blackberry 8100

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
1,407
159
Wana JF naombeni msaada wenu wakiufundi,nina simu yangu aina ya blackberry Pearl 8100 , nimeinunua marekani na nimeitumia huko karibu miaka 2 nilipo kuja hapa tanzania mwaka jana mwenzi 11 niliitumia vizuri tu

bila matatizo baada ya mwenzi mmoja ilizima ghafla na nilipo jaribu kuwasha ikagoma kuwaka mpaka leo hii nimekuwa siwezi kuitumia,nimejaribu kupeleka kwa mafundi wa hapa wameniambia kuwa hawana software za kufanyia flashing,
nika mpata fundi mmoja akaniambia kuwa anaweza nilipo mpelekea akajaribu kuflash akashindwa akadai kuwa ina virus,basi ndugu zangu naombeni mnisaidie kama mnaweza kunielekeza kwa fundi ambae anaweza kutatua

tatizo ili ambalo linanisumbua kichwa changu.au ushauri wa namna gani naweza kulitatua mwenyewe..

blackberry-8100_00.jpg
 
Wana JF naombeni msaada wenu wakiufundi,nina simu yangu aina ya blackberry 8100, nimeinunua marekani na nimeitumia huko karibu miaka 2 nilipo rudi hapa tanzania mwaka jana mwenzi 11 niliitumia vizuri tu

bila matatizo baada ya mwenzi mmoja ilizima ghafla na nilipo jaribu kuwasha ikagoma kuwaka mpaka leo hii nimekuwa siwezi kuitumia,nimejaribu kupeleka kwa mafundi wa hapa wameniambia kuwa hawana software za kufanyia flashing
nika mpata fundi mmoja akaniambia kuwa anaweza nilipo mpelekea akajaribu kuflash akashindwa akadai kuwa ina virus,basi ndugu zangu naombeni mnisaidie kama mnaweza kunielekeza kwa fundi ambae anaweza kutatua

tatizo ili ambalo linanisumbua kichwa changu.au ushauri wa namna gani naweza kulitatua mwenyewe..

blackberry-8100_00.jpg

blackberry-8100_00.jpg
 
ina mwaka mmoja, hapo juu nimekosea kusema nimeitumia huko miaka miwili, niliitumia huko miezi miwili tu,ni brand new.
 
ina mwaka mmoja, hapo juu nimekosea kusema nimeitumia huko miaka miwili, niliitumia huko miezi miwili tu,ni brand new.

Pole sana, nilidhani ina umri zaidi au used ningesema half life yake imefika. Utapata msaada hapa kuna wataalam zaidi.
 
tumsam, hao mafundi uliowapelekea na kujaribu kuifanyia flashing, je walifanya hivyo simu ikiwa imewaka, yaani 'on'.... au hilo linawezekana wakati simu imezimika?
 
Bwana Mkubwa

Kama Imezimika Ni Matatizo Ya Kiufundi Haswa Mambo Ya Umeme Wasiliana Na Huyu 0784406060 Ni Mjuzi Wa Simu Ataweza Kukusaidia Uzuri

Thanks
 
SteveD
ni kwamba walikuwa wanafanya flashing, ikiwa imezima wakadai kuwa kila ikikaribia kumaliza flashing inagoma kumalizia,ila mafundi wengi waliniambia kuwa ni virus,
 
shy:

ahsante kwa ushauri wako nitaufanyia kazi,pia swala la kuwaka kuna siku inawaka yenyewe then inajizima... naomba wenye ushauri zaidi au maoni wanisaidie tafadhali.
 
Mkuu tumsam,

Pole kwa tatizo lililokupata.

Inawezekana hio simu imekufa kwa virusi kama anavyojaribu kusema huyo fundi.

Unajua kuna fature moja ya On/OFF ambayo inakuwezesha kui-set hio simu ijizime kwa muda utakao wewe. Hapo katika Home Screen kuna sehemu ya Options applications ambapo ndio unaset kwamba simu ijizime.

Sasa inawezekana (kwa maoni yangu) wewe au mtu mwingine alieishika hio simu kaifanyia option hio bila kujua. Na kama ni hivyo hatujui simu itawaka vipi, hayo ni mawazo yangu tu.

Sasa tukirudi kwa virusi ni kwamba vinaweza kuwa vimeingia kwenye simu yako kupitia Bluetooth kama ilikuwa "on" na mtu akaweza kufanya "pairing" na akakutumia hiyo midubwana.

Au pia imepata virusi ikiwa Wireless feature ilikuwa "on" na ikajaribu kugain coverage na kukutana na device ingine ambapo waliwasilina na mtu akakutumia virusi.

Kwa hio in future jaribu kuzima hizi features mbili kama huzitumii.

Halafu mkuu hio ni moja ya "smart phones" nzuri sana sijui ni kwanini hujawa mwangalifu nayo.

Ntakupa ushauri baada ya majibu ya huyo fundi ulielekezwa.
 
richard

asante sana kwa maoni yako mazuri ambayo yameni fungua ni kweli nilikuwa na tumia mara nyingi headphone ambayo inatumia Bluetooth hivyo

mda mwingi ilikuwa Bluetooth ipo on, pia kwa upande wa Wireless ilikuwa on kwani nilikuwa na tumia kupokelea e-mail
 
Bwana Mkubwa

Kama Imezimika Ni Matatizo Ya Kiufundi Haswa Mambo Ya Umeme Wasiliana Na Huyu 0784406060 Ni Mjuzi Wa Simu Ataweza Kukusaidia Uzuri

Thanks
hiyo no ya simu uliyo nipa mkuu mbona mwenyewe hapokei simu?
 
hiyo no ya simu uliyo nipa mkuu mbona mwenyewe hapokei simu?

..tum,

..kama ni suala la mafundi hapa bongo inabidi uwe makini sana! kwa ufupi hamna mafundi wazuri wa blackberry.

..sasa, kama unaweza kuongea na watu wa celtel [ingekuwa vizuri kama ungenunua simcard yao,kama hauna,ili wakupe ushirikiano mzuri zaidi] wakueleze zao huwa wanazi-service wapi. nadhani watakuwa na fundi.

..pili, pale shoppers plaza [mikocheni] ghorofa ya kwanza nadhani,kuna mhindi mmoja kijana ana ka-shop kake kanaitwa "ib electronics" ni fundi mzuri ila bei mbaya kidogo. kamwone [yeye sio vijana wake] umweleze tatizo hilo.

..tatu, kama una jamaa wanaoenda uk au usa mara kwa mara,wape hiyo simu waende nayo ikatengenezwe.

..pole kwa usumbufu.
 
Naungana na wewe kabisa hasa point hio ya tatu na ndo nilichotaka nimshauri kama last resort.

Ona sasa, anapewa namba na haipokelewi!

Sidhani kama wanaweza kuitengeneza hapo alipo.
 
Nyongeza kwa alichoandika DsL, ni kwamba: hiyo simu kama ilinunuliwa huko ulaya na ilinunuliwa kwa njia halali kama inavyoonekana, basi tumsam anaweza kujaribu hata kuirudisha kwa manufacturers.

Kwa vile amesema alinunua around october mwaka jana, then, ile internatioanal manufacturer warranty ya mwaka mmoja (pahala pengi) naamini bado inayo, hivyo anaweza kutumia hiyo opportunity kuliko kuhangaika na mafundi ambao hauna uhakika nao.

BTW, thanks kwa jibu hapo mwanzoni, naona kuna ka-ahueni, maana simu inaweza kuwaka na siyo imezima kabisa kabisa....

Pole ndugu, natumaini utatatua tatizo.

SteveD.
 
ndugu zangu.

nashukuru kwa ushauri wenu na maoni yenu,nitajitahidi kuangalia ni jambo gani nitafanya...naomba mwenye maoni zaidi au ushauri anaweza kutoa.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom