Bishara ya bia za jumla-ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bishara ya bia za jumla-ushauri

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mijicho, Mar 4, 2010.

 1. M

  Mijicho Senior Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Heshima mbele ,

  Katika kutafuta ni jinsi gani naweza kujitoa katika kuajiriwa,nimekuwa nikujiuliza ni biashara gani nzuri inaweza kunitoa ,kwa maana ya faida ya haraka,bidhaa kuzunguka haraka,na faida ya haraka,wazo la biashara ya bia za jumla likanijia,naomba yeyote ambaye amewahi kufanya au anajua inafanyika vipi,kuanzia mtaji,uuzaji,usambazaji ,watu wa kuajiri,faida,hasara zake,changamoto na kadhalika.Naombeni mchango wenu
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Si mtaalamu lakini kwa munekano wa juu juu inahitaji mtaji mkubwa kiasi na usafiri mkubwa (lori) na wakati (pickup na canter). Pia unahitaji ghala ama eneo kubwa la wazi jirani na ofisi; na muhimu ofisi iwe sehemu ambayo inafikika kwa urahisi na vizuri ikiwa ni jirani na barabara kuu; hasa wakati wa kupokea mzigo ni muhimu
   
 3. M

  Mijicho Senior Member

  #3
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  thanks for that
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Karibu; ila ni biashara inayolipa sana ukiisimamia kwa karibu na kwa umakini unataka kuifanyia wapi?
   
 5. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwasasa hamna biashara ya kurudisha mtaji haraka haraka kama unavyofikiri, usije ukawehuka utakapoona biashara inalala.
  Biashara inahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana, hasa kwenye kuwapata wateja na kujenga mahusiano nao!
  Kwa uelewa wangu, wateja wengi wa bia za jumla huwa wanahitaji na vitu vingine kama sigara, viroba etc bidhaa flani zinazoendana na vitu vinavyopatikana Bar!

  na wauzaji wengi wa bia za jumla huwa wanawapelekea wateja wao bia mpaka mlangoni (kwa wateja wao wakubwa) na huwa wanamuhusiano mpaka ya kukopeshana. Sasa usitarajie kuingia kwenye biashara leo na kesho ukarudisha mtaji na faida.
  Lazma uwe mvumilivu.

  Ni hayo tu!
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Angalia kama wewe ni mlevi vinginevyo utakula mtaji!
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  @ Kabengwe; ndiyo maana nimemweleza kuwa anahitaji aina 2 za vyombo vya usafiri; Lori kubwa na lori dogo ama pickup! kwa ajili ya usambazaji.
   
 8. M

  Mijicho Senior Member

  #8
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  again,thanks kwa ushauri wakuu,ntazingatia .Ingawa ningependa kujua pia ni kiasi gani cha mtaji nnaweza kuanza nacho esp kwa kununua bidhaa,assume sehem ya biashara ipo
   
 9. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Depending on the need hii siyo muhimu sana. Inategemea zaidi market unayoihudumia. Dada yangu yeye ana mkokoteni na anasave vizuri tu. Mahali pengine hasa Sinza wateja wanakufuata wenyewe.
   
 10. B

  Bobby JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,798
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 180
  I used to have a friend akifanya hiyo biashara. Always alikuwa anadai ilikuwa hailipi kwani alikuwa anaweka pesa nyingi (capital) wakati faida ilikuwa ni kiduchu sana. Kwa madai yake wanaomake ni dealers ambao wao hupewa mzigo on credit wanauza then wakabidhi pesa kwa makampuni.Sina nia ya kukukatisha tamaa, nia yangu ni kukutaka ufanye upembuzi yakinifu b4 hajatie pesa yako huko then ukajuta.
   
 11. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,667
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Unaweza pia kuomba TBL uwe Agent wao hii kidogo inakupunguzia mzigo kwenye capital yako. lakini wana vigezo vyao na unaweza kupata ofisini kwao.
   
 12. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  this sounds good!
   
 13. senator

  senator JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kwa sasa bei bei ya crate kwa jumla zinarange kwenye 20,-27000/- per crate..Kwa kuanzia kama ni bia za jumla na sehemu ni nzuri ukiweka mtaji wa crate 200 si haba as time goes on unaongeza..ila kila penye biashara kawaida mwanzo wake huwa mgumu.Ni kweli kwenye bia kuna faida especial wenye mabar mana wengi wanajiwekea faida mpaka ya 350tsh kwa chupa moja which mean in a crate he/she generates 7000tsh.Ila kwa wauzaji wa Jumla faida ni ndogo unless uwe unawezakuuza big Volume per day.Ni hayo tu mjasiriamali wangu
   
 14. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,581
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  ......Hii biashara inalipa kama umepata sehemu ambayo kuna bar nyingi au grocery maana hao ndio watakuwa wateja wako.
  Na inapendeza zaidi kama ukiamua kuchangaya kuuza kwa jumla beer, soda na maji kwa pamoja. Mwanzoni itakupa shida kwa kuwa mara nyingi mwanzo ni mgumu.Hivyo mwanzoni usitegemee kupata faida ya haraka haraka.

  .......Kuhusu wafanyakazi unatakiwa kutafuta vijana 2 ili wakusaidie kwenda kusambaza kwa wateja wako, sasa hii inategemea kuna baadhi ya wateja watakuja kuchukua wenyewe ila kuna wengine watatoa order na wewe itabidi upeleke.......hivyo itabidi uwape ajira angalau vijana 2 au 1 kwa mwanzoni kama biashara imechanganya unaweza kuajiri vijana zaidi.

  .......Mtaji inategemea mfuko wako ila angalau uwe na kiasi cha milioni 20.Kwa maelezo zaidi ya mtaji nenda TBL kitengo cha masoko pale watakuelezea vizuri maana unaweza hata kuwa agent wao.
   
 15. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,712
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  nakushauri uanze taratibu
  kama nyumbani kwako kuna geti, basi kreti 200 utazifungia ndani ya geti lako bila matatizo yeyote.
  ushauri: wakati unataka kuanza biashara usitegemee faida mpaka mwaka mmoja upite, kipindi chako cha mwanzo unatakiwa u-focus kwenye kuongeza wateja na kupanua biashara na kama unafanya kazi basi usihache kwanza.

  watu wengi wanaofanya hii biashara wana baa zao wenyewe
   
 16. M

  Mijicho Senior Member

  #16
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  niwashukuru tena kwa mara ingine kwa kuchangia ,nimepata uelewa kiasi fulani.Kwa sasa hata nikiamua kuanza ntaweza kujikongoja.Ingawa nashawishika kwenda TBL nione jinsi gani naweza kuwa dealer wao.Si vibaya mtu akatupa breakdown ya biashara hii ukiwa kama dealer wa TBL.Nia haswa ni kutengeneza faida haraka iwapo mtu unaamuwa kuwekeza kwenye biashara hii.Na pengine kama kuna anayejua vigezo vya kuwa dealer waTBL si vibaya akaviweka kabla sijaenda mwenyewe TBL.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...