Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
TUTAFAKARI PAMOJA: Maendeleo hayazuiwi na Vurugu tu!
Watawala wengi hudai "bila amani hakuna maendeleo". Kwa hiyo hutumia kila nguvu kuleta amani na utulivu ili shughuli za maendeleo zifanyike. Hata hivyo, ziko kweli hizi:
1. Amani na utulivu ni vitu 2 tofauti.
2. Polisi waweza kuleta utulivu si amani.
3. Matumizi ya nguvu ili kuleta utulivu, huondoa amani
4. Nafasi ya amani huchukuliwa na hofu na kuleta utulivu wa kulazimisha.
5. Madhara ya hofu ktk maendeleo yanalingana na madhara ya ghasia katika maendeleo.
6. Kwa hiyo, hofu na ghasia vina nguvu sawa. Uzoefu unaonyesha, watu wenye hofu ni hatari kuliko wenye ghasia.
7. Amani ya kweli ni pale maadui au wapinzani, wanapoishi pamoja bila kumalizana.
Yanga ikitoweka, Simba haina maana tena wala mashabiki. Ngedere na mbwa wanapocheza pamoja, upinzani wao haujaisha bali wanaamua kuikubali hali wasiyoweza kuibadili.
Weekend njema.