Binti wa miaka 14 anafaa kuwa mzazi?

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,906
2,955
Mniwie radhi kwa kuleta hoja hii japo wazee wetu yaani viongozi wa dini wako katika mjadala mkali juu ya umri sahihi wa binti kuweza kuolewa na kuwa mzazi, kisheria kadiri ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 binti anaruhusiwa kisheria kuolewa afikishapo miaka 14.

Hii inamaanisha kwamba mabinti wengi wanatakiwa mara tu baada ya kuhitimu elimu ya darasa la saba wanaweza kuolewa kwa mujibu wa sheria. Swali lililopeleka mimi kuleta haya mbele ya wana JF ni kwamba tunaposema huyu ni mtoto tuna maanisha nini hasa? Pitia katika linki hii kwa maoni zaidi ya viongozi wetu

Source: IPP Media

Nawasilisha
 
Bubu,
Hii article nilisoma jana, i felt so ashamed to those who used religion as a shodow for this case. 14 years old hajui hata what is right and what is wrong in this generation.

Apart from that, wanaposema kwamba kuzuia watoto wasio olewe at 14years old kunapush zinaa sio kweli, i need a vivid factors. Tanzania ya leo wanaozini namba moja ni wanandoa, hawa viongozi wa dini wanaoupaka Uisilam matope they need to stop. Tunaishi katika society ambayo inabidi tuongeze elimu kwa wanawake, tuongeze heshima kwa mwanamke, na sio kuwakandamiza.

Kidini ya kiislam, sheria inasema oweni na oleweni pindi mnapofika umri. Haikusema umri gani, lakini imezungumzia kuhusu kutokuwaoza wanawake bikira pasipo maamuzi yao, imezungumzia kuhusu sheria za muoaji na n.k. Sasa hawa mashekh ubwabwa ambao kazi yao ni full time BAKWATA na kupingana na reality need to stop.

Ndoa ni muungano mkubwa sana, unatakiwa ufatishe all the laws and regulation. sasa niambie ni mtoto gani wa miaka 14 anaweza kumtake care mwanaume wa leo? Au ndio wanataka hii kujisawazishia matakwa yao?

I believe 18 is resonable, but 14 is total "no"
 
Haya ni maoni yangu.
Mfano mimi Bibi yangu aliolewa akiwa na miaka 12 flat.(kwa kumuuliza mwenyewe)
Ninachoelewa mimi,ndoa kwa sasa kwa miaka Hiyo hapo haiwezekani kwani kuna mambo kama hayo ya masomo na mengineyo amboyao yamekuja na technologia.Zamani mambo hayo yote haya kuwepo,mtoto wa kike akivunja ungo tu (akianza kupata hedhi/damu ya mwezi)anakua ameshakua na ndoa ili wezekana baada ya kutoka unyago tu,haikujarisha anaumri gani lkn kwa maeelezo ya wengi walio olewa kwa umri huo ni kuanzania miaka 12 mpaka 16.
Siku hizi mambo yamekua tofauti zaidi watu tunaenda zaidi na tamaduni za magharibi na mabadiliko ya hari ya hewa(Not sure)watoto wanachelewa kubarehe na sheria za haki ya mtoto kutoka huko kwa walioendelea haziruhusu ndoa kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18.
Kuhusu nini vitabu vya dini vina sema nashindwa kuzungumzia sana kwani kama vingine vinasema "oeni au oleweni umri unapofika"basi nadhani kuna zaidi ya umri hapo,kwani imani yangu neno lolote divine basi huja na maana kubwa unahitaji elimu zaidi ya kujua lipi dhambi na lipi sawa.
sasa baada ya
 
Nadhani sheria hailazimishi kuwa akifika miaka 14 basi lazima aolewe. Kwa maoni yangu mimi ni kwamba miaka 14 kwa msichana anakuwa amekomaa kimaumbile (yaani amevunja ungo) na anaweza kupata mimba na akazaa. Tatizo linakuja katika nyanja nyingi:

1. Umri huo bint anakuwa hajakomaa kisawasawa (biological maturity) na anweza kupata matatizo wakati wa kujifungua.
2. Hali ngumu ya uchumi wa nchi na familia nyingi kunapelekea mtoto kuzaliwa bila ya maandalizi ya kiumbe hicho kwani kwa uchumi wa Bongo mtoto wa miaka 14 bado hajamaliza hata darasa la 12 ambalo linaweza kumpanua stadi za maisha.
3.Inaweza kuchukuliwa na wazazi wenye mawazo mafupi na tamaa za dunia kumuozesha binti badala ya kumuendeleza.
4. Binti huyo wa miaka 12 akizaaa anapoteza stahili nyingi za kuweza kujiendeleza kimaisha yake mwenyewe na pia mtoto wake.
 
Jafar nakubaliana na wewe 100%. fatwa za dini ziko deep sana, and it need someone who have high knowladge in decision making. Sababu kubwa ya ndoa ni kujenga familia kati ya mke na mume. Sasa kama mmoja wenu hawezi kufanya critical thinking at all, matokeo yake ndio talaka na development za watoto wa mitaani.

Wanaaume wengi wa Kitanzania wanaowa kutokana na matamanio ya kimwili, kitu ambacho ni dhana potofu na unyanyasaji wa wanawake. I believe ya kwamba, karne hizi tunazoishi zinatofauti sana na karne za zamani. Invasion of western culture, economics intergration, and many other factors has hinder wanawake kuolewa at 14yrs old.

Mtoto wa miaka kumi na nne bado anaitaji haki zake za utoto. Mama watoto wangu huko pwani ameajiri house gal wa miaka kumi na nne, matokeo yake ni house gal anapoteza muda mwingi kucheza rede badala ya kupika, aliponiuliza mimi nikamwambia please make sure huyo mtoto anapata haki zake za msingi kama mtoto mwingine.

Watoto wadogo wanafanana, sidhani kama mtoto wa miaka kumi na nne anaweza kuimili mikiki ya nyumba. Nyumba ina procidure zake, kuanzia kitandani mpaka kufuata majukumu. Kama kuolewa kwake ni specific kwa kuzaa, then anaqualify kubeba mimba lakini kuzaa still ni kamari. I hope TAMWA will over rule hii 14yrs law, sababu ni ukandamizaji wa kijinsia
 
Ukiangalia wanaozungumza wote ni wakina baba. Sasa naelewa kwa nini madhehebu mengine yameamua kuwapa nafasi za uongozi wakina mama. Mpka lini wakina baba wataendelea kuwatolea maamuzi kuhusu miili yao? Nashukuru wote waliochangia humu ambamo wengine ni wakina baba wameonyesha msimamo tofauti. Kama walivyosema, MTOTO wa miaka 14 hata kama amebalehe, hajakomaa kimawazo na kimwili. Matatizo kama fistula yanawakumba wengi ambao wanaozaa wakiwa na umri mdogo, ukichangiwa na kuwa wengi wanaofanya hivyo kwa wakati huu ni wale wanaotoka katika familia zisizo na uwezo. Utetezi kuwa kufanya hivyo ni kama ule ambapo mwanamke akibakwa ni makosa yake kwa sababu alimtamanisha mwanaume! Ni mawazo kama haya ambayo watu wanatumia kupinga matumizi ya kondomu ati kwa sababu itachangia kuporomoka kwa maadili ya jamii. Ni mawazo kama haya ndiyo yanapelekea ukitembelea sehemu zetu za starehe utakuta watu wazima wakiwatendea matendo ya aibu pamoja na kutumia lugha za ajabu kwa wasichana wenye umri mdogo wanaohudumia humo! Asante sana Bubu kwa kulileta hapa na Jafar na Mtanganyika kwa kuonyesha kuwa si wanaume wote ni chauvinists!
 
Asante sana Fundi Mchundo kwa mawazo yako mapya. Na kama unataka kuhakikisha hilo kama kweli wanachozungumza hao hao hawapendi watoto wao waolewe katika umri huo wanaopendekeza wao. Binadamu sisi tupo pabaya sana yaani unasubiri kitoto cha mwenzio kivunje ungo na ukishasikia kiko hedhi tu unameza mate kwamba sasa tayari ni halali yangu kuoa. Hata kuku hafanyi hivi, hata ng'ombe hafanyi hivi, utashi tuliopewa na Mwenyezi Mungu umebadilika. Kama hakuna haja ya kufanya mabadiliko naomba niulize swali, hapo kale binadamu waliweza kuishi miaka hata mia. Je kwanini leo hatuwezi kufikia umri huo. Jibu litakuwa ni mabadiliko ya maumbile, sasa je kwanini hata sisi tusifanye mabadiliko hayo. Hadi mwanao afe kwa matatizo hayo ndipo kimya kimya ulaani uamuzi wako. Nyie viongozi wa dini hata nyie mnakuwa makatili namna hiyo? hivi vitoto vitakimbilia wapi?????????????????????????????????????????
 
Mazingira ya sasa hivi hayaruhusu kabisa mtoto wa miaka 14 kuolewa. Zamani jamii ilikua na mfumo wa kusimamia maisha ya family members, mwali anakua chini ya mama mkwe mpaka anapevuka, kwa hiyo hata kazi nzito za nyumbani anakua anasaidiwa na ndugu.
 
Bubu,
Hii article nilisoma jana, i felt so ashamed to those who used religion as a shodow for this case. 14 years old hajui hata what is right and what is wrong in this generation.

Apart from that, wanaposema kwamba kuzuia watoto wasio olewe at 14years old kunapush zinaa sio kweli, i need a vivid factors. Tanzania ya leo wanaozini namba moja ni wanandoa, hawa viongozi wa dini wanaoupaka Uisilam matope they need to stop. Tunaishi katika society ambayo inabidi tuongeze elimu kwa wanawake, tuongeze heshima kwa mwanamke, na sio kuwakandamiza.

Kidini ya kiislam, sheria inasema oweni na oleweni pindi mnapofika umri. Haikusema umri gani, lakini imezungumzia kuhusu kutokuwaoza wanawake bikira pasipo maamuzi yao, imezungumzia kuhusu sheria za muoaji na n.k. Sasa hawa mashekh ubwabwa ambao kazi yao ni full time BAKWATA na kupingana na reality need to stop.

Ndoa ni muungano mkubwa sana, unatakiwa ufatishe all the laws and regulation. sasa niambie ni mtoto gani wa miaka 14 anaweza kumtake care mwanaume wa leo? Au ndio wanataka hii kujisawazishia matakwa yao?

I believe 18 is resonable, but 14 is total "no"

Nitaka nikusaidie hapo nilipo RED.

Hakika Uislam umeweka bayana kuwa mwanamke ataolewa pindi atakapotimiza umri wa kuweza kuhimili mikiki ya ndoa. haukuweka Umri maalum wa kuolewa ila lazima mwanamke awe amesha balekhe.

Vile vile kwa muowaji yaani mwanaume. Rasul amesema " Enyi makundi ya mabarubaru( Shabbab au vijana) na mwenye uwezo wa kuhimili harakati za ndoa basi na aoe na yule atakayeshindwa basi ajizuie kwa kufunga" Hapo utaona hata mwanaume haukutajwa umri.

Vile vile Uislam unatuamrisha kutii mamlaka zinazotutawala katika mambo yasiyo muudhi Muumba.

Sasa kijumla ni sheria za nchi zinazoweza kutawala kwa kuweka bayana kabisa NI UMRI GANI MTU AWEZE KUOA AU KUOLEWA.

Nachelea kusema ndoa katika Tarbia za uislam ni Ibada na ni sunna iliyokokotezwa sana kwetu. Na imewekwa kama makubaliano ya kihiyari maalum ya kuunga udugu baina ya pande mbili kwa kufata kaanuni za Muumba na Sunna za Rasul. Hapa kuna kipengele muhimu sana cha LAZIMA MUOAJI NA MUOLEWAJI LAZIMA WOTE WAKUBALI BILA KUPATA SHINIKIZO LA MTU YOYOTE.
 
Back
Top Bottom