambazi lenzake ili iweje?!
Lile ni changa la macho, Blandina hatafanywa lolote na hii serikali legelege ya mafisadi
Sanasana atatafutiwa ulaji mwingine mahali patamu zaidi
JK bwana..
 
Hata kama ufisadi wa Blandina ukithibitika si kitu cha kushangaa au kukomalia. Aidha, ataje au asitaje ufisadi (wa kutisha) wa viongozi wa Serikali nayo si habari. Kumkomalia mtu kama Blandina ni kupoteza muda. Tusijidanganye, hawezi kufanya fujo zote hizo (za kifisadi) bila mazingira (ya Serikali) kumrushusu. Na tusiharakishe kufikiria kama keshaanguka. Naona hata Jairo tu tumeshamsahau kama vile tayari yuko jela! Nchi hii inaendeshwa kama mishen-taun kwelikweli na inaliwa hasa kama hawana akili nzuri vile. Anayekamatwa na asiye na godfather ndiye anayebebeshwa msalaba. Bila mapinduzi ya kweli hadithi za akina Blandina zitaendelea kutupotezea muda na nyenzo zetu za kufikiri miaka nenda miaka rudi.
 
hii habari uzushi mtupu,huko aliko presha juu
jipeni moyo Maffisadi kwani ataanza kufumua malipo ya Ujenzi wa ubalazo wa Itali ambapo sasa Jumba Bovu limemwangukia Prof Mahalu, then Malipo ya Rada na Vijisent vya Chenge then atafunguka juu ya malipo kibao ya project hewa zilizofanyika kipindi cha Mkapa na Mwanzoni mwa Utawala wa JK na siri kibao za vigogo juu ya uporaji wa nyara za serikali huko maliasili
 
Jambazi likikamatwa na polisi, basi huwa pia linakuwa polisi jamii. Yaani saidia polisi. Blandina please corporate with police kuwajata wizi wenzio.
 
Blandina kuwatia kitanzini Wakurugenzi wa Wizara na Wakuu wa miradi kwani katika shutuma anazotuhumiwa alikuwa anawaagiza kutia saini malipo na yeye kazi yake ilikuwa kwenda kuchukua 10% du mama huyu nikiboko cjawi ona
 
Funguka mama funguka, asikutishe mtu! Wamejitia kumwaga ugali mama, usichelewe kumwaga mboga. Mama Nyoni lete raha mama. Watanzania zaidi ya 98% TUNAVUMILIA kuwa watanzania badala ya kujivunia kuwa watanzania. Teremsha data madam, after all you have nothing to lose!! Ni majira kama haya tulikuwa tunayasubiri ili tupate mlango wa kutokea. Pinda amezidi kupindisha mambo, ametishia watu wazima nyau...., akaona hawatishiki! Sasa anajifanya mtu makini na mwenye busara. CCM imekula kwenu. Ukisikia mtu ni mwana-CCM mtazame na kumhurumia na ikiwezekana muokoe katika tanuru hilo la uovu. Maandiko matakatifu yanasema wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika tanuru la moto. Mama Blandina tupe raha kwa kumwaga mboga kwani hiyo list utakayoshusha inamhusu mzee madevu aka Okampo.
 
Taarifa kutoka chanzo cha karibu na Blandina Nyoni zinasema Kuwa aliyekuwa Katibu mkuu wa wizara ya Afya amesema anasiri nzito ya vigogo mafisidi wote wa nchi hii waliokwapua fedha hazina kupitia miradi na project feki katika kipindi chote alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, amefunguka na kusema nchi hakuna kiongozi msafi kama kuchafuana tutachufuana wote na kama jela itajaa Viongozi wa juu wa serikali wasasa na wastaafu.
Taarifa zinasema amekasirishwa na Kauli za pinda na Mpambe wake Ghasia ambaye anakashifa za kutosha pale utumishi juu ya mishahara na project mabalimbali; Amewataka watanzania wakae mkao wa kupata waporaji wakubwa wa mali ya umma
/QUOTE]

Die water aka mfa maji. ataje tu ila kwake ndo tayari imeshakula. lakini pia wewe jambazi tutajia majambazi wenzako (eti nilikuwa hazina wakati hela zinaibiwa, wewe mama ni taahira nini? kwa nini hukusema?)
 
Taarifa kutoka chanzo cha karibu na Blandina Nyoni zinasema Kuwa aliyekuwa Katibu mkuu wa wizara ya Afya amesema anasiri nzito ya vigogo mafisidi wote wa nchi hii waliokwapua fedha hazina kupitia miradi na project feki katika kipindi chote alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, amefunguka na kusema nchi hakuna kiongozi msafi kama kuchafuana tutachufuana wote na kama jela itajaa Viongozi wa juu wa serikali wasasa na wastaafu.

Taarifa zinasema amekasirishwa na Kauli za pinda na Mpambe wake Ghasia ambaye anakashifa za kutosha pale utumishi juu ya mishahara na project mabalimbali; Amewataka watanzania wakae mkao wa kupata waporaji wakubwa wa mali ya umma

kiongozi mpumbavu hatofautiani na maneno yake.
 
Ninachoshukuru tu huyu Blandina Nyoni na Deo Mtasiwa wote ni wakristo maana wangekuwa waislamu leo mngesikia tamko la Bakwata kwamba waislamu wanaonewa.

Mkuu tujaribu kuepuka mambo ya udini kwenye maslahi ya Taifa kwa kauli yako hii huwatendei haki ndugu zetu waislamu.
 
Taarifa kutoka chanzo cha karibu na Blandina Nyoni zinasema Kuwa aliyekuwa Katibu mkuu wa wizara ya Afya amesema anasiri nzito ya vigogo mafisidi wote wa nchi hii waliokwapua fedha hazina kupitia miradi na project feki katika kipindi chote alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, amefunguka na kusema nchi hakuna kiongozi msafi kama kuchafuana tutachufuana wote na kama jela itajaa Viongozi wa juu wa serikali wasasa na wastaafu.

Taarifa zinasema amekasirishwa na Kauli za pinda na Mpambe wake Ghasia ambaye anakashifa za kutosha pale utumishi juu ya mishahara na project mabalimbali; Amewataka watanzania wakae mkao wa kupata waporaji wakubwa wa mali ya umma

blimey!

where was she?
alikuwa wapi?
alikwina?
alikugu?
 
hawezi,hatadhutu na hata kuja dhubutu kusema lolote lile juu ya wezi hususani anao wafahamu hata kama alikula nao,haitokuja tokea ktk Tanzania yetu hii ya leo

Yeye akubari tu yaishe kuwa imekula kwake
 
Back
Top Bottom