Binti wa Kireno kaondoka na akili zangu kwenye foleni ya chakula cha bure Jijini Geneva (Switzerland)

mkuu haya maneno ni kama yanakuhusu.
Screenshot_20200511-161842_WhatsApp.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
ziko nyingi sana mkuu kwenye hizo ulizotumia ondoa .ch ukiweka hiyo dot ch inakuwa ni site hiyohiyo lakini ya lugha nyingine kijerumani, kifaransa, kiswiss ama kiitalty hizo za kiingereza sachi hivi Parship, meetic,love scout 24, eDarling, connecting singles, swiss friends dates na match pamoja na Elite singles...zipo nyingi mno jaribu hizo
duuh we jamaa kweli starehe unazizingatia sites zote unazijua hahahahaaa
ila kwakweli kwenye ilo suala hatutofautiani sana kiongozi we kula bata tu bwanaa
 
Wakuu leo nimeenda kupanga foleni ya kuchukua chakula cha bure kinachotolewa na mamlaka za jijini hapa kwa ajili ya wahamiaji, nimeona haiwezekani na ni ujinga mwarabu na raia wa ulaya akapange foleni ya kupata hiki chakula halafu mimi ninunue wakati ubora ni uleule na hakuna masharti kwenye ugawaji wake, na kiukweli imekuwa siku nzuri sana kwangu nimekutana na binti mrembo sana wa kireno ambaye amevuruga kabisa akili zangu kwa siku ya leo..

Nikiwa nimevalia T-shirt yangu ya ZANZIBAR na suruali ya jeans mida ya saa4 kasoro asubuhi kwa saa za hapa Uswisi nikawa nimefika mitaa ya Cornavin linapopatikana duka kubwa la vyakula la Migros – Supermarket wanapotoa vyakula hivi kwa watu wa karibu na mitaa yangu kama serikali ilivyoelekeza kupitia matangazo ya TV.

Watu walikuwa wachache sana na hapa ndipo macho yangu yakamuona huyu mrembo ambae baada ya kuzungumza nae akanieleza ni raia wa ureno aisee sikuwahi kuwaza na kujua kabisa kama kuna wareno wazuri namna hii, uzuri ni kwamba mimi sio muoga na haikunipa shida kumsogelea baada ya kumuangalia kwa mda kidogo ili nimuanze mazungumzo na kwa bahati nzuri na yeye hakuwa na shida akaonesha ukarimu na ushirikiano wa kutosha akaniambia anaitwa Bellina anafanya kazi kampuni ya ROLEX hapa jijini GENEVA kwa sasa wamepeana rotation ya kwenda kazini ili kujikinga na mambukizi tukajikuta kadri tunavyoendelea kupiga stori ndivyo tunavyoanza kuzoeana zaidi, watu wakawa wanaona kama tunafahamiana kabla kumbe ndio siku yetu ya kwanza kukutana baadae tukabadilishana namba za simu na tukaachana baada ya kupata mahitaji yetu.

Tangu niachane naye hapo Migros Supermarket akili yote inamuwaza yeye tu,nimefika kwangu cha kwanza kufanya ni kum-whatsapp alivojibu nikajihisi amani kidogo tukaendelea tena kuchart kwa kumuwekea vibwagizo vya mapenzi na yeye anajibu kiukweli hapa naiona kabisa lockdown yangu inakuwa nzuri sana siku mbili zijazo naamini nitakuwa na mtu mzuri wa kusaidiana nae huu mzigo wa kukaa ndani, ile hali ya kizunguzungu,stress na msongo wa mawazo inaenda kuisha hivi karibuni.

Huyu mrembo amefanya mawazo yangu yasifikirie kitu kingine chochote kwa mda huu zaidi ya kumfikiria yeye peke yake na nisiwe na utulivu wa akili kabisa mpaka kuna kazi ya ofisi hapa nilipigiwa simu ili niifanye online na inahitaji umakini mkubwa ili ikamilike kwa ufanisi lakini naona kabisa nitaiharibu imebidi niwapigie simu kuwaeleza najisikia vibaya kiafya.

Nina hakika hata mipaka ya ufaransa ikifunguliwa mpenzi wangu akaja na akanifumania nae hatasema kitu kabisa, zaidi atanipongeza tu.

Chukua hatua stahiki,Corona ipo na ni hatari
Parabora
Geneva - Switzerland
Mkuu Geneva nilifika hapo mwaka 2017,migros ni supermarket kubwa mno,haikuwa rahisi kukaa Geneva six months kwa special UN task,nilipenda mno kuishi huko
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom