Binti wa miaka 14 aozeshwa kwa mahari ya Ng’ombe wawili,Mbuzi na Pombe

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Mama mmoja mkazi wa kijiji cha Ilkurot wilayani Arumeru mkoani Arusha anatuhumiwa kumuozesha binti yake mwenye umri wa miaka kumi na nne na kupokea mahari ya ng’ombe wawili,mbuzi mmoja na debe mbili za pombe.

Baada ya kupata taarifa hizo ambazo dhahiri zinakiuka haki za mtoto ikiwemo ile ya kupata elimu ,ITV ikafunga safari hadi kijijini hapo ambapo inakutana na baadhi ya viongozi wa eneo hilo,ambao wanakiri kulifahamu sakata hilo.

Akizungumzia sakata hilo la binti yake kuozeshwa baba mzazi wa mtoto huyo Melau Loosho anasema mwanae ameozeshwa kwa siri akiwa wilayani Kiteto kwenye majukumu ya kutafuta maisha.

Bi.Shimu Loosho ndiye mama mzazi wa binti huyo ambaye alikutwa akiwa naye nyumbani kwa madai kuwa muoaji amesafiri ,anasema binafsi amelazimika kumuozesha mtoto wake baada ya mtoto mwenyewe kukubaliana na mumewe hatua ambayo wanaharakati wa utetezi wa haki za binadamu wilayani humo wanasema ni ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto unaopaswa kudhibitiwa mapema kutokana na kukithiri kwa ndoa za utotoni katika maeneo hayo ya wafugaji

Habari za awali zinaeleza kuwa binti aliyeozeshwa alikua mwanafunzi kabla ya kukatishwa masomo miaka miwili iliyopita.

ITV inaendelea kufuatilia sakata hili ikiwa ni pamoja na kuutafuta uongozi wa wilaya ya Arumeru ili kujua msimamo wake katika suala hili.
 
Back
Top Bottom