Bishop calls for redefinition of national ‘peace and tranquility’

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
Bishop calls for redefinition of national ‘peace and tranquility'
JIANG ALIPO
Daily News; Sunday,March 23, 2008 @00:03

RETIRING Archbishop of the Anglican Church of Tanzania Donald Mtetemela said in Dar es Salaam yesterday that persistent social problems threatens Tanzania's peace and stability.

"When we are praying this Easter we should ask ourselves if our nation and Tanzanian society has true peace and tranquility. There may be no killings in our country like in our neighbours, but should we say that we have peace just because there are no sounds of guns in the streets?" asked the archbishop.

He was giving his last Easter greeting as the archbishop of the church. The bishop wondered if peace could be maintained in a society where there is uneven distribution of wealth; where there is a yawning gap between the poor and the rich, where the HIV/AIDS pandemic is ravaging society, where there is corruption, where use of narcotics was growing.

The bishop said Christians should only give ‘Peace be Upon You' greeting when they are not the sources of pain, discrimination and wrongdoings in the society. He is expected to retire on May 25, this year. The newly elected Archbishop of the Anglican Church of Tanzania is Dr Valentino Mokiwa.
 
Ni ufisadi mtupu Pasaka
Basil Msongo
Daily News; Sunday,March 23, 2008 @00:02

*Maaskofu wasema unanyang'anya haki ya Watanzania
*Mwingine aitaka Serikali kutopoteza muda na tume

SIKUKUU ya Pasaka ya mwaka huu imeadhimishwa kwa maaskofu mbalimbali wakitoa ujumbe mkali wa kukemea ufisadi ulioibuka kwa kasi nchini.

Maaskofu wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo walianza kukemea ufisadi tangu Ijumaa iliyopita katika ibada ya Ijumaa Kuu ambayo huadhimishwa kukumbuka mateso ya Yesu Kristo msalabani.

Kukemea ufisadi kumeendelezwa tena katika salamu za Pasaka kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela.

Askofu Mkuu Mtetemela alisema ufisadi huo unawanyima maelfu ya Watanzania haki zao. Askofu Mtetemela amehoji kama ni halali kusema Tanzania kuna amani kama mfumo wa utawala umeingiliwa na rushwa na ufisadi uliokithiri.

Askofu huyo anayemaliza muda wake wa kuliongoza Kanisa la Anglikana Tanzania aliyasema hayo jana katika salamu za Pasaka kwa Watanzania na kusema kuwa, viongozi wakiwamo wa dini na serikali wajiulize kama kweli wao ni wajumbe wa amani kwa wanaowaongoza.

"Tutasemaje kuna amani kama vijana wetu wamenaswa katika janga la dawa za kulevya? Kama wachache wameshika njia za uchumi na wanakusanya mali na mamilioni wanazidi kudidimia katika umasikini uliokithiri na kusababisha pengo kati ya masikini na tajiri kuzidi kupanuka?" aliuliza.

Aliuliza Tanzania itasemaje ina amani kama wananchi mijini wanaishi kwa mashaka ya kuvamiwa na majambazi? Kama gharama za maisha zinazidi kupanda hivyo masikini kupoteza matumaini ya kuwa na maisha bora?

"Hizi ni salamu zangu za mwisho kwenu nikiwa Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania. Natumaini wengi wenu mlisikia kwamba tulifanya uchaguzi tarehe 28 Februari 2008 na kumpata Askofu Mkuu Mteule, Baba Askofu Dk. Valentino Mokiwa wa Dar es Salaam" alisema Askofu Mkuu Mtetemela.

Askofu Mokiwa atatawazwa rasmi Mei 25 mwaka huu, Mtetemela ataendelea kuwa Askofu wa Dayosisi ya Ruaha, Iringa.

Wakati huo huo Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini amesema jambo la msingi kwa watu wenye uwezo si kutoa fedha nyingi za sadaka Kanisani bali kuwasaidia kwanza majirani zao masikini na kutumia pia muda wao kuwatembelea wenye shida wakiwamo yatima na wajane.

Askofu Kilaini alisema kutoa sadaka kubwa Kanisani hakuna maana kwa Mungu kama huwasaidii masikini na wengine wenye matatizo na ndiyo maana amri ya upendo ni muhimu katika maisha ya kila siku.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, Ijumaa asubuhi wakati akijibu maswali ya watangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika kipindi cha Jambo Afrika Jambo Tanzania. "Hakuna mwenye upendo mkubwa kuliko wa yule anayejitoa kwa ajili ya rafiki zake," alisema Askofu Kilaini na kusisitiza kwamba, kama matajiri hawajitoi, ni vigumu kwao kuingia katika ufalme wa mbinguni.

"Hivyo jitoleeni, fanyeni mnachoweza kwa ajili ya wengine….leteni upendo katika familia, toeni ujumbe wa upendo, ujumbe wa amani" alisema. "Msalaba wako ni kupenda wengine, kutimiza wajibu wako……tukitaka kupata sisi wenyewe tutapoteza, tukijitoa tutapata".

Awali Askofu Kilaini, alisema, Wakristo wanapaswa kufufuka pamoja na Kristo na kuacha maovu. Alilieleza HabariLeo Jumapili kuwa, watu wengi wametawaliwa na mambo ya kidunia ikiwa ni pamoja na uchu wa kutafuta fedha hivyo kumsahau Mungu.

Kwa mujibu wa Askofu Kilaini, ipo mifano mingi ya watu hao wakiwamo mafisadi wanaotajwa katika tuhuma mbalimbali. Askofu Kilaini pia aliwataka walioiba fedha kwa kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) warudishe fedha hizo na riba.

Wakati hayo yakizungumzwa Dar es Salaam , Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, naye hakuwa nyuma kuungana na maaskofu wenzake katika ibada ya Ijumaa Kuu kukemea ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi. Kiongozi huyo wa Kanisa aliwataka waumini kuacha dhambi ya uchoyo ukiwamo wa fedha na raha za mwili kwa kuwa ina madhara makubwa kwa jamii.

Alitaja mifano ya dhambi ya uchoyo kuwa ni ubakaji wa watoto na mauaji ya albino kwa kuwa vyote hivyo vinasababishwa na tamaa ya utajiri.

Naye Askofu wa Kanisa la Menonite Tanzania Dayosisi ya Mashariki, Steven Mang'ana, alisema viongozi wanapaswa kukemea maovu waziwazi na wajenge mazingira ili wananchi wapate haki na waishi kwa amani.

Aliyasema hayo Alhamisi wiki hii wakati akizungumza na HabariLeo Jumapili kuelezea ujumbe wa Pasaka wa mwaka huu na akaeleza kukerwa na mlolongo wa kuundwa tume kuchunguza masuala mbalimbali kwa madai kuwa baadhi ya mambo yanayochunguzwa na tume hizo yangeweza kutolewa uamuzi bila kuundwa tume.

"Kama Taifa tumekosa mwelekeo, viongozi tuwe wawazi, tunashindwa kukemea maovu, hii ni ishara mbaya" alisema.

Kwa mujibu wa Askofu huyo, taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari kuhusu maovu mbalimbali ukiwamo ufisadi, rushwa, uonevu, umasikini, ujambazi, ukosefu wa ajira, wananchi kukosa huduma muhimu yakiwamo maji safi na salama vinasababisha wananchi wakate tamaa.

Alisema, viongozi wa Kanisa nao wana wajibu wa kukemea maovu na wahubiri amani na upendo miongoni mwa waumini wao na jamii kwa ujumla.
 
THERE SHOULD COME A TIME WHERE MAASKOFU WATAANDAMANA NDO MUONE THESE ISSUES ARE SERIOUS......! FROM RC,ANGLICAN,MENONNITE,TO LUTHERAN TUMESHUHUDIA WALEZI WA IMANI WAKIPAZA SAUTI ZAO AGAINST UFISADI....!
BADO HATUJAONA BAADHI YA VIONGOZI WA KIDINI NA KISIASA WAKIWA KINYUME NA HILI.....!
ASANTENI WAANGALIZI WETU KWA KULIONA HILI......."atamaniye kazi ya uaskofu........."
 
Back
Top Bottom