jean phillipe beyun
Senior Member
- May 18, 2015
- 142
- 167
Kuna binti ambae tunafanya kazi pamoja na ambae nilimtoa outing siku moja, kinyume na matarajio akaniletea kundi la wasichana wenzie kunifilisi nami nika apply umafia wa hali juu kwa kuwakimbia na kuwatelekeza na bili kubwa waliyotumia wenyewe, mi nilikunywa bia 3 tu
Sasa kumbe tangu siku hiyo ameendesha kampeni kali ya kunichafua hapa kazini kwa mabinti wenzie kiasi kwamba hata nikiomba kampani ya kawaida tu kwenda lunch mabinti hunitazama chini hadi juu na mwisho kunisonya msonyo mkali sana na kuondoka zao huku wakitamka maneno kwa methali na mafunzo, wengine wakiniambia "" unalo babu"" sasa sijajua maana yake hadi sasa
Yote tisa, kumi nikaona nijaribu bahati yangu kwa binti mwingine ambae ni mtaratibu sana, yupo kivyake vyake na anaishi ki british sana hapa kazini, baada ya mazungumzo ya siku kadhaa, nikaona nimtafutie zawadi ndogo kusindikizia ujumbe wangu wa mahaba, weekend hii nikaenda dukani pale sinza duka moja linauza chupi tu za akina dada nikawaeleza nia yangu wakanifungia vizuri kwenye package maalum
Leo asubuhi tulipo sign in tu nikaangalia kushoto na kulia watu hawanitazami nikaenda haraka kwenye meza yake na kumpa kishkaji na kumwambia ni zawadi yake ni zawadi yake
Akaipokea nikarudi kwenye idara yangu maana tupo ghorofa tofauti ya 3 na 4
Nashangaa baada kama ya lisaaa moja nashtuka kumuona yule binti akinifuata huku amefura na kunirushia ile chupi usoni ikiwa imeshafunguliwa kwenye package yake na kuanza kunipaka kwamba namuonaje hadi nampelekea chupi,? Kwamba nisimfananishe yeye na flani (yule niliemkimbia bar)
Kumbe yule binti kaeleza kampuni nzima?
Nimepata aibu ya milele leo
Hivi wakuu nimekosea wapi?
Kumpelekea mwanamke zawadi kuna ubaya?
Mbona tulikua tunaenda vizuri tu tangu juzi? Au ni sumu amepewa na yule binti mwingine?