Binti wa miaka 25 kufuatana na mama yake kila mahali ni sahihi?

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Kuna msemo usemao, mama ni mama na mtoto hakui kwa mama yake. Ni sawa ila tuje kwenye hoja.

Kuna mabinti wakubwa hadi miaka 30 ila wanapenda kufuatana sana na mama zao hasa kwenye misherehe. Wanasahau kuwa mama anahitaji kutoka na mume wake na binti atoke na mume ama mchumba wake.

Mbona vijana hawaongozani na baba zao? Yaani mke anamuaga kabisa mume wake kila weekend anamsindikiza mama sehemu fulani. Hasa mabinti ambao ni wa pekee kwa wazazi hao.

Tuelezane waungwana, je huu ni ungwana? At least miaka mingapi kumsindikiza mama kila mahali? Nani anafanya makosa kati ya binti anayejipeleka au mama anayempokea?
 
Si bora huyo anamsindikiza mamake..je ingekua anasindikiza mashoga kila mahali ingekuwaje
binadamu hawakosi la kusema, angemsindikiza baba yake ingesemwa anatembea nae, akimsindikiza mumewe itasemekana ana wivu hampi nafasi sasa mama pia ishaulizwa kama ni sawa.
 
Hakuna kama mama,tena mie Mama yangu alipo kua hai hakuna sehemu amabapo siendi nae nimarafiki wazuri sanaaaa
hata nikienda holiday mr yuko busy na masomo au kazi namchukua,na mr ana kua na amani nnapokua na Mama yangu
au mama yake kuliko nikiwa peke yangu na watoto yani lazima mmoja wapo awepo,na harusini hua si mtu wa harusini lakini simuachi driver akampeleka,mie nakua driver wake namshusha halafu bro au hubby anamfata au kama nimchana namfata
mwenyewe ,duu umenitonesha kidonda ...hakuna ubaya wowote tena hakuna mama anaemtakia mwanawe mabaya
akimuona anafanya makosa atamwelekeza kua sio hivyo mwanangu mume hajibiwi hivyo,au apana mda huu baki na mumeo
au hiki usifanye hatotaka mwanawe aharibikiwe,yani kua proud mkeo kua karibu na mazazi wake na wako...
 
Kwangu miye ni sawa, lkn isiwe too much. Maana kama umeshaolewa huo muda wa kuwa unaambatana na mama yako kila mara unaupata wapi. Au labda kama huyo mama yake ni mjane na mpweke.
 
hili sijambo dogo kama linavyooneka! Mara nyingi linabomoa familia kwa kuwa mwanaume mwenye busara atakaa kimya hata kuukiza lakini linaweza kusababisha mwanaume kutafuta faragha kwingine
 
Ao ndio wasiri wa kweli ambao upelekea Mama au Mwana kumegwa uzuri kabisa bila siri kuvuja Mama usema aenda kwa Mwana, Mwana naye uaga enda kwa Mama.
 
Hakuna kama mama,tena mie Mama yangu alipo kua hai hakuna sehemu amabapo siendi nae nimarafiki wazuri sanaaaa
hata nikienda holiday mr yuko busy na masomo au kazi namchukua,na mr ana kua na amani nnapokua na Mama yangu
au mama yake kuliko nikiwa peke yangu na watoto yani lazima mmoja wapo awepo,na harusini hua si mtu wa harusini lakini simuachi driver akampeleka,mie nakua driver wake namshusha halafu bro au hubby anamfata au kama nimchana namfata
mwenyewe ,duu umenitonesha kidonda ...hakuna ubaya wowote tena hakuna mama anaemtakia mwanawe mabaya
akimuona anafanya makosa atamwelekeza kua sio hivyo mwanangu mume hajibiwi hivyo,au apana mda huu baki na mumeo
au hiki usifanye hatotaka mwanawe aharibikiwe,yani kua proud mkeo kua karibu na mazazi wake na wako...
Kwa upande wangu siafiki kuwa mke wangu atakuwa katika mazingira yasiyo hatarishi (kimchepuko) akiwa na mama yake au watoto wake WA KIKE. Naamini atakuwa katika mikono salama hasa akiwa na mtoto wa kiume (maana naye ana wivu na mamake biologically) au mama yangu mzazi (maana ni mahasimu kwani mama yangu ana wivu biologically na mke wangu) hivyo kuna kuogopana. Kufuatana fuatana na mtoto wako wa kike hasa kwa akina Kitwanga, humomonyoa maadili kwa watoto wa kike.
 
Kuna msemo usemao, mama ni mama na mtoto hakui kwa mama yake. Ni sawa ila tuje kwenye hoja.

Kuna mabinti wakubwa hadi miaka 30 ila wanapenda kufuatana sana na mama zao hasa kwenye misherehe. Wanasahau kuwa mama anahitaji kutoka na mume wake na binti atoke na mume ama mchumba wake.

Mbona vijana hawaongozani na baba zao? Yaani mke anamuaga kabisa mume wake kila weekend anamsindikiza mama sehemu fulani. Hasa mabinti ambao ni wa pekee kwa wazazi hao.

Tuelezane waungwana, je huu ni ungwana? At least miaka mingapi kumsindikiza mama kila mahali? Nani anafanya makosa kati ya binti anayejipeleka au mama anayempokea?
Kwa hiyo hata kitchen parties aende na mumewe?.
 
Back
Top Bottom