Black Jesus (Based on true story)

Nicodemas Tambo Mwikozi

JF-Expert Member
Aug 13, 2016
663
1,047
Sumbawanga ndiyo nyumbani kwetu, na kitongoji maarufu kiitwacho Mazwi ndiko hasa nilikozaliwa, kukulia na kujanjarukia!

Umbali wa takribani mita mia moja tu kutoka nyumbani kwetu, mahali nilipokulia na kuishi na bibi na babu yangu, ndipo unapopatikana uwanja maarufu mkoani Rukwa uliopewa jina la baba wa taifa la Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, yaani Nelson Mandela Stadium.

Ukitoa uwanja wa sasa wa taifa, pamoja na ule wa shamba la bibi uliofanyiwa marekebisho, bado uwanja wa Nelson Mandela umeendelea kukaa kwenye rekodi ya viwanja vitatu bora tulivyo navyo Tanzania. Ikiwa ni pamoja na ule wa Ali Hassan Mwinyi uliopo Tabora, CCM kirumba wa Mwanza, na pengine ule wa Sheikh Abeid Karume wa Arusha....sijui, sina hakika!

Huwezi kuuzungumzia uwanja wa Nelson Mandela pasipo kumzungumzia aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa kipindi hicho, Jenerali Tumaniel Kiwelu.

Jenerali Kiwelu ndiye hasa aliyefanya ndoto ya Sumbawanga kuwa na uwanja bora kabisa wa mpira itimie. Kiwelu anakumbukwa mpaka leo, kama kiongozi shupavu, mchapakazi na mpenda maendeleo.

Moja ya simulizi alizowahi kunipa bibi yangu kuhusu Kiwelu, ni pale alipokuwa mwalimu wa shule ya msingi Mwenge.

Siku hiyo bibi alikuwa darasani. Akiwa anaendelea na majukumu yake ya kufundisha wanafunzi wake ambao walizoea kumwita Mwalimu bibi, aligundua kuwa kuna mtu alikuwa akichungulia dirishani kutokea upande wa nje wa nyuma ya darasa.

Ilimshangaza kiasi cha kumpa udadisi wa kusogea pale dirishani kutaka kujua, kulikoni mtu mzima akae nje ya darasa na kuchungulia mwalimu na wanafunzi wake mithili ya mwizi!

Lahaula! Akakutana uso kwa uso na mtu aliyemjua fika, kiongozi mkuu na 'amiri jeshi' wa mkoa wa Rukwa! Alikuwa ni jenerali Kiwelu.

Bibi alishtuka kwa kuwa hakutegemea kukutana na sura ya mkuu wa mkoa katika mazingira yale. Lakini Jenerali alimtuliza kwa tabasamu la upole kisha akammwagia pongezi za kutosha kwa jinsi alivyowajibika kikamilifu kuwaelemisha watoto. Zaidi sana alimpa pole kutokana na mazingira mabovu ya kazi, ikiwemo ukosefu wa madawati ya watoto pamoja na vitendea kazi vingine.

Baada ya hapo Mheshimiwa Kiwelu alimuaga na kumuahidi kuyafanyia kazi hayo mapungufu. Cha ajabu hakutaka japo kupita ofisini kukutana na Mwalimu mkuu, alirudi kwenye gari lake la ofisi na kuondoka zake. Kesho yake walishangaa kuona malori mawili makubwa yameleta madawati mapya!

Huyo ndiye Jenerali Kiwelu, anayekumbukwa mpaka leo na wote walioshuhudia uongozi wake.

Mtaa wa Kiwelu uliopo katikati ya Manispaa ya Sumbawanga ni sehemu ya ukumbusho wa shujaa, Jenerali Tumaniel Kiwelu.

Wakati bibi ananisimulia kisa hicho cha mkuu wa mkoa, nilikuwa na umri wa miaka saba, au nane, au tisa, lakini usiozidi kumi.

Tena niliona kama ananichelewesha, maana rafiki yangu kipenzi John alikuwa nje ananisubiri. Kama mara mbili au tatu alikuwa amesharusha mawe batini, ishara ambayo nilijua wazi ilimaanisha nini.

Tulikuwa na ratiba yetu ya kwenda kutengeneza mahindi makavu katika mtindo tuliouhusudu kuliko chochote.

Nakumbuka vizuri kabisa, wakati huo mji mzima ulitegemea kukoboa na kusaga nafaka katika mashine za watu watatu maarufu..... Kama haikuwa mashine ya Nguvumali, basi kulikuwa na mtu anaitwa Ngajiro, ikishindikana kote kulikuwa na mwarabu aliyeitwa Mselem..... Hao watatu ndiyo walikuwa wanamiliki mashine za uhakika za kusaga na kukoboa.

Eneo zilipokuwa mashine hizo hapakuwa mbali kutoka nyumbani ingawaje zilikuwa zimejipanga mbali na makazi ya watu, kama zinavyotaka sheria za afya na usalama wa makazi.

Jengo la mashine za Ngajiro ndilo lilikuwa la mwisho, baada yake yalifuata makaburi na hakukuwa na makazi ya watu tena.

Nyuma yake zilipakana na mto maarufu Sumbawanga unaoitwa mto Lwiche.

Kabla ya kufika mtoni kuna sehemu maalum ambako pumba za mpunga zilikuwa zikitupwa na kisha kuchomwa moto. Kumbuka kwa miaka ile hata mambo ya chips yalikuwa hakuna. Kwa hiyo zile pumba hazikuwa na kazi yoyote zaidi ya kutupwa, tofauti na leo ambapo zimegeuka bidhaa!

Zikishawashwa, zilikuwa zinaungua na kuteketea taratibu na hatimaye kubaki jivu tupu. Hili jivu lenye moto ndilo hasa tulilolihitaji kwaajili ya kutengeneza mahindi yetu.

Wenyewe tulipendelea kuliita jivu hilo vumba. Na kitendo cha kuweka mahindi kwenye vumba la moto ili yaive tuliita kuvumbosha. Hahaaaaa....(nimekumbuka mbali sana)

Kuvumbosha mahindi ndiyo mchezo uliotumalizia muda hata wa kucheza na watoto wenzetu. Licha ya kupigwa marufuku kila mara, na kuchapwa kila nilipobainika lakini bado sikukoma!

Mahindi yaliyokuwa yakilipuka kwa mtindo wa bisi (nyumbani ufipani tunaita mkokoli) yalikuwa ni matamu mno. Utamu wake ndiyo ulisababisha niwe navumilia fimbo za bibi, kuliko kukosa 'mikokoli'!

Baada ya kusikiliza 'kinafiki' kisa cha bibi na mkuu wake wa mkoa (maana akili yangu yangu yote ilikuwa nje), nilimtoroka bibi kwa staili ya kwenda msalani. Baada ya hapo, hakuniona tena!

Dakika kumi baadae nilikuwa na swahiba wangu John, bize 'tukivumbosha mahindi'!

Mahindi ya siku hiyo yalikuwa mazuri kweli kweli, kwa vile yasivyoisha kulipuka! Puh! Puh! Pah!
Basi ikawa sisi na mikokoli, mikokoli na sisi!

Tulikuja kushtuka jua limezama!
Midomo na mikono yetu ikiwa imejaa masizi ya vumba!

Nikamuomba mwenzangu turudi nyumbani, maana mimi sikuruhusiwa kuwa nje ya nyumba baada ya saa kumi na mbili jioni. Na mbaya zaidi muda huo ulishapita.
Tukaafikiana.

Tukiwa njiani kurudi nyumbani, ndipo tukakutana na Black Jesus!

Kuna miaka fulani Sumbawanga kulikuwa na vichaa wengi. Na pengine hawakuwa wengi kihivyo, labda walifahamika zaidi kutokana na mji kuwa mdogo.

Naweza kukumbuka baadhi yao, kuna kichaa alikuwa anaitwa Godi malangali! Kuna mwingine alikuwa anaitwa Hitla au Chababa! Kuna chizi mwingine alifahamika kwa jina la mshondoli, mwingine ninayemkumbuka ni chizi aliyeitwa Norway!

Black Jesus alikuwa ni miongoni mwa vichaa waliotamba kipindi hicho. Ilikuwa mwishoni mwa miaka ya 80 kama sio mwanzoni mwa miaka ya 90. Wenye kumbukumbu nzuri wanaweza kunisahihisha.

Tofauti na vichaa wengine, Black Jesus alikuwa ni mpole, na hakuwa mgomvi kabisa. Tena wakati mwingine alikuwa akizungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha ulioshangaza watu.
Kuna watu waliamini kuwa Black Jesus alilogwa! Wengine walidai kuwa aliwahi kuiba vile vikombe vya dhahabu kanisani (RC) akapata laana! Kwa ufupi hakuna aliyejua kwa yakini asili ya uchizi wake.

Kitu kimoja kilichokuwa dhahiri ni lafudhi yake. Lafudhi yake ilionesha kuwa hakuwa mwenyeji wa Sumbawanga. Alipozungumza lafudhi yake ilikuwa imenyooka vizuri na ilipishana kabisa na lafudhi iliyozoeleka ya wenyeji. Wala haikuwa rahisi kugundua alikuwa na asili ya wapi!

Lakini kwa upole wake, watu wengi walimpenda na mara nyingi walimpa chakula.

Kama vichaa wengine, uso wake ulikuwa mweusi tii kwa uchafu, nywele zake timtim, na kutwa nzima angeonekana akizunguka huku na kule katika eneo la soko kuu.

Kila alipotembea alikuwa na furushi kubwa lililojaa makaratasi, matambara na uchafu mwingine.

". Jesus is black! Jesus is black!"

Alisikika akizungumza peke yake kila mara na popote pale ambapo ungemkuta. Na baada ya kusema hivyo angecheka. Na hapo ungepata nafasi ya kugundua kuwa alikuwa na mwanya katikati ya meno yake ya juu.

Nadhani ndiyo maana akapewa jina la Black Jesus!

Kila jua lilipozama Black Jesus alikuwa anarudi taratibu kutoka sokoni na kuelekea eneo la nyuma ya uwanja wa Nelson Mandela ambako kulikuwa na vyumba vingi ambavyo vilikuwa kama pagala maana havikupata wapangaji. Wapangaji pekee waliovitendea haki ni wavuta bangi, wezi, na watu wasio na haya walioamua kuvigeuza kuwa sehemu ya kwenda kuhifadhia haja zao kubwa!

Kama unavyoona katika picha, hivyo vyumba ambavyo kwa sasa vimejaa wafanyabiashara, kipindi hicho viliishia kuwa mapango ya popo na sehemu ya kutupia takataka.

Black Jesus alikuwa amejichagulia mojawapo ya vyumba hivyo na kuvifanya sehemu yake ya mapumziko kila giza linapoingia.

Cha ajabu jioni ya leo Black Jesus alikuwa ametokea makaburini, na sio sokoni kama tulivyozoea.

Akili ya kitoto iliyoambatana na utukutu ikatutuma kumfuatilia!

Kuna kitu kilichotupa hamu ya kumdadisi huyu chizi siku ya leo. Ni ile haraka yake! Alikuwa anatembea haraka haraka na alionekana kama anayewahi kitu! Siku zote Black Jesus alifanya mambo yake taratibu! Alitembea taratibu! Aliongea taratibu, na hata kula, alikula taratibu sana. Kama hataki vile!

Hatua zake zilituacha lakini hatukukoma kumfuata maana tulikijua chumba chake. Akawa ametupotea machoni kwa ajili ya kiza kilichoanza kutanda.

Tulienda taratibu kufuata uelekeo wa chumba chake, wakati tukiwa tumekaribia chumba chake tulishangaa kumuona anatokea dirishani. Mara hii ameshaingia na anatoka tena?! Tulishangaa.

Hata hivyo tukalala chini ili asituone. Na hakutuona!

Safari hii akiwa kaacha furushi lake aliondoka na kuelekea upande wa kulia ambako kuna bohari la serikali, mwendo wake ukiwa ni ule ule wa haraka.

Tulitazamana na mwenzangu kwa mshangao, kisha tukacheka!

"Anaenda wapi huyu chizi?"

Macho yetu yaliulizana bila majibu!

Kisha nikwamwambia John turudi nyumbani, giza limeanza kuingia. John alikuwa na ushawishi sana. Akaniambia kabla hatujaenda kwanini tusiende kuchungulia humo ndani anamolala tujue kuna nini?

Ili iweje? Sikumkubalia haraka, lakini mwisho sijui ni nguvu gani ilinijia, nikamkubilia!

Hatukuishia kuchungulia, bali tukaamua kuingia ndani kabisa kwa kupitia dirishani, maana mlango ulikuwa ni kama haupitiki, kifusi cha uchafu na udongo kilikuwa kimekula robo tatu ya nafasi ya uwazi wa mlango.

Humo ndani tukakaribishwa na harufu ya mavi ya kale, japo wahenga wanadai kuwa huwa hayanuki!

Chumba kilijaa uchafu wa kila aina, ambao hata sikuweza kuutambua isipokuwa maboksi yaliyotandazwa kama kitanda! Sikuwa na shaka ndiyo kilikuwa kitanda cha Black Jesus.

Akili ya ajabu zaidi ikatutuma tuangalie lile furushi lake ambalo lilikuwa limedondoka pembeni ya hayo maboksi.

John ndiye akawa wa kwanza kuchomoa makaratasi na matambara yaliyofundikwa juu ya furushi lile. Nilisita tena, hofu!

John twende bana!

Nilimsisitiza kwa sauti yenye ubaridi. Giza na harufu ya humu ndani vilisisimua damu yangu kwa hofu.
Je akirudi? Akitukuta humu itakuwaje? Hata kama ni mpole....huwezi jua!

Wakati ameafiki tuondoke nikaona chupa fulani iliyosindikwa kwa gunzi kwenye mdomo wake. Nikaamua kuivuta na kufanikiwa kuichomoa kutoka kwenye furushi hilo, lengo langu tujue tu kuna nini ndani ya ile chupa...
Ikawa vuta nikuvute!
Gunzi likatushinda kuchomoa. Si mimi wala John aliyeweza kulitoa.

"Twende John... Mie naondoka!"
Sauti niliyoitoa ilikuwa ya amri zaidi kuliko ombi. Na hapo hapo nikaitupa ile chupa chini na kuanza kuondoka.

Baada ya kupanda dirisha na kutoka nje, John naye alinifuata, lakini mkononi alikuwa ameshikilia ile chupa iliyotushinda kufungua!

"Yanini?" Nilimuuliza kwa mshangao.
"Tukajaribu kufungulia nyumbani..."
"Wewe...!"
Nilisita baada ya kukosa neno la kumwambia. Tulitembea haraka haraka, kimya kimya huku tukigeuka kuangalia nyuma kila mara.

Nyumba yetu na ya akina John zinapakana. Tulipofika nyumbani nikamuuliza kuhusu hiyo chupa, nikitaka kujua ataifichaje?

Ntaificha kwenye hayo maua!

Nyumba yetu ilikuwa imezungukwa na miti ubani pande zote, pamoja na aina fulani ya maua yenye kutoa vitunda fulani vidogo vidogo vyeusi.

Sikuwa na muda wa kumuaga nikaingia ndani!

Kwanza nilipokelewa na fimbo, na sikushangaa. Adhabu ya pili ikawa kuoga maji ya baridi. Hiyo ya pili ndiyo ilikuwa adhabu mbaya zaidi kwangu, kwa baridi ya Sumbawanga ya enzi zile, ilikuwa heri viboko kuliko kuoga maji ya baridi.

Nilisindikizwa bafuni kwa fimbo, huku nikikokota ndoo yangu ya chuma kuelekea bafuni. ( hizi ndoo za chuma siku hizi sizioni)

Bibi alikasirika sana siku hiyo. Nilirudi nyumbani karibia saa moja na nusu usiku. Na aliahidi kuanzia siku ile ndiyo ingekuwa mwanzo na mwisho kuniruhusu kwenda kucheza.

Babu ambaye hakuwa msemaji sana, alikasirika pia siku hiyo. Hivyo baada ya chakula cha usiku nilienda kulala mapema, maana wazee walikuwa wamenuna.

"Usisahau kuzima koroboi wewe!"

Bibi alinisisitiza kabla sijalala.

Ni kama robo saa tu ilikuwa imepita tangu nipande kitandani, tukapata ugeni wa kushtua!

Mtu mmoja aliyevalia nadhifu shati jeupe na kulichomeka vema (utadhani alitumia mwiko) katika suruali yake nyeusi alikuwa amekuja mle ndani kuulizia uwezekano wa watoto wawili waliochukua chupa kwenye moja ya vyumba vichafu cha Nelson Mandela.

Walikuwa wamebishana kwa muda na bibi, ukizingatia mtu mwenyewe alikuwa mgeni kabisa machoni pao, na hakujipambanua vema kama alikuwa askari kanzu au lah. Alichosisitiza ni kuona watoto wawili waliochukua chupa na kuonekana wameingia hapa!

Ndipo nikaja kuamshwa!

"We Folo....mlienda mandela leo?"

Sauti ya bibi ilikuwa nzito na ikanitisha kama vile sijawahi kuisikia tangu nizaliwe.

Hata hivyo nilikataa kata kata. Akaniamsha na kunipeleka sebuleni ambako gwaride la utambulisho kutoka kwa mtu asiyejulikana lilikuwa likiningoja!

" Nadhani ni huyu huyu.....eti mtoto, mlienda kuchukua nini kule Mandela?"

Alinistaajabisha sana mgeni huyu, licha ya utu uzima wake alikosoje subira hata kidogo?

Unaambiwa hata nilivyomwamkia hakuitika, alichosisitiza ni kuwa aliniona naingia kwenye chumba kimojawapo kati ya vyumba vichafu visivyo na mwenyewe vya Nelson Mandela.

Na mbona simuelewi? Anauliza au anasema?

Nilimkazia macho huku nikishangazwa na ubaridi niliokutana nao mwilini wakati tumegonganisha macho na huyu mtu. Mwangaza mdogo wa chemli ulitosha kuona nuru ya kuogofya kwenye macho yake. Lakini hata hivyo nikaendelea kumtazama kwa ujasiri wa nje ilhali ndani nikiwa nimeishiwa nguvu.

Mbona kama nimewahi kumuona huyu mtu? Nilimuonea wapi? Lini? Kafuata nini? Ile chupa ya Black Jesus inamuhusu nini huyu baba? Au katumwa?

Nikakataa kata kata! Sijawahi na huwa siingii katika vyumba vile vyenye giza vya Nelson Mandela.

Tena baada ya kumkatalia hivyo nilimuoma ametabasamu ghafla na kuonekana kuafikiana na mimi, kisha akawageukia babu na bibi na kuwataka radhi kwa usumbufu. Akakiri kwa maneno yake kuwa ni kweli atakuwa amenifananisha! Lakini niligundua kitu kama kejeli katika kauli na macho yake.

Kabisa nilihisi...mdomoni alikana, lakini macho yake yaliongea. Wewe ndiye uliyechukua ile chupa, na utanieleza ilipo!
Hayo niliyaona dhahiri kwenye macho yake.

Akaaga na kuondoka.

Ukabaki mjadala kwa babu na bibi.
Huyu ni nani? Mbona simjui kabisa?
Alihoji zaidi bibi kwa wasiwasi.

Lakini babu alikuwa mtulivu na alionekana kumezwa na imani ya askari kanzu aliyekuwa kwenye majukumu yake ya kipelelezi...

Ila bibi alikataa....babu akamshangaa. Nikaulizwa tena nikataa...

Kisha nikaamriwa nikalale.
Nikarudi zangu chumbani, huku nikiwa na hofu kubwa sana moyoni.

Macho ya yule mtu yakawa kama tochi iliyoendelea kunimulika akilini.

Japo nilitakiwa kuzima kibatari, lakini nilijiapiza kuwa sitazima tena kibatari badala yake ningepunguza tu utambi.
Waliotumia vibatali wanajua adha hii. Maana asubuhi unaweza kuamka ukiingiza kidole puani ni moshi mtupu utafikiri 'egzost' ya gari.

Kuna kitu kilikuwa kinanitisha kwa sasa. Dirisha la chumba changu lilikuwa linatazama uchochoroni....ndiyo uchochoro unaoelekea nyuma na kukutana na lile jalala au dampo, kisha uwanja wa Nelson Mandela!

Kumetokea nini?

Mawazo na mashaka niliyokuwa nayo hayakuweza kupiku uzito wa usingizi uliokuwa unabembembea kwenye papi za macho yangu. Sikuchukua raundi, nikawa nimelala. Nililala bila kuzima kibatari.

Usiku wa manane mvua ilianza kunyesha. Baridi ikaongezeka, nikajikunja vizuri zaidi ndani ya blanket langu. Nikaendelea kuuchapa.

Kisha ndoto ya ajabu ikanijia. Nikaota nikiwa nimelala pale pale kitandani tena baridi ikiwa imezidi kunipiga na upepo unavuma kama vile niko nje, lile blanket lisifae kitu!

Nikainua uso wangu kutazama dirishani, nikaona dirisha liko wazi!

Ajabu zaidi ni kwamba mvua ikawa inapita dirishani, kisha inakunja kona na kuja kuninyeshea usoni! Mvua gani hii ya kishetani? Mvua inakata kona kama L? Tena inachagua kuninyeshea usoni tu, ikiacha maeneo mengine makavu kabisa!

Mshangao ulipozidi ndoto ikakatika!
Moyo ulikuwa unapiga kwa nguvu sana. Nikasema loh, afadhali! Ndoto nyingine hizi!

Ngoja niendeleee kulala...nikajiambia! Kabla sijajifunika blanket hadi usoni, nikashangaa amenimwagia tena maji!

Na wala hakuyatoa mbali, aliyochota kwa kutumia kata kwenye mtungi uliokuwa kwenye pembe ya chumba changu hiki hiki, mkono wa kushoto tu ukishavuka mlangoni.

Nikajipangusa yale maji huku nikijaribu kukaa na kumtazama vizuri. Alikuwa amevaa nguo zile zile, shati jeupe na suruali nyeusi. Tena inaonekana hakuwa amethubutu kuonja hata lepe la usingizi.

" Chupa yangu iko wapi?"
Aliniuliza kwa sauti ya kutosha, wala hakuonesha kuogopa kuamsha waliolala!

Mara ya kwanza kupata hisia za kukaukiwa mate ilikuwa ni siku hiyo. Na mara mbili nilizojaribu kumeza mate niliambulia patupu. Kinywa hakikuwa na mate kabisa!

"Aliondoka nayo John!" Nilimjibu huku nikiwa siamini kama sauti yangu ilitokea mdomoni au sehemu nyingine! Hofu niliyokuwa nayo ni zaidi ya hiyo uliyonayo wewe!

"Haya nipeleke kwao....!"
Asiyejulikana aliniamuru huku akinifunua kwa nguvu na kuruhusu baridi kali ilinichape miguuni. Halafu akaniinua na kunitoa kitandani bila huruma.

Ndipo nikagundua kuwa madirisha mawili ya mbao yaliyotenganishwa na kizingiti cha mbao yalikuwa wazi.

Ndiyo! Madirisha mengi ya kwenye nyumba zetu za kimaskini yalikuwa hivyo. Hakukuwa na nondo wala grill za aina yoyote. Madirisha ya chumba changu yalikuwa mfano wa nusu mbili za milango iliyotenganishwa na huo ubao katikati ambao ndio ulikuwa na misumari iliyotumika kama komeo.

Alinisogeza dirishani, akaniinua na kunipenyeza hapo huku akiniamuru nirukie nje. Wakati anafanya hivyo nilimuona akitabasamu, ndipo nikauona mwanya wake kwa mara nyingine.

Wakati nashangazwa na hayo nilimsikia akitamka yale maneno yake, kama mtu anayeimba.....

"Jesus is black! Jesus is black! Jesus is..."

Nashangaa kwanini sikuzirai; huyu bwana hakuwa mwingine zaidi ya BLACK JESUS mwenyewe!

Hiki ni moja ya visa vingi vya ukweli nilivyopitia utotoni nikiwa na bibi yangu.

Ntamalizia baadae, mchana!BLACK JESUS

Ntamalizia baadae, mchana!......

SEHEMU YA PILI

BLACK JESUS (Tamati)

Baada ya kunipitisha dirishani, yeye pia alijipenyeza na kurukia nje kabla hata sijainuka pale chini nilipoangukia.

Akanishika mkono wangu kwa nguvu kisha akanisukuma kwa nguvu kiasi cha kupepesuka, japo sikuanguka. Alichonifanya hakikutofautiana na mfugaji anavyoswaga mfugo wake!

Ulikuwa ni msafara kuelekea nyumbani kwa kina John. Alinitanguliza kama msukule, na kwa namna ya ajabu sikuwa na nguvu japo ya kupiga kelele za kuomba msaada achilia mbali kukimbia. Black Jesus alikuwa amenishika pabaya.

Kiguu na njia mpaka mbele ya mlango wa nyumba ya kina John. Nikamuelekeza kwa kidole kuwa humo ndimo alimo mwenye chupa yake.

Akanikazia macho kisha akaniuliza kwa sauti ya kunong'onona.
"Una hakika huyo mwenzako aliyechukua chupa yangu anakaa humu?"

Nilimwitikia kwa kichwa huku nikimtazama kwa macho yaliyojaa hofu. Bado nilikuwa siamini kama huyu ndiye yule Black Jesus, mwendawazimu aliyeshinda kutwa akizunguka huku na kule akiwa na mazagazaga yake ya kiendawazimu!

Nilitamani Mungu afanye muujiza jua liwake ghafla, kisha watu wote watoke majumbani mwao na kuja hapa nilipo ili tushirikiane kumshangaa kiumbe huyu ambaye kwa sasa sikumtofautishi na zimwi au jini. Kichaa mchana kumbe usiku ni mzima kama jiwe?

Wakati nafikiria hayo ambayo kimsingi hayawezekani kutokea, alitoa kitu kama gundi ya karatasi(soltape) kisha akaifungua na kunibandika nayo mdomoni ili nisiweze kupiga kelele. Baada ya hapo akanifunga kamba miguuni na mikononi, ndipo akanisomba kimzobemzobe na kwenda kunificha kwenye moja ya vichaka vya maua yaliyozunguka nyumba yetu.

Yote haya niliyaona kama mwendelezo wa ndoto iliyoanzia chumbani kwangu wakati mvua ya ajabu ikiwa inapita dirishani na kunifuata kitandani. Sikuwa na nguvu ya kubisha wala kujitetea.

Kulikuwa na harufu fulani kwenye ile soltape iliyofungwa mdomoni iliyonifanya nipige chafya kama mbili au tatu. Tena nilipiga kwa tabu sana. Hebu fikiria mtu upige chafya huku mdomo ukiwa umefungwa, hiyo chafya inatofautiana vipi na chafya ya mbuzi?

Akiwa ameridhishwa na hizo chafya, nilimuona akigeuka taratibu na kuelekea kwenye moja ya madirisha ya nyumba ya kina John. Sikufanikiwa kuona alichokifanya kabla fahamu hazijanitoka!

*****

Raia wema walikuwa wameniokota asubuhi kwenye yale maua na kunipeleka nyumbani.

Inavyoonesha bibi hakuwa na habari kama mjukuu wake sikuwa nimelala ndani. Lakini alivyokwenda chumbani na kwenda kukuta kitanda kitupu huku dirisha likiwa wazi, akaamini alichoambiwa na wale wasamaria.

Nilikuwa natetemeka kwa baridi iliyonipiga usiku kucha mfano wa kifaranga cha kuku. Baridi ilikuwa imepenya hadi kwenye mifupa.

Walijaribu kuniuliza hili na lile lakini sikuweza kuwajibu lolote zaidi ya kutoa machozi kimya kimya. Sikuwa sawa kisaikolojia.

Ndiyo maana ikashauriwa nipewe chai ya moto au uji. Bibi akaniandalia chai nzito na mayai mawili ya bata ambao tulikuwa tukiwafuga. Kidogo siha yangu ikarejea kwenye unafuu.

Hata hivyo ilishauriwa nipumzishwe chumbani kwa muda ili kuruhusu akili yangu ikae sawa kabla ya kuwasimulia kilichonikuta. Lakini mpaka muda huo kila mtu alikuwa anasema lake. Wengine waliamini tukio hilo lilikuwa la kishirikina, lakini kuna wengine walidhani pengine nilikuwa nimepatwa na zile ndoto ambazo huwafanya watu wainuke na kufanya vitendo vingi ilhali wakiwa bado usingizini.

Ni muda huo huo ndipo mama yake rafiki yangu John alipoingia pale ndani na kutoa taarifa iliyozua taharuki mpya. John alikuwa haonekani, na dirisha la chumba chake lilikutwa likiwa wazi huku milango yote ya nyumba yao ikiwa imefungwa.

Hapo ikabidi wazee wote wakiongozwa na bibi aliyekwishawadodosa kuhusiana na ule ugeni wa mtu asiyefahamika aliyekuja kuniulizia jana usiku, wanizingire upya na kunihoji kwa msisitizo wa kipekee.

Kugundua kwamba John pia alikuwa ametekwa na Black Jesus, sikuona haja ya kuendelea kuficha. Nikaamua kuanika ukweli wote hadharani, kuanzia ule muda tumekutana naye akitokea makaburini mpaka tulivyoenda kuchukua chupa yake iliyosindikwa kwa gunzi lililotushinda kufungua kwenye chumba chake pale uwanjani.

Nilishuhudia jinsi walivyopigwa butwaa kwa maelezo niliyowapa. Ni dhahiri, sehemu ya mshangao wao ilikuwa ikinihoji ni kwa vipi tulipata ujasiri wa kwenda kufukunyua siri za mwendawazimu yule asiye na ugomvi na mtu?

Sikuwaficha pia kuhusu mtu aliyeniingilia usiku kwa mbinu za mizimu kama sio kijasusi. Na nilipotanabahisha kwamba mtu huyo ambaye sikuwa na shaka ndiye aliyemteka John alikuwa ni yule kichaa maarufu Black Jesus, miguno iliwatoka wazee wa watu kwa mshangao!

Ikashauriwa kuwa ile chupa ijaribu kutafutwa kwenye maua ambayo John alikusudia kuificha. Hisia zilinijia kuwa usiku ule John hakuweza kukumbuka sehemu hasa alipoificha ile chupa, hivyo ikamchukiza na kumlazimu Black Jesus kuondoka naye baada ya kuikosa.

Wazee walianza zoezi la kufukunyua hapa na pale kuzunguka nyumba yetu. Baada ya dakika kumi na tano mtu mmoja alikuwa amekutana chupa nyeusi ilikuwa imeshindiliwa kwa gunzi. Na walipoileta mbele yangu kwa utambuzi, niliitikia kwa kichwa huku nikitetemeka kwa hofu. Mambo yalikuwa yamebadilika kwa kasi sana. Kutoka kwenye 'kuvumbosha mahindi' na kufikia hatua ya kutekana?! Halikuwa jambo dogo. Tena nilijuta kuliko unavyoweza kufikiria.

Swala likaja, ile chupa ifunguliwe au ipelekwe kituo cha polisi kwa uchunguzi zaidi?

Yakaibuka malumbano na mvutano wa hapa na pale, lakini kundi liliongozwa na mjumbe wa nyumba kumi ambaye tayari tulishakuwa naye hapa, lilishinda na kuafikiana kuifungua chupa.

Akachaguliwa kijana mmoja mwenye nguvu achomoe gunzi ili waone kilichokuwemo ndani ya chupa.

Aliibana ile chupa katikati ya miguu yake na kuvuta lile gunzi kwa nguvu mpaka akafanikiwa kulichomoa. Watu wote walikuwa wamemtumbulia macho kijana huyo kusubiri kuona kilichokuwemo ndani ya chupa.

" Kuna nini humo?" Mtu mmoja aliropoka baada ya kukosa simile. Waoga wachache walianza kurudi nyuma taratibu katika mkao ambao ungewawezesha kutimua mbio, endapo chochote cha kuhatarisha usalama wao kingetokea.

Huyu kijana baada ya kutikisa, kuchungulia na kuigeuza ile chupa huku na kule, aliwaomba watu wampatie kitu kama sahani au sinia. Kabla mshangao hawaujawamaliza, mtu mmoja alileta sahani.

Huyo kijana akaanza kumimina kitu kisichoeleweka kutoka ndani ya ile chupa kuelekea kwenye sahani aliyopewa. Ilichukua sekunde kadhaa kabla ya uji mzito uliometameta mfano wa madini ya fedha uliopoanza kububujikia taratibu kwenye ile sahani.

Ukimya uliokuwepo pale uwani ulidhihirisha hofu waliyokuwa nayo watu wote. Ile sahani ikaanza kuzungushwa ili kila mwenye ufahamu aweze kusema chochote kuhusiana na uji huo ambao ni dhahiri ulikuwa ni aina fulani ya madini adimu.

"Zebaki!" Mtu mmoja aliropoka.
"Ndiyo nini?" Mwingine akahoji.
"Ni aina ya madini...!"

Mvurugano ulioibuka ulipelekea taarifa zipelekwe kituo cha polisi.

Polisi walikuja na kuchukua ile chupa. Mimi pia nilichukuliwa, pamoja na bibi na mjumbe wa nyumba kumi kwa ajili ya kwenda kutoa maelezo ya kuwasaidia polisi.

Mpaka saa sita mchana tulikuwa tumerudi nyumbani baada ya kutoa ushirikiano uliowatosheleza polisi. Nilikuwa hoi kwa uchovu.

Ile chupa yenye madini ya zebaki ilibaki polisi.

Msako wa kumsaka Black Jesus na mtoto John ulianza. Cha ajabu siku hiyo Black Jesus hakuonekana kabisa sehemu zote alizozoeleka. Na hata kwenye chumba chake alichokitumia kulala kule Nelson Mandela, hakuwepo wala mizigo yake haikuonekana. Ni wazi Black Jesus alidhihirika kuwa mtu hatari ambaye hakuwa kichaa kama tulivyodhani.

Taarifa ziligaa mjini kwa kasi ya ajabu. Mji mzima ukawa na habari za matukio ya Black Jesus na jinsi alivyosakwa na polisi.

Mtaa wetu ulikuwa umezizima kwa simanzi na hofu ya majanga mazito ya kupotelewa na mtoto John. Hali yangu ndiyo ilikuwa mbaya zaidi. Kila nilipomfikiria John na jinsi jana jioni tulivyokuwa tukifurahia pamoja 'mikokoli' nilikosa raha. Machozi yakawa yananitoka muda wote.

Usiku ukaingia. Si John wala black Jesus aliyekuwa amepatikana.

Wazee wa mtaa wakiongozwa na mjumbe wa nyumba kumi, walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa kina John huku vikao vya namna ya kuendesha uchunguzi na ukombozi wa mtoto John vikiwa vimepamba moto.

Kwenye saa mbili askari polisi wawili walikuja kwa lengo la kuwafariji wazazi wa John na kuwatia moyo kuhusiana na walipofikia juu ya harakati za kumpata John. Lakini wazee wenye hekima waligundua kuwa kazi ilishakuwa ngumu na askari hao walitumwa tu kuja kuangalia kama kuna lolote jipya kuhusiana utekwaji wa John.

Polisi waliondoka, wazee wakaendelea kuwepo. Kwa namna fulani ni kama walikuwa wameanza maombolezo ya kuondokewa na mtoto John. Mara kadhaa kilio cha uchungu cha mama John kilisikika, kisha akatulizwa na wanawake wenzake. Hali ilitia simanzi mno.

Watu wakiwa wanaendelea kuota moto, kwenye majira ya saa nne na nusu usiku walishangaa kumuona mtoto John akiingia pale nyumbani huku akiwa anakimbia kwa hofu na mashaka. Ilikuwa kama ndoto.

Alikuwa amechafuka hafai! Yowe kubwa lilisikika na haikujulikana mara moja kama ilikuwa shangwe au mshangao. Watu waliokuwa wamerejea majumbani mwao walifurika upya nyumbani kwa kina John.

John mwenyewe akapotelewa na fahamu mara tu baada ya kufika kwenye mlango wa nyumba yao. Hakika ulikuwa usiku wa hekaheka!

Baada ya kumpatia huduma ya kwanza John alizinduka. Alikuwa amechakaa kwa kiasi cha kufadhaisha. Mwili wake ulijaa vidonda na damu zilizogandiana kila sehemu. Miguuni alikuwa amechanjwachanjwa kwa vitu mithili ya wembe mkali.

Baada ya kuogeshwa kwa maji moto na kupewa chakula, John akasimulia kilichomkuta.

Kumbe ule usiku baada ya kuchomolewa chumbani kwa staili ya kushangazwa kama ilivyotokea kwangu, aliamriwa aelekeze chupa ilipo. Naye kwa hofu ya kitoto hakumficha jinsi alivyoificha chupa ile kwenye maua. Walijaribu kuisaka bila mafanikio, na ndipo kwa hasira Black Jesus akaamua kumchukua kwa kuamini kuwa alikuwa akisema uongo.

Nyuma ya bohari kuu la serikali kulikuwa na vyumba vilivyowahi kuezuliwa na mvua kubwa iliyowahi kunyesha siku za nyuma. Eneo hili lilikuwa linatazama kabisa na makaburi. Na hakukuwa na makazi ya watu. Huko ndiko John alikoenda kufichwa na kufungwa kwa kamba.

Kama isingekuwa utundu na ujasiri alipkuwa nao, leo hii tungekuwa tunaongelea mengine.

Mtoto John alifungua zile kamba kwa meno yake na kufanikiwa kutoka nje ya jengo alokuwa kafichwa. Wakati anatoka ndipo akamuona Black Jesus kwa mbali akirudi na kuanza kumkimbiza kwa hasira.

John alijikuta amekimbilia kwenye mkondo wa maji ya mto Lwiche ambao umezingirwa na majani, matete na vichaka vikubwa. Ni huko ndiko alikojificha kutwa nzima akihofia kujitokeza na kudakwa na Black Jesus ambaye alionekana akimsaka huku na kule kando ya mto ule.

Ni usiku huu ndipo alipojipa ujasiri wa kutoka vichakani, akiwa ameshajeruhiwa kwa majani na miiba yenye ncha kali mpaka alipofanikiwa kutoka nje ya mto na kukimbilia nyumbani kwa staili ya kujifichaficha.

Watu walisikitika sana.

Taarifa hizi zilipowafikia polisi walikuja kumchukua kwa uchunguzi zaidi na kumrudisha nyumbani baadae sana.

Lakini walau watu walienda kulala wakiwa na amani mtoto John alikuwa hai. Japo dukuduku liliendelea kuwatafuna wote, Black Jesus alikuwa ni nani hasa? Alikuwa kajificha wapi? Alikuwa na malengo gani?
Na vipi kuhusu madini ya zebaki, alikusudia kufanyia nini?

Siku, wiki, mwezi na hatimaye miezi ilikatika bila Black Jesus kuonekana wala kusikika! Likabaki kuwa fumbo la imani.....

Siku Jenerali Tumaniel Kiwelu alipopata habari zake alituita kwenye ofisi yake, ili aweze kutufahamu na kutupongeza pia kwa ujasiri. Na picha hii hapa chini nilipiga na bibi baada ya kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Rukwa siku hiyo.

Lakini Black Jesus ni nani?
Alikuwa na lengo gani?
Na vipi kuhusu madini ya zebaki aliyokuwa akitembea nayo, alikusudia kuyafanyia nini?

Itaendelea......

.
images%20(1).jpeg
 
Sumbawanga ndiyo nyumbani kwetu, na kitongoji maarufu kiitwacho Mazwi ndiko hasa nilikozaliwa, kukulia na kujanjarukia!

Umbali wa takribani mita mia moja tu kutoka nyumbani kwetu, mahali nilipokulia na kuishi na bibi na babu yangu, ndipo unapopatikana uwanja maarufu mkoani Rukwa uliopewa jina la baba wa taifa la Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, yaani Nelson Mandela Stadium.

Ukitoa uwanja wa sasa wa taifa, pamoja na ule wa shamba la bibi uliofanyiwa marekebisho, bado uwanja wa Nelson Mandela umeendelea kukaa kwenye rekodi ya viwanja vitatu bora tulivyo navyo Tanzania. Ikiwa ni pamoja na ule wa Ali Hassan Mwinyi uliopo Tabora, CCM kirumba wa Mwanza, na pengine ule wa Sheikh Abeid Karume wa Arusha....sijui, sina hakika!

Huwezi kuuzungumzia uwanja wa Nelson Mandela pasipo kumzungumzia aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa kipindi hicho, Jenerali Tumaniel Kiwelu.

Jenerali Kiwelu ndiye hasa aliyefanya ndoto ya Sumbawanga kuwa na uwanja bora kabisa wa mpira itimie. Kiwelu anakumbukwa mpaka leo, kama kiongozi shupavu, mchapakazi na mpenda maendeleo.

Moja ya simulizi alizowahi kunipa bibi yangu kuhusu Kiwelu, ni pale alipokuwa mwalimu wa shule ya msingi Mwenge.

Siku hiyo bibi alikuwa darasani. Akiwa anaendelea na majukumu yake ya kufundisha wanafunzi wake ambao walizoea kumwita Mwalimu bibi, aligundua kuwa kuna mtu alikuwa akichungulia dirishani kutokea upande wa nje wa nyuma ya darasa.

Ilimshangaza kiasi cha kumpa udadisi wa kusogea pale dirishani kutaka kujua, kulikoni mtu mzima akae nje ya darasa na kuchungulia mwalimu na wanafunzi wake mithili ya mwizi!

Lahaula! Akakutana uso kwa uso na mtu aliyemjua fika, kiongozi mkuu na 'amiri jeshi' wa mkoa wa Rukwa! Alikuwa ni jenerali Kiwelu.

Bibi alishtuka kwa kuwa hakutegemea kukutana na sura ya mkuu wa mkoa katika mazingira yale. Lakini Jenerali alimtuliza kwa tabasamu la upole kisha akammwagia pongezi za kutosha kwa jinsi alivyowajibika kikamilifu kuwaelemisha watoto. Zaidi sana alimpa pole kutokana na mazingira mabovu ya kazi, ikiwemo ukosefu wa madawati ya watoto pamoja na vitendea kazi vingine.

Baada ya hapo Mheshimiwa Kiwelu alimuaga na kumuahidi kuyafanyia kazi hayo mapungufu. Cha ajabu hakutaka japo kupita ofisini kukutana na Mwalimu mkuu, alirudi kwenye gari lake la ofisi na kuondoka zake. Kesho yake walishangaa kuona malori mawili makubwa yameleta madawati mapya!

Huyo ndiye Jenerali Kiwelu, anayekumbukwa mpaka leo na wote walioshuhudia uongozi wake.

Mtaa wa Kiwelu uliopo katikati ya Manispaa ya Sumbawanga ni sehemu ya ukumbusho wa shujaa, Jenerali Tumaniel Kiwelu.

Wakati bibi ananisimulia kisa hicho cha mkuu wa mkoa, nilikuwa na umri wa miaka saba, au nane, au tisa, lakini usiozidi kumi.

Tena niliona kama ananichelewesha, maana rafiki yangu kipenzi John alikuwa nje ananisubiri. Kama mara mbili au tatu alikuwa amesharusha mawe batini, ishara ambayo nilijua wazi ilimaanisha nini.

Tulikuwa na ratiba yetu ya kwenda kutengeneza mahindi makavu katika mtindo tuliouhusudu kuliko chochote.

Nakumbuka vizuri kabisa, wakati huo mji mzima ulitegemea kukoboa na kusaga nafaka katika mashine za watu watatu maarufu..... Kama haikuwa mashine ya Nguvumali, basi kulikuwa na mtu anaitwa Ngajiro, ikishindikana kote kulikuwa na mwarabu aliyeitwa Mselem..... Hao watatu ndiyo walikuwa wanamiliki mashine za uhakika za kusaga na kukoboa.

Eneo zilipokuwa mashine hizo hapakuwa mbali kutoka nyumbani ingawaje zilikuwa zimejipanga mbali na makazi ya watu, kama zinavyotaka sheria za afya na usalama wa makazi.

Jengo la mashine za Ngajiro ndilo lilikuwa la mwisho, baada yake yalifuata makaburi na hakukuwa na makazi ya watu tena.

Nyuma yake zilipakana na mto maarufu Sumbawanga unaoitwa mto Lwiche.

Kabla ya kufika mtoni kuna sehemu maalum ambako pumba za mpunga zilikuwa zikitupwa na kisha kuchomwa moto. Kumbuka kwa miaka ile hata mambo ya chips yalikuwa hakuna. Kwa hiyo zile pumba hazikuwa na kazi yoyote zaidi ya kutupwa, tofauti na leo ambapo zimegeuka bidhaa!

Zikishawashwa, zilikuwa zinaungua na kuteketea taratibu na hatimaye kubaki jivu tupu. Hili jivu lenye moto ndilo hasa tulilolihitaji kwaajili ya kutengeneza mahindi yetu.

Wenyewe tulipendelea kuliita jivu hilo vumba. Na kitendo cha kuweka mahindi kwenye vumba la moto ili yaive tuliita kuvumbosha. Hahaaaaa....(nimekumbuka mbali sana)

Kuvumbosha mahindi ndiyo mchezo uliotumalizia muda hata wa kucheza na watoto wenzetu. Licha ya kupigwa marufuku kila mara, na kuchapwa kila nilipobainika lakini bado sikukoma!

Mahindi yaliyokuwa yakilipuka kwa mtindo wa bisi (nyumbani ufipani tunaita mkokoli) yalikuwa ni matamu mno. Utamu wake ndiyo ulisababisha niwe navumilia fimbo za bibi, kuliko kukosa 'mikokoli'!

Baada ya kusikiliza 'kinafiki' kisa cha bibi na mkuu wake wa mkoa (maana akili yangu yangu yote ilikuwa nje), nilimtoroka bibi kwa staili ya kwenda msalani. Baada ya hapo, hakuniona tena!

Dakika kumi baadae nilikuwa na swahiba wangu John, bize 'tukivumbosha mahindi'!

Mahindi ya siku hiyo yalikuwa mazuri kweli kweli, kwa vile yasivyoisha kulipuka! Puh! Puh! Pah!
Basi ikawa sisi na mikokoli, mikokoli na sisi!

Tulikuja kushtuka jua limezama!
Midomo na mikono yetu ikiwa imejaa masizi ya vumba!

Nikamuomba mwenzangu turudi nyumbani, maana mimi sikuruhusiwa kuwa nje ya nyumba baada ya saa kumi na mbili jioni. Na mbaya zaidi muda huo ulishapita.
Tukaafikiana.

Tukiwa njiani kurudi nyumbani, ndipo tukakutana na Black Jesus!

Kuna miaka fulani Sumbawanga kulikuwa na vichaa wengi. Na pengine hawakuwa wengi kihivyo, labda walifahamika zaidi kutokana na mji kuwa mdogo.

Naweza kukumbuka baadhi yao, kuna kichaa alikuwa anaitwa Godi malangali! Kuna mwingine alikuwa anaitwa Hitla au Chababa! Kuna chizi mwingine alifahamika kwa jina la mshondoli, mwingine ninayemkumbuka ni chizi aliyeitwa Norway!

Black Jesus alikuwa ni miongoni mwa vichaa waliotamba kipindi hicho. Ilikuwa mwishoni mwa miaka ya 80 kama sio mwanzoni mwa miaka ya 90. Wenye kumbukumbu nzuri wanaweza kunisahihisha.

Tofauti na vichaa wengine, Black Jesus alikuwa ni mpole, na hakuwa mgomvi kabisa. Tena wakati mwingine alikuwa akizungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha ulioshangaza watu.
Kuna watu waliamini kuwa Black Jesus alilogwa! Wengine walidai kuwa aliwahi kuiba vile vikombe vya dhahabu kanisani (RC) akapata laana! Kwa ufupi hakuna aliyejua kwa yakini asili ya uchizi wake.

Kitu kimoja kilichokuwa dhahiri ni lafudhi yake. Lafudhi yake ilionesha kuwa hakuwa mwenyeji wa Sumbawanga. Alipozungumza lafudhi yake ilikuwa imenyooka vizuri na ilipishana kabisa na lafudhi iliyozoeleka ya wenyeji. Wala haikuwa rahisi kugundua alikuwa na asili ya wapi!

Lakini kwa upole wake, watu wengi walimpenda na mara nyingi walimpa chakula.

Kama vichaa wengine, uso wake ulikuwa mweusi tii kwa uchafu, nywele zake timtim, na kutwa nzima angeonekana akizunguka huku na kule katika eneo la soko kuu.

Kila alipotembea alikuwa na furushi kubwa lililojaa makaratasi, matambara na uchafu mwingine.

". Jesus is black! Jesus is black!"

Alisikika akizungumza peke yake kila mara na popote pale ambapo ungemkuta. Na baada ya kusema hivyo angecheka. Na hapo ungepata nafasi ya kugundua kuwa alikuwa na mwanya katikati ya meno yake ya juu.

Nadhani ndiyo maana akapewa jina la Black Jesus!

Kila jua lilipozama Black Jesus alikuwa anarudi taratibu kutoka sokoni na kuelekea eneo la nyuma ya uwanja wa Nelson Mandela ambako kulikuwa na vyumba vingi ambavyo vilikuwa kama pagala maana havikupata wapangaji. Wapangaji pekee waliovitendea haki ni wavuta bangi, wezi, na watu wasio na haya walioamua kuvigeuza kuwa sehemu ya kwenda kuhifadhia haja zao kubwa!

Kama unavyoona katika picha, hivyo vyumba ambavyo kwa sasa vimejaa wafanyabiashara, kipindi hicho viliishia kuwa mapango ya popo na sehemu ya kutupia takataka.

Black Jesus alikuwa amejichagulia mojawapo ya vyumba hivyo na kuvifanya sehemu yake ya mapumziko kila giza linapoingia.

Cha ajabu jioni ya leo Black Jesus alikuwa ametokea makaburini, na sio sokoni kama tulivyozoea.

Akili ya kitoto iliyoambatana na utukutu ikatutuma kumfuatilia!

Kuna kitu kilichotupa hamu ya kumdadisi huyu chizi siku ya leo. Ni ile haraka yake! Alikuwa anatembea haraka haraka na alionekana kama anayewahi kitu! Siku zote Black Jesus alifanya mambo yake taratibu! Alitembea taratibu! Aliongea taratibu, na hata kula, alikula taratibu sana. Kama hataki vile!

Hatua zake zilituacha lakini hatukukoma kumfuata maana tulikijua chumba chake. Akawa ametupotea machoni kwa ajili ya kiza kilichoanza kutanda.

Tulienda taratibu kufuata uelekeo wa chumba chake, wakati tukiwa tumekaribia chumba chake tulishangaa kumuona anatokea dirishani. Mara hii ameshaingia na anatoka tena?! Tulishangaa.

Hata hivyo tukalala chini ili asituone. Na hakutuona!

Safari hii akiwa kaacha furushi lake aliondoka na kuelekea upande wa kulia ambako kuna bohari la serikali, mwendo wake ukiwa ni ule ule wa haraka.

Tulitazamana na mwenzangu kwa mshangao, kisha tukacheka!

"Anaenda wapi huyu chizi?"

Macho yetu yaliulizana bila majibu!

Kisha nikwamwambia John turudi nyumbani, giza limeanza kuingia. John alikuwa na ushawishi sana. Akaniambia kabla hatujaenda kwanini tusiende kuchungulia humo ndani anamolala tujue kuna nini?

Ili iweje? Sikumkubalia haraka, lakini mwisho sijui ni nguvu gani ilinijia, nikamkubilia!

Hatukuishia kuchungulia, bali tukaamua kuingia ndani kabisa kwa kupitia dirishani, maana mlango ulikuwa ni kama haupitiki, kifusi cha uchafu na udongo kilikuwa kimekula robo tatu ya nafasi ya uwazi wa mlango.

Humo ndani tukakaribishwa na harufu ya mavi ya kale, japo wahenga wanadai kuwa huwa hayanuki!

Chumba kilijaa uchafu wa kila aina, ambao hata sikuweza kuutambua isipokuwa maboksi yaliyotandazwa kama kitanda! Sikuwa na shaka ndiyo kilikuwa kitanda cha Black Jesus.

Akili ya ajabu zaidi ikatutuma tuangalie lile furushi lake ambalo lilikuwa limedondoka pembeni ya hayo maboksi.

John ndiye akawa wa kwanza kuchomoa makaratasi na matambara yaliyofundikwa juu ya furushi lile. Nilisita tena, hofu!

John twende bana!

Nilimsisitiza kwa sauti yenye ubaridi. Giza na harufu ya humu ndani vilisisimua damu yangu kwa hofu.
Je akirudi? Akitukuta humu itakuwaje? Hata kama ni mpole....huwezi jua!

Wakati ameafiki tuondoke nikaona chupa fulani iliyosindikwa kwa gunzi kwenye mdomo wake. Nikaamua kuivuta na kufanikiwa kuichomoa kutoka kwenye furushi hilo, lengo langu tujue tu kuna nini ndani ya ile chupa...
Ikawa vuta nikuvute!
Gunzi likatushinda kuchomoa. Si mimi wala John aliyeweza kulitoa.

"Twende John... Mie naondoka!"
Sauti niliyoitoa ilikuwa ya amri zaidi kuliko ombi. Na hapo hapo nikaitupa ile chupa chini na kuanza kuondoka.

Baada ya kupanda dirisha na kutoka nje, John naye alinifuata, lakini mkononi alikuwa ameshikilia ile chupa iliyotushinda kufungua!

"Yanini?" Nilimuuliza kwa mshangao.
"Tukajaribu kufungulia nyumbani..."
"Wewe...!"
Nilisita baada ya kukosa neno la kumwambia. Tulitembea haraka haraka, kimya kimya huku tukigeuka kuangalia nyuma kila mara.

Nyumba yetu na ya akina John zinapakana. Tulipofika nyumbani nikamuuliza kuhusu hiyo chupa, nikitaka kujua ataifichaje?

Ntaificha kwenye hayo maua!

Nyumba yetu ilikuwa imezungukwa na miti ubani pande zote, pamoja na aina fulani ya maua yenye kutoa vitunda fulani vidogo vidogo vyeusi.

Sikuwa na muda wa kumuaga nikaingia ndani!

Kwanza nilipokelewa na fimbo, na sikushangaa. Adhabu ya pili ikawa kuoga maji ya baridi. Hiyo ya pili ndiyo ilikuwa adhabu mbaya zaidi kwangu, kwa baridi ya Sumbawanga ya enzi zile, ilikuwa heri viboko kuliko kuoga maji ya baridi.

Nilisindikizwa bafuni kwa fimbo, huku nikikokota ndoo yangu ya chuma kuelekea bafuni. ( hizi ndoo za chuma siku hizi sizioni)

Bibi alikasirika sana siku hiyo. Nilirudi nyumbani karibia saa moja na nusu usiku. Na aliahidi kuanzia siku ile ndiyo ingekuwa mwanzo na mwisho kuniruhusu kwenda kucheza.

Babu ambaye hakuwa msemaji sana, alikasirika pia siku hiyo. Hivyo baada ya chakula cha usiku nilienda kulala mapema, maana wazee walikuwa wamenuna.

"Usisahau kuzima koroboi wewe!"

Bibi alinisisitiza kabla sijalala.

Ni kama robo saa tu ilikuwa imepita tangu nipande kitandani, tukapata ugeni wa kushtua!

Mtu mmoja aliyevalia nadhifu shati jeupe na kulichomeka vema (utadhani alitumia mwiko) katika suruali yake nyeusi alikuwa amekuja mle ndani kuulizia uwezekano wa watoto wawili waliochukua chupa kwenye moja ya vyumba vichafu cha Nelson Mandela.

Walikuwa wamebishana kwa muda na bibi, ukizingatia mtu mwenyewe alikuwa mgeni kabisa machoni pao, na hakujipambanua vema kama alikuwa askari kanzu au lah. Alichosisitiza ni kuona watoto wawili waliochukua chupa na kuonekana wameingia hapa!

Ndipo nikaja kuamshwa!

"We Folo....mlienda mandela leo?"

Sauti ya bibi ilikuwa nzito na ikanitisha kama vile sijawahi kuisikia tangu nizaliwe.

Hata hivyo nilikataa kata kata. Akaniamsha na kunipeleka sebuleni ambako gwaride la utambulisho kutoka kwa mtu asiyejulikana lilikuwa likiningoja!

" Nadhani ni huyu huyu.....eti mtoto, mlienda kuchukua nini kule Mandela?"

Alinistaajabisha sana mgeni huyu, licha ya utu uzima wake alikosoje subira hata kidogo?

Unaambiwa hata nilivyomwamkia hakuitika, alichosisitiza ni kuwa aliniona naingia kwenye chumba kimojawapo kati ya vyumba vichafu visivyo na mwenyewe vya Nelson Mandela.

Na mbona simuelewi? Anauliza au anasema?

Nilimkazia macho huku nikishangazwa na ubaridi niliokutana nao mwilini wakati tumegonganisha macho na huyu mtu. Mwangaza mdogo wa chemli ulitosha kuona nuru ya kuogofya kwenye macho yake. Lakini hata hivyo nikaendelea kumtazama kwa ujasiri wa nje ilhali ndani nikiwa nimeishiwa nguvu.

Mbona kama nimewahi kumuona huyu mtu? Nilimuonea wapi? Lini? Kafuata nini? Ile chupa ya Black Jesus inamuhusu nini huyu baba? Au katumwa?

Nikakataa kata kata! Sijawahi na huwa siingii katika vyumba vile vyenye giza vya Nelson Mandela.

Tena baada ya kumkatalia hivyo nilimuoma ametabasamu ghafla na kuonekana kuafikiana na mimi, kisha akawageukia babu na bibi na kuwataka radhi kwa usumbufu. Akakiri kwa maneno yake kuwa ni kweli atakuwa amenifananisha! Lakini niligundua kitu kama kejeli katika kauli na macho yake.

Kabisa nilihisi...mdomoni alikana, lakini macho yake yaliongea. Wewe ndiye uliyechukua ile chupa, na utanieleza ilipo!
Hayo niliyaona dhahiri kwenye macho yake.

Akaaga na kuondoka.

Ukabaki mjadala kwa babu na bibi.
Huyu ni nani? Mbona simjui kabisa?
Alihoji zaidi bibi kwa wasiwasi.

Lakini babu alikuwa mtulivu na alionekana kumezwa na imani ya askari kanzu aliyekuwa kwenye majukumu yake ya kipelelezi...

Ila bibi alikataa....babu akamshangaa. Nikaulizwa tena nikataa...

Kisha nikaamriwa nikalale.
Nikarudi zangu chumbani, huku nikiwa na hofu kubwa sana moyoni.

Macho ya yule mtu yakawa kama tochi iliyoendelea kunimulika akilini.

Japo nilitakiwa kuzima kibatari, lakini nilijiapiza kuwa sitazima tena kibatari badala yake ningepunguza tu utambi.
Waliotumia vibatali wanajua adha hii. Maana asubuhi unaweza kuamka ukiingiza kidole puani ni moshi mtupu utafikiri 'egzost' ya gari.

Kuna kitu kilikuwa kinanitisha kwa sasa. Dirisha la chumba changu lilikuwa linatazama uchochoroni....ndiyo uchochoro unaoelekea nyuma na kukutana na lile jalala au dampo, kisha uwanja wa Nelson Mandela!

Kumetokea nini?

Mawazo na mashaka niliyokuwa nayo hayakuweza kupiku uzito wa usingizi uliokuwa unabembembea kwenye papi za macho yangu. Sikuchukua raundi, nikawa nimelala. Nililala bila kuzima kibatari.

Usiku wa manane mvua ilianza kunyesha. Baridi ikaongezeka, nikajikunja vizuri zaidi ndani ya blanket langu. Nikaendelea kuuchapa.

Kisha ndoto ya ajabu ikanijia. Nikaota nikiwa nimelala pale pale kitandani tena baridi ikiwa imezidi kunipiga na upepo unavuma kama vile niko nje, lile blanket lisifae kitu!

Nikainua uso wangu kutazama dirishani, nikaona dirisha liko wazi!

Ajabu zaidi ni kwamba mvua ikawa inapita dirishani, kisha inakunja kona na kuja kuninyeshea usoni! Mvua gani hii ya kishetani? Mvua inakata kona kama L? Tena inachagua kuninyeshea usoni tu, ikiacha maeneo mengine makavu kabisa!

Mshangao ulipozidi ndoto ikakatika!
Moyo ulikuwa unapiga kwa nguvu sana. Nikasema loh, afadhali! Ndoto nyingine hizi!

Ngoja niendeleee kulala...nikajiambia! Kabla sijajifunika blanket hadi usoni, nikashangaa amenimwagia tena maji!

Na wala hakuyatoa mbali, aliyochota kwa kutumia kata kwenye mtungi uliokuwa kwenye pembe ya chumba changu hiki hiki, mkono wa kushoto tu ukishavuka mlangoni.

Nikajipangusa yale maji huku nikijaribu kukaa na kumtazama vizuri. Alikuwa amevaa nguo zile zile, shati jeupe na suruali nyeusi. Tena inaonekana hakuwa amethubutu kuonja hata lepe la usingizi.

" Chupa yangu iko wapi?"
Aliniuliza kwa sauti ya kutosha, wala hakuonesha kuogopa kuamsha waliolala!

Mara ya kwanza kupata hisia za kukaukiwa mate ilikuwa ni siku hiyo. Na mara mbili nilizojaribu kumeza mate niliambulia patupu. Kinywa hakikuwa na mate kabisa!

"Aliondoka nayo John!" Nilimjibu huku nikiwa siamini kama sauti yangu ilitokea mdomoni au sehemu nyingine! Hofu niliyokuwa nayo ni zaidi ya hiyo uliyonayo wewe!

"Haya nipeleke kwao....!"
Asiyejulikana aliniamuru huku akinifunua kwa nguvu na kuruhusu baridi kali ilinichape miguuni. Halafu akaniinua na kunitoa kitandani bila huruma.

Ndipo nikagundua kuwa madirisha mawili ya mbao yaliyotenganishwa na kizingiti cha mbao yalikuwa wazi.

Ndiyo! Madirisha mengi ya kwenye nyumba zetu za kimaskini yalikuwa hivyo. Hakukuwa na nondo wala grill za aina yoyote. Madirisha ya chumba changu yalikuwa mfano wa nusu mbili za milango iliyotenganishwa na huo ubao katikati ambao ndio ulikuwa na misumari iliyotumika kama komeo.

Alinisogeza dirishani, akaniinua na kunipenyeza hapo huku akiniamuru nirukie nje. Wakati anafanya hivyo nilimuona akitabasamu, ndipo nikauona mwanya wake kwa mara nyingine.

Wakati nashangazwa na hayo nilimsikia akitamka yale maneno yake, kama mtu anayeimba.....

"Jesus is black! Jesus is black! Jesus is..."

Nashangaa kwanini sikuzirai; huyu bwana hakuwa mwingine zaidi ya BLACK JESUS mwenyewe!

Hiki ni moja ya visa vingi vya ukweli nilivyopitia utotoni nikiwa na bibi yangu.

Ntamalizia baadae, mchana!BLACK JESUS

Sumbawanga ndiyo nyumbani kwetu, na kitongoji maarufu kiitwacho Mazwi ndiko hasa nilikozaliwa, kukulia na kujanjarukia!

Umbali wa takribani mita mia moja tu kutoka nyumbani kwetu, mahali nilipokulia na kuishi na bibi na babu yangu, ndipo unapopatikana uwanja maarufu mkoani Rukwa uliopewa jina la baba wa taifa la Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, yaani Nelson Mandela Stadium.

Ukitoa uwanja wa sasa wa taifa, pamoja na ule wa shamba la bibi uliofanyiwa marekebisho, bado uwanja wa Nelson Mandela umeendelea kukaa kwenye rekodi ya viwanja vitatu bora tulivyo navyo Tanzania. Ikiwa ni pamoja na ule wa Ali Hassan Mwinyi uliopo Tabora, CCM kirumba wa Mwanza, na pengine ule wa Sheikh Abeid Karume wa Arusha....sijui, sina hakika!

Huwezi kuuzungumzia uwanja wa Nelson Mandela pasipo kumzungumzia aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa kipindi hicho, Jenerali Tumaniel Kiwelu.

Jenerali Kiwelu ndiye hasa aliyefanya ndoto ya Sumbawanga kuwa na uwanja bora kabisa wa mpira itimie. Kiwelu anakumbukwa mpaka leo, kama kiongozi shupavu, mchapakazi na mpenda maendeleo.

Moja ya simulizi alizowahi kunipa bibi yangu kuhusu Kiwelu, ni pale alipokuwa mwalimu wa shule ya msingi Mwenge.

Siku hiyo bibi alikuwa darasani. Akiwa anaendelea na majukumu yake ya kufundisha wanafunzi wake ambao walizoea kumwita Mwalimu bibi, aligundua kuwa kuna mtu alikuwa akichungulia dirishani kutokea upande wa nje wa nyuma ya darasa.

Ilimshangaza kiasi cha kumpa udadisi wa kusogea pale dirishani kutaka kujua, kulikoni mtu mzima akae nje ya darasa na kuchungulia mwalimu na wanafunzi wake mithili ya mwizi!

Lahaula! Akakutana uso kwa uso na mtu aliyemjua fika, kiongozi mkuu na 'amiri jeshi' wa mkoa wa Rukwa! Alikuwa ni jenerali Kiwelu.

Bibi alishtuka kwa kuwa hakutegemea kukutana na sura ya mkuu wa mkoa katika mazingira yale. Lakini Jenerali alimtuliza kwa tabasamu la upole kisha akammwagia pongezi za kutosha kwa jinsi alivyowajibika kikamilifu kuwaelemisha watoto. Zaidi sana alimpa pole kutokana na mazingira mabovu ya kazi, ikiwemo ukosefu wa madawati ya watoto pamoja na vitendea kazi vingine.

Baada ya hapo Mheshimiwa Kiwelu alimuaga na kumuahidi kuyafanyia kazi hayo mapungufu. Cha ajabu hakutaka japo kupita ofisini kukutana na Mwalimu mkuu, alirudi kwenye gari lake la ofisi na kuondoka zake. Kesho yake walishangaa kuona malori mawili makubwa yameleta madawati mapya!

Huyo ndiye Jenerali Kiwelu, anayekumbukwa mpaka leo na wote walioshuhudia uongozi wake.

Mtaa wa Kiwelu uliopo katikati ya Manispaa ya Sumbawanga ni sehemu ya ukumbusho wa shujaa, Jenerali Tumaniel Kiwelu.

Wakati bibi ananisimulia kisa hicho cha mkuu wa mkoa, nilikuwa na umri wa miaka saba, au nane, au tisa, lakini usiozidi kumi.

Tena niliona kama ananichelewesha, maana rafiki yangu kipenzi John alikuwa nje ananisubiri. Kama mara mbili au tatu alikuwa amesharusha mawe batini, ishara ambayo nilijua wazi ilimaanisha nini.

Tulikuwa na ratiba yetu ya kwenda kutengeneza mahindi makavu katika mtindo tuliouhusudu kuliko chochote.

Nakumbuka vizuri kabisa, wakati huo mji mzima ulitegemea kukoboa na kusaga nafaka katika mashine za watu watatu maarufu..... Kama haikuwa mashine ya Nguvumali, basi kulikuwa na mtu anaitwa Ngajiro, ikishindikana kote kulikuwa na mwarabu aliyeitwa Mselem..... Hao watatu ndiyo walikuwa wanamiliki mashine za uhakika za kusaga na kukoboa.

Eneo zilipokuwa mashine hizo hapakuwa mbali kutoka nyumbani ingawaje zilikuwa zimejipanga mbali na makazi ya watu, kama zinavyotaka sheria za afya na usalama wa makazi.

Jengo la mashine za Ngajiro ndilo lilikuwa la mwisho, baada yake yalifuata makaburi na hakukuwa na makazi ya watu tena.

Nyuma yake zilipakana na mto maarufu Sumbawanga unaoitwa mto Lwiche.

Kabla ya kufika mtoni kuna sehemu maalum ambako pumba za mpunga zilikuwa zikitupwa na kisha kuchomwa moto. Kumbuka kwa miaka ile hata mambo ya chips yalikuwa hakuna. Kwa hiyo zile pumba hazikuwa na kazi yoyote zaidi ya kutupwa, tofauti na leo ambapo zimegeuka bidhaa!

Zikishawashwa, zilikuwa zinaungua na kuteketea taratibu na hatimaye kubaki jivu tupu. Hili jivu lenye moto ndilo hasa tulilolihitaji kwaajili ya kutengeneza mahindi yetu.

Wenyewe tulipendelea kuliita jivu hilo vumba. Na kitendo cha kuweka mahindi kwenye vumba la moto ili yaive tuliita kuvumbosha. Hahaaaaa....(nimekumbuka mbali sana)

Kuvumbosha mahindi ndiyo mchezo uliotumalizia muda hata wa kucheza na watoto wenzetu. Licha ya kupigwa marufuku kila mara, na kuchapwa kila nilipobainika lakini bado sikukoma!

Mahindi yaliyokuwa yakilipuka kwa mtindo wa bisi (nyumbani ufipani tunaita mkokoli) yalikuwa ni matamu mno. Utamu wake ndiyo ulisababisha niwe navumilia fimbo za bibi, kuliko kukosa 'mikokoli'!

Baada ya kusikiliza 'kinafiki' kisa cha bibi na mkuu wake wa mkoa (maana akili yangu yangu yote ilikuwa nje), nilimtoroka bibi kwa staili ya kwenda msalani. Baada ya hapo, hakuniona tena!

Dakika kumi baadae nilikuwa na swahiba wangu John, bize 'tukivumbosha mahindi'!

Mahindi ya siku hiyo yalikuwa mazuri kweli kweli, kwa vile yasivyoisha kulipuka! Puh! Puh! Pah!
Basi ikawa sisi na mikokoli, mikokoli na sisi!

Tulikuja kushtuka jua limezama!
Midomo na mikono yetu ikiwa imejaa masizi ya vumba!

Nikamuomba mwenzangu turudi nyumbani, maana mimi sikuruhusiwa kuwa nje ya nyumba baada ya saa kumi na mbili jioni. Na mbaya zaidi muda huo ulishapita.
Tukaafikiana.

Tukiwa njiani kurudi nyumbani, ndipo tukakutana na Black Jesus!

Kuna miaka fulani Sumbawanga kulikuwa na vichaa wengi. Na pengine hawakuwa wengi kihivyo, labda walifahamika zaidi kutokana na mji kuwa mdogo.

Naweza kukumbuka baadhi yao, kuna kichaa alikuwa anaitwa Godi malangali! Kuna mwingine alikuwa anaitwa Hitla au Chababa! Kuna chizi mwingine alifahamika kwa jina la mshondoli, mwingine ninayemkumbuka ni chizi aliyeitwa Norway!

Black Jesus alikuwa ni miongoni mwa vichaa waliotamba kipindi hicho. Ilikuwa mwishoni mwa miaka ya 80 kama sio mwanzoni mwa miaka ya 90. Wenye kumbukumbu nzuri wanaweza kunisahihisha.

Tofauti na vichaa wengine, Black Jesus alikuwa ni mpole, na hakuwa mgomvi kabisa. Tena wakati mwingine alikuwa akizungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha ulioshangaza watu.
Kuna watu waliamini kuwa Black Jesus alilogwa! Wengine walidai kuwa aliwahi kuiba vile vikombe vya dhahabu kanisani (RC) akapata laana! Kwa ufupi hakuna aliyejua kwa yakini asili ya uchizi wake.

Kitu kimoja kilichokuwa dhahiri ni lafudhi yake. Lafudhi yake ilionesha kuwa hakuwa mwenyeji wa Sumbawanga. Alipozungumza lafudhi yake ilikuwa imenyooka vizuri na ilipishana kabisa na lafudhi iliyozoeleka ya wenyeji. Wala haikuwa rahisi kugundua alikuwa na asili ya wapi!

Lakini kwa upole wake, watu wengi walimpenda na mara nyingi walimpa chakula.

Kama vichaa wengine, uso wake ulikuwa mweusi tii kwa uchafu, nywele zake timtim, na kutwa nzima angeonekana akizunguka huku na kule katika eneo la soko kuu.

Kila alipotembea alikuwa na furushi kubwa lililojaa makaratasi, matambara na uchafu mwingine.

". Jesus is black! Jesus is black!"

Alisikika akizungumza peke yake kila mara na popote pale ambapo ungemkuta. Na baada ya kusema hivyo angecheka. Na hapo ungepata nafasi ya kugundua kuwa alikuwa na mwanya katikati ya meno yake ya juu.

Nadhani ndiyo maana akapewa jina la Black Jesus!

Kila jua lilipozama Black Jesus alikuwa anarudi taratibu kutoka sokoni na kuelekea eneo la nyuma ya uwanja wa Nelson Mandela ambako kulikuwa na vyumba vingi ambavyo vilikuwa kama pagala maana havikupata wapangaji. Wapangaji pekee waliovitendea haki ni wavuta bangi, wezi, na watu wasio na haya walioamua kuvigeuza kuwa sehemu ya kwenda kuhifadhia haja zao kubwa!

Kama unavyoona katika picha, hivyo vyumba ambavyo kwa sasa vimejaa wafanyabiashara, kipindi hicho viliishia kuwa mapango ya popo na sehemu ya kutupia takataka.

Black Jesus alikuwa amejichagulia mojawapo ya vyumba hivyo na kuvifanya sehemu yake ya mapumziko kila giza linapoingia.

Cha ajabu jioni ya leo Black Jesus alikuwa ametokea makaburini, na sio sokoni kama tulivyozoea.

Akili ya kitoto iliyoambatana na utukutu ikatutuma kumfuatilia!

Kuna kitu kilichotupa hamu ya kumdadisi huyu chizi siku ya leo. Ni ile haraka yake! Alikuwa anatembea haraka haraka na alionekana kama anayewahi kitu! Siku zote Black Jesus alifanya mambo yake taratibu! Alitembea taratibu! Aliongea taratibu, na hata kula, alikula taratibu sana. Kama hataki vile!

Hatua zake zilituacha lakini hatukukoma kumfuata maana tulikijua chumba chake. Akawa ametupotea machoni kwa ajili ya kiza kilichoanza kutanda.

Tulienda taratibu kufuata uelekeo wa chumba chake, wakati tukiwa tumekaribia chumba chake tulishangaa kumuona anatokea dirishani. Mara hii ameshaingia na anatoka tena?! Tulishangaa.

Hata hivyo tukalala chini ili asituone. Na hakutuona!

Safari hii akiwa kaacha furushi lake aliondoka na kuelekea upande wa kulia ambako kuna bohari la serikali, mwendo wake ukiwa ni ule ule wa haraka.

Tulitazamana na mwenzangu kwa mshangao, kisha tukacheka!

"Anaenda wapi huyu chizi?"

Macho yetu yaliulizana bila majibu!

Kisha nikwamwambia John turudi nyumbani, giza limeanza kuingia. John alikuwa na ushawishi sana. Akaniambia kabla hatujaenda kwanini tusiende kuchungulia humo ndani anamolala tujue kuna nini?

Ili iweje? Sikumkubalia haraka, lakini mwisho sijui ni nguvu gani ilinijia, nikamkubilia!

Hatukuishia kuchungulia, bali tukaamua kuingia ndani kabisa kwa kupitia dirishani, maana mlango ulikuwa ni kama haupitiki, kifusi cha uchafu na udongo kilikuwa kimekula robo tatu ya nafasi ya uwazi wa mlango.

Humo ndani tukakaribishwa na harufu ya mavi ya kale, japo wahenga wanadai kuwa huwa hayanuki!

Chumba kilijaa uchafu wa kila aina, ambao hata sikuweza kuutambua isipokuwa maboksi yaliyotandazwa kama kitanda! Sikuwa na shaka ndiyo kilikuwa kitanda cha Black Jesus.

Akili ya ajabu zaidi ikatutuma tuangalie lile furushi lake ambalo lilikuwa limedondoka pembeni ya hayo maboksi.

John ndiye akawa wa kwanza kuchomoa makaratasi na matambara yaliyofundikwa juu ya furushi lile. Nilisita tena, hofu!

John twende bana!

Nilimsisitiza kwa sauti yenye ubaridi. Giza na harufu ya humu ndani vilisisimua damu yangu kwa hofu.
Je akirudi? Akitukuta humu itakuwaje? Hata kama ni mpole....huwezi jua!

Wakati ameafiki tuondoke nikaona chupa fulani iliyosindikwa kwa gunzi kwenye mdomo wake. Nikaamua kuivuta na kufanikiwa kuichomoa kutoka kwenye furushi hilo, lengo langu tujue tu kuna nini ndani ya ile chupa...
Ikawa vuta nikuvute!
Gunzi likatushinda kuchomoa. Si mimi wala John aliyeweza kulitoa.

"Twende John... Mie naondoka!"
Sauti niliyoitoa ilikuwa ya amri zaidi kuliko ombi. Na hapo hapo nikaitupa ile chupa chini na kuanza kuondoka.

Baada ya kupanda dirisha na kutoka nje, John naye alinifuata, lakini mkononi alikuwa ameshikilia ile chupa iliyotushinda kufungua!

"Yanini?" Nilimuuliza kwa mshangao.
"Tukajaribu kufungulia nyumbani..."
"Wewe...!"
Nilisita baada ya kukosa neno la kumwambia. Tulitembea haraka haraka, kimya kimya huku tukigeuka kuangalia nyuma kila mara.

Nyumba yetu na ya akina John zinapakana. Tulipofika nyumbani nikamuuliza kuhusu hiyo chupa, nikitaka kujua ataifichaje?

Ntaificha kwenye hayo maua!

Nyumba yetu ilikuwa imezungukwa na miti ubani pande zote, pamoja na aina fulani ya maua yenye kutoa vitunda fulani vidogo vidogo vyeusi.

Sikuwa na muda wa kumuaga nikaingia ndani!

Kwanza nilipokelewa na fimbo, na sikushangaa. Adhabu ya pili ikawa kuoga maji ya baridi. Hiyo ya pili ndiyo ilikuwa adhabu mbaya zaidi kwangu, kwa baridi ya Sumbawanga ya enzi zile, ilikuwa heri viboko kuliko kuoga maji ya baridi.

Nilisindikizwa bafuni kwa fimbo, huku nikikokota ndoo yangu ya chuma kuelekea bafuni. ( hizi ndoo za chuma siku hizi sizioni)

Bibi alikasirika sana siku hiyo. Nilirudi nyumbani karibia saa moja na nusu usiku. Na aliahidi kuanzia siku ile ndiyo ingekuwa mwanzo na mwisho kuniruhusu kwenda kucheza.

Babu ambaye hakuwa msemaji sana, alikasirika pia siku hiyo. Hivyo baada ya chakula cha usiku nilienda kulala mapema, maana wazee walikuwa wamenuna.

"Usisahau kuzima koroboi wewe!"

Bibi alinisisitiza kabla sijalala.

Ni kama robo saa tu ilikuwa imepita tangu nipande kitandani, tukapata ugeni wa kushtua!

Mtu mmoja aliyevalia nadhifu shati jeupe na kulichomeka vema (utadhani alitumia mwiko) katika suruali yake nyeusi alikuwa amekuja mle ndani kuulizia uwezekano wa watoto wawili waliochukua chupa kwenye moja ya vyumba vichafu cha Nelson Mandela.

Walikuwa wamebishana kwa muda na bibi, ukizingatia mtu mwenyewe alikuwa mgeni kabisa machoni pao, na hakujipambanua vema kama alikuwa askari kanzu au lah. Alichosisitiza ni kuona watoto wawili waliochukua chupa na kuonekana wameingia hapa!

Ndipo nikaja kuamshwa!

"We Folo....mlienda mandela leo?"

Sauti ya bibi ilikuwa nzito na ikanitisha kama vile sijawahi kuisikia tangu nizaliwe.

Hata hivyo nilikataa kata kata. Akaniamsha na kunipeleka sebuleni ambako gwaride la utambulisho kutoka kwa mtu asiyejulikana lilikuwa likiningoja!

" Nadhani ni huyu huyu.....eti mtoto, mlienda kuchukua nini kule Mandela?"

Alinistaajabisha sana mgeni huyu, licha ya utu uzima wake alikosoje subira hata kidogo?

Unaambiwa hata nilivyomwamkia hakuitika, alichosisitiza ni kuwa aliniona naingia kwenye chumba kimojawapo kati ya vyumba vichafu visivyo na mwenyewe vya Nelson Mandela.

Na mbona simuelewi? Anauliza au anasema?

Nilimkazia macho huku nikishangazwa na ubaridi niliokutana nao mwilini wakati tumegonganisha macho na huyu mtu. Mwangaza mdogo wa chemli ulitosha kuona nuru ya kuogofya kwenye macho yake. Lakini hata hivyo nikaendelea kumtazama kwa ujasiri wa nje ilhali ndani nikiwa nimeishiwa nguvu.

Mbona kama nimewahi kumuona huyu mtu? Nilimuonea wapi? Lini? Kafuata nini? Ile chupa ya Black Jesus inamuhusu nini huyu baba? Au katumwa?

Nikakataa kata kata! Sijawahi na huwa siingii katika vyumba vile vyenye giza vya Nelson Mandela.

Tena baada ya kumkatalia hivyo nilimuoma ametabasamu ghafla na kuonekana kuafikiana na mimi, kisha akawageukia babu na bibi na kuwataka radhi kwa usumbufu. Akakiri kwa maneno yake kuwa ni kweli atakuwa amenifananisha! Lakini niligundua kitu kama kejeli katika kauli na macho yake.

Kabisa nilihisi...mdomoni alikana, lakini macho yake yaliongea. Wewe ndiye uliyechukua ile chupa, na utanieleza ilipo!
Hayo niliyaona dhahiri kwenye macho yake.

Akaaga na kuondoka.

Ukabaki mjadala kwa babu na bibi.
Huyu ni nani? Mbona simjui kabisa?
Alihoji zaidi bibi kwa wasiwasi.

Lakini babu alikuwa mtulivu na alionekana kumezwa na imani ya askari kanzu aliyekuwa kwenye majukumu yake ya kipelelezi...

Ila bibi alikataa....babu akamshangaa. Nikaulizwa tena nikataa...

Kisha nikaamriwa nikalale.
Nikarudi zangu chumbani, huku nikiwa na hofu kubwa sana moyoni.

Macho ya yule mtu yakawa kama tochi iliyoendelea kunimulika akilini.

Japo nilitakiwa kuzima kibatari, lakini nilijiapiza kuwa sitazima tena kibatari badala yake ningepunguza tu utambi.
Waliotumia vibatali wanajua adha hii. Maana asubuhi unaweza kuamka ukiingiza kidole puani ni moshi mtupu utafikiri 'egzost' ya gari.

Kuna kitu kilikuwa kinanitisha kwa sasa. Dirisha la chumba changu lilikuwa linatazama uchochoroni....ndiyo uchochoro unaoelekea nyuma na kukutana na lile jalala au dampo, kisha uwanja wa Nelson Mandela!

Kumetokea nini?

Mawazo na mashaka niliyokuwa nayo hayakuweza kupiku uzito wa usingizi uliokuwa unabembembea kwenye papi za macho yangu. Sikuchukua raundi, nikawa nimelala. Nililala bila kuzima kibatari.

Usiku wa manane mvua ilianza kunyesha. Baridi ikaongezeka, nikajikunja vizuri zaidi ndani ya blanket langu. Nikaendelea kuuchapa.

Kisha ndoto ya ajabu ikanijia. Nikaota nikiwa nimelala pale pale kitandani tena baridi ikiwa imezidi kunipiga na upepo unavuma kama vile niko nje, lile blanket lisifae kitu!

Nikainua uso wangu kutazama dirishani, nikaona dirisha liko wazi!

Ajabu zaidi ni kwamba mvua ikawa inapita dirishani, kisha inakunja kona na kuja kuninyeshea usoni! Mvua gani hii ya kishetani? Mvua inakata kona kama L? Tena inachagua kuninyeshea usoni tu, ikiacha maeneo mengine makavu kabisa!

Mshangao ulipozidi ndoto ikakatika!
Moyo ulikuwa unapiga kwa nguvu sana. Nikasema loh, afadhali! Ndoto nyingine hizi!

Ngoja niendeleee kulala...nikajiambia! Kabla sijajifunika blanket hadi usoni, nikashangaa amenimwagia tena maji!

Na wala hakuyatoa mbali, aliyochota kwa kutumia kata kwenye mtungi uliokuwa kwenye pembe ya chumba changu hiki hiki, mkono wa kushoto tu ukishavuka mlangoni.

Nikajipangusa yale maji huku nikijaribu kukaa na kumtazama vizuri. Alikuwa amevaa nguo zile zile, shati jeupe na suruali nyeusi. Tena inaonekana hakuwa amethubutu kuonja hata lepe la usingizi.

" Chupa yangu iko wapi?"
Aliniuliza kwa sauti ya kutosha, wala hakuonesha kuogopa kuamsha waliolala!

Mara ya kwanza kupata hisia za kukaukiwa mate ilikuwa ni siku hiyo. Na mara mbili nilizojaribu kumeza mate niliambulia patupu. Kinywa hakikuwa na mate kabisa!

"Aliondoka nayo John!" Nilimjibu huku nikiwa siamini kama sauti yangu ilitokea mdomoni au sehemu nyingine! Hofu niliyokuwa nayo ni zaidi ya hiyo uliyonayo wewe!

"Haya nipeleke kwao....!"
Asiyejulikana aliniamuru huku akinifunua kwa nguvu na kuruhusu baridi kali ilinichape miguuni. Halafu akaniinua na kunitoa kitandani bila huruma.

Ndipo nikagundua kuwa madirisha mawili ya mbao yaliyotenganishwa na kizingiti cha mbao yalikuwa wazi.

Ndiyo! Madirisha mengi ya kwenye nyumba zetu za kimaskini yalikuwa hivyo. Hakukuwa na nondo wala grill za aina yoyote. Madirisha ya chumba changu yalikuwa mfano wa nusu mbili za milango iliyotenganishwa na huo ubao katikati ambao ndio ulikuwa na misumari iliyotumika kama komeo.

Alinisogeza dirishani, akaniinua na kunipenyeza hapo huku akiniamuru nirukie nje. Wakati anafanya hivyo nilimuona akitabasamu, ndipo nikauona mwanya wake kwa mara nyingine.

Wakati nashangazwa na hayo nilimsikia akitamka yale maneno yake, kama mtu anayeimba.....

"Jesus is black! Jesus is black! Jesus is..."

Nashangaa kwanini sikuzirai; huyu bwana hakuwa mwingine zaidi ya BLACK JESUS mwenyewe!

Hiki ni moja ya visa vingi vya ukweli nilivyopitia utotoni nikiwa na bibi yangu.

Ntamalizia baadae, mchana!.......View attachment 763079
Daah safi sana inasisimua sana..!! Hizi.ndio fani za kujivunia.
 
Ila sio stori ya kweli ni hadithi tuu ilio changanyika na ukweli hapo kwa mkuu wa mkoa Tumainiel kiwelu. Hongera lakini.
 
Similar Discussions

21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom