Binti yao kaniacha lakini ndugu zake bado wanatamani kuwasiliana na mimi

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
8,953
16,891
Wakuu hii imekaaje,

Binti amenipotezea lakini kwa vile mahusiano yetu yalikua open kwa watu wote imetokea ndugu zake na binti wanapenda sana kuwasiliana na mimi.
Yaani ikipita hata week sijawatafuta basi watalalamika hao.

Nifanyaje wakuu?
 
Kilichokuunganisha nao ni mwanao ila kakuacha bhasi muunganiko na wao unajifia wenyewe, wapotezee kabisa au usubirie huyo ex wako aseme unajipendekeza kwa ndugu zake!
 
Wakuu hii imekaaje,
Binti amenipotezea lakini kwa vile mahusiano yetu yalikua open kwa watu wote imetokea ndugu zake na binti wanapenda sana kuwasiliana na mimi.
Yaani ikipita hata week sijawatafuta basi watalalamika hao.
nifanyaje wakuu?
utakua unawakatia mpunga kisela wewe,endelea kusambaza upendo usipo pendeka
 
Mawasiliano ya nn sasa, achana nao ikibidi usiwapigie wala kupokea simu zao, mind your business
 
Umenikumbusha mkuu

kuna siku nilikwendaga kwa demu mmoja nikaa kwao kama miezi miwili hivi. kwa kuwa yule demu nlimpenda sana ila yeye alinichana ukweli hawezi kuwa na mimi. nilipoona naitwa itwa kaka kaka ikabidi nibadilishe gia hewani. nikatunga umbea nimeitwa nyumbani niende.

siku naondoka nikapigia voda nikawaambia funga line zangu. nikasepa siku hiyo. mpaka leo nafikiria nilivyopewa hisani yao na baba na mama na ndugu zake. ila niliwapigia simu siku moja kuwaeleza nilifika salama ila walinigombeza sana sikufanya sawa. ila ndo ivyo nilianywa mjinga.

cha kukushauri baddili line wala hutasumbuka tena na itakuwa ndo njia rahisi ya kumsahau na kuwapotezea hao ndugu zake. usiwaendekeze utaumia bure bila sababu
 
Mkuu umechana na mpenzi wako sio ndugu zake, hilo la kawaida tena kama kuna Dada MTU ndo huwa wanapenda kuwasiliana na Ex Shem, usiwaze
 
Back
Top Bottom