Binti wa kizigua anataka kunipeleka kwao. Naombeni ushauri wa haraka

hannibali

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
468
427
Habari za Leo wanaJamiiForums wote na poleni kwa majukumu ya kilasiku ya kutafuta kipato.

Niende kwenye mada moja kwa moja kiufupi mimi ni mpita njia nimetokea maeneo ya kilifi Kenya kuja Tanzania kutafuta fursa mbili tatu za kimaisha na malengo yangu binafsi zaidi ni kufika jiji kubwa la Dar es Salaam, nimepitia njia ya tanga na nikaona sio mbaya nikae siku mbili hapa tanga ili niangalie mazingira ya hapa kwa ujumla.

Kwakweli nilivutiwa na life style ya watu wa huku kuanzia kwenye ukarimu wao na maisha yao kwa ujumla wanavoishi. Katika siku mbili hizo nikakutana na binti mmoja mkarimu sana ambaye ndio alikuwa ananielekeza baadhi ya sehemu za huku na alinitambulisha kuwa yeye kabila lake ni zigua.

Basi nikapanga niongeze siku mbili zingine za kukaa huku kwa maana nizidi kutembelea sehemu nyingi zaidi, hizo siku nne za kuwa huku ziliisha jana lakini nikaona sio mbaya niongeze mbili zingine ambapo leo na kesho, sasa huyu binti kaniambia kwakuwa nitaondoka kesho kutwa basi sio mbaya nikaenda nae kwao ambapo ni nje kidogo ya mji kwa siku ya kesho halafu ndio niondoke.

Kusema kweli kwa ukarimu alionionesha tangu siku ya kwanza hapa nilishindwa kumpa jibu la haraka nikasema basi anipe muda halafu nitamjibu

Sasa wanajukwaa naomba ushauri wenu vipi nimkubalie kwenda kwao au vipi kwa maana mimi ni mgeni na sijui vizuri utaratibu wa maisha ya watu wa huku vizuri.

Nilikuwa naomba ushauri wenu wanajukwaa.

Asanteni!
 
Kuna babu yetu alienda tanga kikazi mpaka leo hajarudi

angalia yasikukute

hata hivyo kilichokufanya ukae siku zote huko ni nyege tu
Hapana sio nyege nataka nifahamu mazingira zaidi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom