Binti mwenye malengo makubwa jijini Mwanza, ni mfano bora kwa wengine

Mar 12, 2016
72
32

Mfahamu binti Johari Swedy, mwanafunzi na mkazi wa Jiji la Mwanza. Ni binti anaestahili kuigwa na wengine kutokana na juhudi na malengo yake maishani.

Johari Swedy (kushoto) akizungumza na George Binagi @BMG (kulia) alipokuwa katika eneo la Ahsante Moto Jijini Mwanza.

Kutana na binti Johari Swedy (19), mkazi wa Jiji la Mwanza. Alizaliwa mwaka 1997. Ni mwanafunzi ambae historia ya masomo yake ilianzia shule ya msingi Mabatini aliposoma darasa la kwanza hadi darasa la saba na baadae akajiunga na shule ya sekondari Mtoni zote za Jijini Mwanza ambapo alisoma kidato cha kwanza hadi kidato cha na nne.

Baadae alijiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule ya sekondari Lugeye kabla ya kuhamia Mwanza Sekondari zote pia za Jijini Mwanza, mwaka huu kwa ajili ya kuhitimisha masomo yake ya kidato cha Sita.

Sifa kubwa aliyonayo binti huyu ni kuwa miongoni mwa mabinti wanaopenda kusoma masomo ya sayansi hapa nchini. Alijiunga na masomo yake ya kidato cha tano baada ya kufaulu vizuri masomo ya sayansi ambayo ni Fizikia, Kemia na Baiolojia kwa maana ya mchepuo wa PCB.

Kama ilivyo kwa wanafunzi wenye malengo ya kufanikiwa maishani, binti huyu anazo ndoto zake. Mosi ni kujikiza katika kipaji chake cha utangazaji baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya juu. Kipaji ambacho ni utangazaji. Lakini pia anasema pamoja na ndoto hiyo, anayo malengo mengine ya kuwa daktari ama mfamasia.

“Mimi ndoto zangu ni kuwa mtangazaji. Vile vile nina malengo zaidi kama si kuwa mtangazaji labda niwe mfamasia au niwe daktari”. Anasema binti huyu na kutanabaisha kwamba kipaji chake cha utangazaji kilianza kuonekana baada ya kujiunga na Mtandao wa Vijana na Wanahabari Watoto mkoani Mwanza (Mwanza Youth and Chilren Network-MYCN) ambapo alikuwa akiongoza kipindi cha watoto (Sayari ya Watoto) cha redio na luninga kupitia Metro Fm na Barmedas Tv zote za Jijini Mwanza.

Binti huyu anaenda mbali zaidi na kuwahamasisha wanafunzi wa kike nchini, kupenda kusoma masomo ya sayansi kutokana na umuhimu wake na anawatoa hofu wale wenye mtizamo hasi juu ya masomo ya sayansi kwamba masomo hayo ni magumu.

“Masomo ya sayansi kiukweli watu wanayachukulia kuwa ni masomo magumu, lakini ukiamua unaweza, napenda wasome masomo ya sayansi kwa sababu ni masomo mazuri sana na kama ni mtu kweli unapenda kusoma na unapenda ndoto zako zitimie, soma masomo ya sayansi maana yanakuruhusu kufanya kazi yoyote ile”. Anasema binti huyu.

Mbali na masomo, binti huyu anao mwamko mkubwa wa kujifunza mambo mbalimbali kuhusu maisha. Akiwa likizo anapenda sana kujifunza kuhusu kazi za nyumbani pamoja na ujasiriamali. Anasema muda wake wa likizo huutumia katika kusoma masomo ya ziada (tuition) na kumsaidia mama yake shughuli za gengeni (Mama lishe) katika Mtaa maarufu wa akina mama na baba lishe wa Ahsante Moto uliopo stendi ya zamani ya Tanganyika Jijini Mwanza.

“Mimi ni mjasiriamali kutokana na kuwa namsaidia mama yangu shughuli mbalimbali za kupika, nikiwa likizo. Kama sijaenda tuition (masomo ya ziada) nakuja kumsaidia mama shughuli za upishi, najifunza pia mambo mengine kuhusiana na biashara, anapokuwa hayupo mimi huwa naisimamia biashara kama ni ya kwangu”. Anaeleza binti Johari.

Mama mzazi wa Johari, aitwae Devota Alex maarufu kwa jina la Mama Taus ambae ni Mama lishe katika eneo la Ahsante Moto Jijini Mwanza, anasema anajivunia juhudi za binti yake katika kujifunza mambo mbalimbali muhimu katika maisha ambayo anasema yanamjengea binti huyu msingi imara kwa ajili ya maisha yake ya baadae.
 
huyu kweli ni mwanamke wa shoka
 
Sioni cha ajabu kuhusu huyo binti.Ninachoona ni malengo,malengo,malengo yaani malengo hewa ambayo hajayafikia.Anaongelea ndoto anazoota.Maisha sio kuota ni vitu halisi.Huwezi kuandika kuwa mtu amwige mtu kuota malengo!!! Watu huiga vitu halisia sio ndoto.

Pia lengo la kusema anasoma masomo ya sayansi halafu mwisho anataka kuwa mtangazaji ni upotezaji muda.Hawezi soma masomo magumu kama ya sayansi mwisho aishie utangazaji.Hilo si la kuiga.Kama lengo ni kuwa mtangazaji angesoma masomo kama KLF (kiswahili,kingereza na Kifaransa) KIDATO CHA TANO NA SITA ili aje kuwa mtangazaji mahiri
 
Yule alihutubia UN maendeleo yake vipi?namkubali zaidi kwa harakati zake za kimya kimya
 
Sioni cha ajabu kuhusu huyo binti.Ninachoona ni malengo,malengo,malengo yaani malengo hewa ambayo hajayafikia.Anaongelea ndoto anazoota.Maisha sio kuota ni vitu halisi.Huwezi kuandika kuwa mtu amwige mtu kuota malengo!!! Watu huiga vitu halisia sio ndoto.

Pia lengo la kusema anasoma masomo ya sayansi halafu mwisho anataka kuwa mtangazaji ni upotezaji muda.Hawezi soma masomo magumu kama ya sayansi mwisho aishie utangazaji.Hilo si la kuiga.Kama lengo ni kuwa mtangazaji angesoma masomo kama KLF (kiswahili,kingereza na Kifaransa) KIDATO CHA TANO NA SITA ili aje kuwa mtangazaji mahiri

hata mimi nimeshindwa kushangaa,
 
Mimi mtazamo wangu ni kwamba anaweza kusoma masomo ya sayansi na akawa mtangazaji mwenye uelewa mkubwa katika mahojiano hasa katika vipindi vinavyohusiana na mambo ya kisayansi katika media za hapa nchini au mataifa ya nje.
 
brah brah nyingi???hivi kuwa na malengounayoyaita makubwa ndo kitu cha kushangaza ? Ishu ni vitendo!... hata uwe na malengo ya kujenga nyumba angani huwezi lingana na mtu aliyefanikisha kujenga kibanda ardhini!

BANGO
 
Sioni cha ajabu kuhusu huyo binti.Ninachoona ni malengo,malengo,malengo yaani malengo hewa ambayo hajayafikia.Anaongelea ndoto anazoota.Maisha sio kuota ni vitu halisi.Huwezi kuandika kuwa mtu amwige mtu kuota malengo!!! Watu huiga vitu halisia sio ndoto.

Pia lengo la kusema anasoma masomo ya sayansi halafu mwisho anataka kuwa mtangazaji ni upotezaji muda.Hawezi soma masomo magumu kama ya sayansi mwisho aishie utangazaji.Hilo si la kuiga.Kama lengo ni kuwa mtangazaji angesoma masomo kama KLF (kiswahili,kingereza na Kifaransa) KIDATO CHA TANO NA SITA ili aje kuwa mtangazaji mahiri
we yehodaya wa wapi?kwani hauwezi kuwa daktari alafu mtangazaji?acheni zenu za kuwakatisha wa tamaa.damn it
 
Samahani mtoa mada lakini mbona sijaona cha ziada ambacho kimepambwa katika heading ya thread yako......

Abnormality makes popurality ........lakini hii haijaendana kabisa
 
Inavutia zaidi kushuhudia mwanzo wa ndoto/malengo yako,changamoto ulizopambana nazo hapo njiani mpaka kufikia mafanikio hayo.

Ila kusema tu aigwe kutokana na hicho anachoota haijajitosheleza
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom