Binti yangu Fransiska, Nimesoma kwa makini ujumbe wako

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,836
Dear Aunt, Naomba msaada wako nifanye nini? Mimi ni mke wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume wangu ana angalia TV.

Sikufika mbali gari ghafla likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu anisaidie. Nilipofika nyumbani sikuamini macho yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa jirani yetu.

Nilimkabiri mume wangu na kwa bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao una mwaka sasa, lakini cha ajabu amesema atalazimika kumuacha huyo binti pole pole ili asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado mdogo.

Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba ushauri Mzee wangu Fransiska wa Mwenge

JIBU

Binti yangu Fransiska, Nimesoma kwa makini ujumbe wako, kitu ambacho nimekiona mara moja ni hili tatizo la gari kuzimika ghafla. Kwanini uendeshe gari na baada ya muda mfupi lizime? Hapa kuna matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza kuwa chanzo.

Inawezekana plag mbovu au uchafu umeingia kwenye mrija unaopeleka mafuta kwenye injini. Au pengine ni tatizo la umeme, au fuel pump, ulicheki kama petroli ipo? Ikiwezekana waone mafundi warekebishe hivyo nilivyovitaja.

Nategemea ushauri huo utakusaidia mwanangu
 
hiyo ndo shida ya kuendesha gari bovu...mwishowe unajikuta kwenye matatizo Fransiska!
 
Mzee hajakosea coz katumia Tafsida tu!kama nimuelewa utamsoma tu Lol!
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom