Binti wa chenge mbaroni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, imemhukumu binti wa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Madina Chenge (25), alipe faini ya Sh 30,000 au atumikie jamii kwa miezi mitatu.

Msichana huyo amepatikana na hatia ya kuendesha gari bila kufuata sheria za barabarani na kugonga gari lingine.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Samwel Maweda, ametoa hukumu huyo leo baada ya kuridhishwa na maelezo ya upande wa mashitaka.

Kabla ya kutoa adhabu huyo, Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi, Naima Mwanga, aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kuongeza umakini kwa watu wengine.

Kabla ya hukumu, mahakama ilitoa nafasi ya kujitetea kwa mshitakiwa, alikiri makosa yake na akaomba apunguziwe adhabu.

Mahakama ilitoa hukumu ya kuitumikia jamii kwa miezi mitatu ama kulipa faini ya Sh 30,000. Mtuhumiwa alilipa faini na kuachiwa huru.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Novemba 17, mwaka huu saa 11:30 jioni, Madina alitenda kosa hilo akiwa anaendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 193 AYL.

Ilidaiwa mahakamani kuwa,gali alilikuwa akiendesha msichana huyo liligonga gari lingine aina ya Toyota Land Cruiser T958ATS katika Barabara ya Umoja wa Mataifa na kusababisha uharibifu wa magari yote mawili.
 
Haya sasa na babake mwambieni kesi ya rada imeisha atoe laki moja
naipenda tanzania nchi yangu,....hivi hii serikali kweli imejaa mapunguani...mnafikiri babake angepewa adhabu kali kwa kuua na kukutwa na gari isiyo na bima...huyu asingefanya ujinga kama huu,...anyway endeleeni jamani ndio mshakamata nchi .
 
Huu utani mwingine jamani umepitiliza adhabu kaili 30,000! Adhabu kali navyojua ni 30,000 na kifungo!

Binti wa Chenge ahukumiwa
Imeandikwa na Kenny Kwenga; Tarehe: 10th December 2009 @ 19:00 Imesomwa na watu: 306; Jumla ya maoni: 0

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, imemhukumu binti wa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Madina Chenge (25), alipe faini ya Sh 30,000 au atumikie jamii kwa miezi mitatu.

Msichana huyo amepatikana na hatia ya kuendesha gari bila kufuata sheria za barabarani na kugonga gari lingine.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Samwel Maweda, ametoa hukumu huyo leo baada ya kuridhishwa na maelezo ya upande wa mashitaka.

Kabla ya kutoa adhabu huyo, Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi, Naima Mwanga, aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kuongeza umakini kwa watu wengine.

Kabla ya hukumu, mahakama ilitoa nafasi ya kujitetea kwa mshitakiwa, alikiri makosa yake na akaomba apunguziwe adhabu.

Mahakama ilitoa hukumu ya kuitumikia jamii kwa miezi mitatu ama kulipa faini ya Sh 30,000. Mtuhumiwa alilipa faini na kuachiwa huru.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Novemba 17, mwaka huu saa 11:30 jioni, Madina alitenda kosa hilo akiwa anaendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 193 AYL.

Ilidaiwa mahakamani kuwa,gali alilikuwa akiendesha msichana huyo liligonga gari lingine aina ya Toyota Land Cruiser T958ATS katika Barabara ya Umoja wa Mataifa na kusababisha uharibifu wa magari yote mawili.
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4790
 
Haya sasa na babake mwambieni kesi ya rada imeisha atoe laki moja
naipenda tanzania nchi yangu,....hivi hii serikali kweli imejaa mapunguani...mnafikiri babake angepewa adhabu kali kwa kuua na kukutwa na gari isiyo na bima...huyu asingefanya ujinga kama huu,...anyway endeleeni jamani ndio mshakamata nchi .

Jamaa anagombania tena jimbo! wakimpa huyu mlafi kura tumekwisha watanzania!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom