Bizari kiungo cha mboga chenye faida nyingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bizari kiungo cha mboga chenye faida nyingi

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Nov 9, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Inawezekana katika maisha yako hujawahi kula mboga iliyowekwa kiungo kinachoitwa bizari, kama umewahi, inawezekana pia hujawahi kujua faida zake mwilini.

  Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii ya mimea unaochimbwa kama mizizi, mfano wa tangawizi, lakini tangawizi yenyewe ina rangi ya njano na hujulikana pia kama ‘manjano’ kutokana na rangi yake.

  Kiungo hiki kinatumiwa sana katika Bara la Asia na hasa India na China. Kutokana na umuhimu wake kiafya, vyakula vingi hupikwa kwa kuchanganya na kiungo hiki ambacho sasa kimeenea dunia nzima, ikiwemo Tanzania.

  FAIDA ZA BIZARI KIAFYA
  Bizari hutumika na watu wengi kama kiungo cha mboga cha kuongeza ladha katika mchuzi na pengine kuweka rangi, lakini kuna faida nyingi unazozipata unapotumia kiungo hiki kila mara katika mapishi yako.

  Inaelezwa kuwa bizari ina virutubisho vyenye uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili, mara 8 zaidi ya Vitamin C na Vitamin E, ina uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu (cholesterol) na kuzuia mtu kuzeeka kabla ya wakati.
  [​IMG]Aidha, bizari huimarisha sehemu za magoti hivyo kukuepusha na matatizo ya miguu kuuma. Bizari pia hun’garisha ngozi na kuifanya kuwa yenye afya na huimarisha pia mfumo wa usagaji chakula (Digestion).

  SUALA LA UBORA NI MUHIMU
  Katika ulimwengu wa maendeleo ya sayansi na teknolijia tulionao sasa, bizari hutengenezwa viwandani na kuhifadhiwa kwa usafirishaji sehemu mbalimbali duniani na kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu. Katika hali kama hiyo, si ajabu kukuta bizari iliyoongezewa kemikali zingine za kuhifahdia chakula.

  Bizari ya aina hiyo, tayari inakosa faida zilizoelezwa hapo juu, hivyo ni suala muhimu kuangalia ubora wa bizari unayoitumia na mahali inapotoka. Katika nchi yetu, Mungu ametujaalia ardhi yenye rutuba ambapo kiungo kama hiki kinalimwa na kupatikana kwa wingi na kwa uhalisia wake.

  Katika suala la kujali ubora, pendelea zaidi kununua bizari kutoka sokoni ambayo imetengenezwa katika mazingira safi na salama na bila kuchanganywa na kitu kingine. Iwapo pia utanunua bizari iliyokwisha hifadhiwa, ni vyema ukasoma maelezo yake kuona kama haina vikorombwezo (additives) vingine.

  Ni ukweli ulio wazi kuwa ukitumia bizari iliyobora utapa faida nyingi kiafya, hivyo hakikisha katika upikaji wako wa kitoweo cha nyama, kama vile kuku, samaki, ngo’mbe unaweka bizari. Upikaji mzuri ni ule wa kuweka kiungo hicho mwisho baada ya mboga yako kuchemka na kuiva, kwani haitakiwi bizari kuchemka sana.

  turmericdryleaf.jpg


  Kwa ujumla hizi ndizo faida utakazozipata ukiifanya bizari kuwa sehemu ya viungo katika mlo wako wa kila siku:
  UTAIMARISHA KINGA YA MWILI WAKO

  UTAIMARISHA AFYA YA MACHO

  UTAIMARISHA SEHEMU ZA VIUNGIO VYA MWILI WAKO

  UTAIMARISHA UTENDAJI KAZI WA INI

  UTAIMARISHA CHEMBE HAI ZA MWILI

  UTAIMARISHA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA

  UTAIMARISHA MFUMO WA DAMU MWILINI

  UTASHUSHA KIWANGO CHA KOLESTRO MWILINI

  UTAIMARISHA MFUMO WA UZALISHAJI MBEGU ZA UZAZI

  UTAIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI MWILINI.
   
 2. i

  igwe sr. Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hizi bizari sikuiz sindo zinauzwa kwenye makopo mfano onga mchuzi mix, chicken masala na royco?nakumbuka enzi hzo,zilikuwa zinauzwa magengeni kwa kupimwa,unamwambia muuzaji nipimie ya kiasi kadhaa.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  barikiwa
   
 4. BMM

  BMM Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  asante sana mzizi kwa kunikumbusha, i previously used this, will resume.
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  mee too na hasa kwa ajili ya

  UTASHUSHA KIWANGO CHA KOLESTRO MWILINI

  UTAIMARISHA MFUMO WA UZALISHAJI MBEGU ZA UZAZI

  UTAIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI MWILINI.
   
 6. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Dah asante... Naenda kuitafuta, umenikumbusha mbali kweli.
   
 7. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi bizari ndio Curry Powder?
   
Loading...