Binti wa kazi za ndani House girl anahitajika

mgungani

Member
May 13, 2022
38
60
Natafuta binti wa kazi za ndani.

Mshahara 60,000 kula, mawazi, dawa, nguo juu yangu.

Kazi kupika kufua kuandalia mtoto chakula.

Kukaa kwa mwajiri.

Mahali DSM

Kama uko mikoani nauli itatumwa na utapokelewa Mbezi.

Piga simu au nibip kwa mawasiliano 0653 141 189
 
Ulaya huwa wasaidizi aka house girl wanaajiliwa na matajiri maana hohe hahe with ordinary life huwezi kumuafford maana ana haki zote kama mwajiriwa mwingine.

Hiyo hela ni ndogo sana kumlipa binadamu mwenzio, naye anahitaji kuwa na future, hapo ni kama unamfanya mtumwa.

angalau mlipe 200k, NSSF mlipie, matibabu, mwisho wa mwaka unampa bonus.
 
Lakini wewe uliepo ulaya una mwambia mzee wako awe na beki 3 huku bongo. Mshahara wake unampa ngapi?
 
Nilishakataza Wazazi wangu kukaa na house girl, baadala yake wanakaa na ndugu zangu ambao nawasomesha.

Halafu mimi sikai Ulaya nakaa zangu Tandika Dar hapa, Kwangu sikai na house girl maana sihitaji kumfanya binadamu mwenzangu mtumwa na kumtumikisha huku sina uwezo wa kumlipa, nilipogundua hili niliachana kabisa na hili jambo.

Siku nikiamua kukaa na binti au mabinti wa watu nitamlipa kima cha chini na haki zake zote.
 
Ulaya huwa wasaidizi aka house girl wanaajiliwa na matajiri maana hohe hahe with ordinary life huwezi kumuafford maana ana haki zote kama mwajiriwa mwingine.

Hiyo hela ni ndogo sana kumlipa binadamu mwenzio, naye anahitaji kuwa na future, hapo ni kama unamfanya mtumwa.

angalau mlipe 200k, NSSF mlipie, matibabu, mwisho wa mwaka unampa bonus.
Umeongea ukweli mtupu kiongozi ila tatizo hii ni bongo
 
Hizo kazi alitakiwa afanye mke wake,kwa kuwa wote mna majikimu mulnhezeeni huyo binti mtakaye mpata mshahara,angalau 150K-200K.

Huwezi mlipa binadamu mwenzio 60K ,huku wewe ukienda baada kwa siku 1 unatumia zaidi ya hiyo.lasivyo tafuta nduhu akudaidie kazi.
 
Msaidizi wa mama ntilie akiumwa juu yake, pa kulala juu yake na mahitaji mengine yote. 60K kwako ndogo ila kwa mwingine ni kubwa so long ana pakula na kulala.
Utawaweza binadamu na wema wa kuigiza mitandaoni!!.
Hapo utakuta wamewafuga hao mabinti majumbani mwao wanaamsha saa 11 alfajiri na kuwalaza tano usiku na gubu juu huku wakiwalipa 50K...ila nyuma ya keyboard sasa malaika yeye!!.
 
Hizo kazi alitakiwa afanye mke wake,kwa kuwa wote mna majikimu mulnhezeeni huyo binti mtakaye mpata mshahara,angalau 150K-200K.

Huwezi mlipa binadamu mwenzio 60K ,huku wewe ukienda baada kwa siku 1 unatumia zaidi ya hiyo.lasivyo tafuta nduhu akudaidie kazi.
Kumbuka huyu binti halipi kodi, hana gharama za chakula, matibabu n.k. Jaribu kuthaminisha hivi vyote, plus hiyo 60k halafu jiulize mshahara ungekuwa kiasi gani.
 
60 ni iliyobaki baada ya kula kulala mavaz na kuumwa chief. Ni kama laki 3 per month mkuu.
 
Nilishakataza Wazazi wangu kukaa na house girl, baadala yake wanakaa na ndugu zangu ambao nawasomesha.

Halafu mimi sikai Ulaya nakaa zangu Tandika Dar hapa, Kwangu sikai na house girl maana sihitaji kumfanya binadamu mwenzangu mtumwa na kumtumikisha huku sina uwezo wa kumlipa, nilipogundua hili niliachana kabisa na hili jambo.

Siku nikiamua kukaa na binti au mabinti wa watu nitamlipa kima cha chini na haki zake zote.
Usitumie lugha ya mtumwa kwa mfanyakazi wa ndani, ingawa analipwa hela ndogo. Lakini amekubaliana na muajiriwa wake kwa huo mshahara. Mfano kama mshahara wa mwalimu na daktari ni midogo sana kwa ajira yao lakini sio watumwa. Mtumwa huwa halipwi mshahara na hufanya kazi kinyume na matakwa yake.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom