Black Americans wanaondoka Tanzania na hizi ndio sababu zao

Kama mnavyojua hawa black Americans walikuja kwa kasi sana hapa Tanzania ila kwa sasa wanaondoka kwa wingi na hizi ndio baadhi ya sababu wanazozitoa

..ishu ya viza, kupata permit imekuwa ni ishu mpaka inawabidi kila baada ya miezi mitatu watoke nje ya nchi ili wagongewe viza nyingine.

..mazingira magumu ya kufanya biashara, hii ni kuanzia mchakato wa usajili wa kampuni kwani sheria za nchi zinataka lazima awe na partner mzawa sasa hii wengi hawaitaki kwa sababu hawaoni mantiki ya kuingia ubia na mtu ambae humjui ikizingatia wao ni wageni kwenye hii nchi

..
Kutoruhusiwa kumiliki ardhi, Hii ni moja ya factor kubwa inayowafanya waghairi kuendelea kuishi Tanzania kwa sababu wengi wao wamekuja africa wakiwa na long term plans sasa wanashindwa kuipa nafasi Tanzania sababu hawawezi kumiliki ardhi .. sasa wanauliza watajicommit vip kuishi Tanzania kwa muda mrefu ikiwa hawana access ya ardhi badala yake wanachagua nchi km gambia, ghana na rwanda.

Mmmh, katafakari upya mr Mbowe
 
Back
Top Bottom