Binti wa Miaka 14 Amuua Mama Yake Aliyemkataa Mpenzi Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti wa Miaka 14 Amuua Mama Yake Aliyemkataa Mpenzi Wake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Jun 22, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Tylar Witt Monday, June 22, 2009 4:23 AM
  Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 14 wa nchini Marekani anashikiliwa na polisi baada ya kumuua mama yake ambaye alikuwa akiupinga uhusiano wake na mvulana mwenye umri wa miaka 19. Tylar Witt mwenye umri wa miaka 14 na mpenzi wake Steven Colver, 19, wanashikiliwa na polisi baada ya kushirikiana kumuua mama huyo ambaye alikuwa akiupinga uhusiano wao.

  Taylar inasemekana alikuwa anapenda kutembea kimapenzi na wanaume wenye umri mkubwa akiwadanganya kuwa umri wake ni miaka 16.

  Wawili hao inasemekana walikimbia nje ya mji baada ya kumuua mama huyo kwa kumshambulia sana na kumuachia majeraha makubwa.

  Mwili wa mama huyo aliyejulikana kwa jina la Joanne Witt mwenye umri wa miaka 47 ulikutwa nyumbani kwake Sacramento, California baada ya wafanyakazi wenzake kuripoti polisi baada ya kutoonekana kazini kwa siku kadhaa.

  Mkuu wa polisi wa eneo hilo Jim Byers alisema kwamba mama huyo alifariki baada ya kupata majeraha makubwa lakini alikataa kuelezea kuelezea zaidi juu ya kifo hicho ingawa tetesi za majirani zinasema mama huyo alifariki baada ya kuchomwa chomwa na kisu.

  Binti huyo na mpenzi wake walikamatwa wakiwa umbali wa maili 100 kutoka kwenye nyumba hiyo wakiwa wamechoka kutokana na maisha ya kuwakimbia polisi kwa siku kadhaa.

  Majirani na nyumba hiyo walisema kwamba hiyo si mara ya kwanza polisi kuitwa kwenye nyumba hiyo.

  Polisi walisema kwamba binti huyo alishawahi kukamatwa na polisi mwezi uliopita baada ya kumshambulia mama yake.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2302998&&Cat=2
   
 2. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pole sana mama. Mtoto amevuna alichopanda na akafurahie hilo penzi lupango!
   
Loading...