Birthday party: Je, Ni Mzazi au Mpenzi?

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Wana JF, Habari za leo?

Kwa muda sasa nimekuwa nikitafakari namna ambavyo kwa siku za hivi karibuni, watu wamekuwa wakiandaa hizi birth day parties ...
Kwa kifupi, wimbi kubwa limezuka la sherehe hizi ndogo kuaandaliwa na mpenzi/Mke/Mume na mara nyingi wazazi huwa hawashirikishwi na pengine hata kualikwa, ingawaje ni ukweli usiopingika kuwa wao ndiyo haswa waliotuleta duniani na ndiyo sababu kuu ya sisi kufanya birth day party.

Swali langu ni kuwa, ni right attitude kufanya birthday bila kuwaalika wazazi? Ni nani hasa anayepaswa kuandaa birthday; mzazi au mpenzi au unajiandalia mwenyewe? Na kama ni mpenzi ndiyo mwenye hilo jukumu, wazazi wana nafasi gani kwenye hiyo sherehe??

Wenu,

HP
 
Birthday ni kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa mtoto siku hizi naona hata wakubwa nao wanalilia kufanyiwa birthday...mara nyingi sana inatakiwa iwe ni family gatherings, hapo ni wakati wa kucatch up with family members, and enjoy the special feeling of being surrounded na family yako...na ukiweza kuwalika marafiki zako pia sio mbaya.

Kwa hio sio tabia nzuri kabisa kufanya birthday part, bila kuwepo wazazi wako au family yako.

Birhtday za kuandaliwa na wapenzi its a big joke, na huyo mwanaume hausiki na kumbu kumbu za kuzaliwa kwako inakuwa kama unajidhalilisha tu...kama kisha kuoa hapa sawa, ana hesabika kisha kuwa a member of your family.

Mpenzi wako akufanyie sherehe, siku za kuoana tu.
 
Wasubiri wenye hiyo fani mwaya,mie hua namshukuru mungu kwa kutoa sadaka ya shukran na kurudi hm kupumzika zangu basi,mchuchu wangu naye wala hanaga mizuka ya kuandaa party hasa hasa huwa analeta kadi na kunipongeza basi tunaendelea na mambo mengine!!
 
Kwa upande wangu huwa wazazi wangu wote wawili wanashiriki.... Tena baba yangu hutenga muda kabisa kwa ajili ya kuniombea dua. Huwa ni mwepesi wa kuikumbuka siku yangu kwani zinatofautiana siku 2 na yake. Mama yangu ndio usiseme,kama nipo mbali anapata tabu sana kwani huwa anapenda anione siku hiyo.
 
Siku kama hiyo ni furaha sana kwa mzazi wako kuwepo kwani yeye ndio MC wa mambo yote,mie ikifika wakati wa uhai wa Mama nilazima niwe home tunapika chakula dua kidogo na yalobakia ni kicheko hunikumbusha nilivyokua mdogo nilikua nafanyaje yani raha kwakwenda mbele,lakini sikuizi sioni tena raha ikifika sikuyangu yakuzaliwa inakua majonzi kwani namkumbuka sana Mama,Mwenyezi mungu ampe kauli thabit yaarab....
 
Back
Top Bottom