Binti wa Miaka 10 Ajifungua Mtoto Hispania

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
52,051
2,000
Binti wa Miaka 10 Ajifungua Mtoto Hispania
5093778.jpg

Wednesday, November 03, 2010 1:33 AM
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 wa nchini Hipsania amejifungua mtoto baada ya kufanya mapenzi na mtoto mwenzake.Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 amejifungua mtoto katika mji mmoja wa kusini mwa Hispania na mamlaka husika zinachunguza tukio hilo ili kuamua kama wamnyang'anye mtoto huyo au mwachie amlee.

Msichana huyo mwenye umri mdogo alijifungua mtoto mwenye uzito wa kilo 2.8 wiki iliyopita kwenye mji wa Jerez de la Frontera, alisema Bi. Micaela Navarro, ambaye ni wa waziri wa masuala ya jamii wa kitongoji cha Andalusia.

Bi. Navaro aliwaambia waandishi wa habari kuwa baba wa mtoto aliyezaliwa naye ni mtoto mwenye umri mdogo ambaye jina lake limewekwa kapuni.

Wizara ya Afya ilisema kuwa msichana huyo na mtoto wake wote wana afya njema.

Magazeti ya Hispania yalinukuliwa yakisema kuwa msichana huyo alikuwa ni raia wa Romania.

Gazeti la Diario de Jerez liliwanukuu madaktari wakisema kuwa mama wa mtoto huyo aliwaambia kuwa ni jambo la kawaida nchini Romania wasichana wenye umri mdogo kuzaa watoto.

Wataalamu wanaonya kuwa wasichana wenye umri mdogo wanapopata mimba huyatia maisha yao katika hatari kubwa.

Utafiti umeonyesha kuwa wasichana wenye umri chini ya miaka 16 wanapopata ujauzito wana uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto njiti na watoto wao wachanga huenda wakafiri ndani ya mwaka mmoja.
 

ENZO

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,096
2,000
c ajabu! hapo mimba ilipoingilia hapo hapo inatokea.
 

afrodenzi

Platinum Member
Nov 1, 2010
18,154
2,000
c ajabu! hapo mimba ilipoingilia hapo hapo inatokea.

muheshimiwa mtot wa miaka kumi tundu litakuwa kubwa kweli kutoa kichwa cha mtoto???? ni rahisi kuingia hapo lakini sijui ilitokaje mzee... i cant get the picture.....
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
11,857
2,000
muheshimiwa mtot wa miaka kumi tundu litakuwa kubwa kweli kutoa kichwa cha mtoto???? ni rahisi kuingia hapo lakini sijui ilitokaje mzee... i cant get the picture.....

wakati wa kutoa mtoto vichocheo vya uzazi hukuza tundu kuwa shimo, si swala la miaka kumi ni swala la vichocheo vya uzazi kuwepo.
 

afrodenzi

Platinum Member
Nov 1, 2010
18,154
2,000
wakati wa kutoa mtoto vichocheo vya uzazi hukuza tundu kuwa shimo, si swala la miaka kumi ni swala la vichocheo vya uzazi kuwepo.

duuuhh ok
asante we learn something new every day...:smile:
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom