Binti Makamba, Lundenga, Miss Tanzania na roho zinazoelea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti Makamba, Lundenga, Miss Tanzania na roho zinazoelea!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mizizi, Sep 14, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni dalili ya wazi kwamba ile dhana ya uzalendo iliyodumu kwa muda mrefu hapa Tanzania imeelekea kutoweka!

  Kikubwa na cha kushtusha ni kusikia taarifa ya Lundenga kwamba alipata taarifa saa tisa alasiri, wakati bado roho za watanzania zikiwa zinaendelea kuelea ndani ya maji ya kina kirefu kwenye bahari ya hindi.

  Ila lingine la kusikitisha ni kwamba, katika wadau wa tukio hilo ni Mtoto wa aliyekuwa katibu mkuu wa ccm taifa hivi karibuni! Hii inaonyesha udhaifu wa hawa viongozi wetu katika malezi na makuzi ya vijana wao katika masuala ya uzalendo na tamaduni za watanzania. Kama viongozi wetu wanatoa pruducts kama hizi majumbani mwao, tusitegemee mazuri kwenye utendaji wao kama methari ya kingereza inayotafsirika kwa kiswahili "nionyeshe rafiki yako, nikuambie tabia yako"

  Nilichojiuliza hapa ni kwamba, Mdhamini ndie mwenye influence katika project yeyote kutokea, sasa hapa vodacom hawawezi kwa namna yoyote ile kujiondoa kwenye lawama juu ya kadhia hii!

  Kufanya tukio la Miss Tanzania huku roho za watanzania zikiwa zinahangaika majini kuokoa uhai wao ni dharau kubwa kwa wahanga ha tukio hilo
  Pia Tukio hilo halikuwa na hadhi kuitwa miss Tanzania, kwa kuwa baadhi ya watanzania walikuwa katika ajali, na wengine walikuwa ni maiti zinazoelea majini!

  Ushauri wangu ni kwamba!
  1. Vodacom inatakiwa ijitokeze na kuomba radhi wa tz na wazanzibari kwa dharau waliyoionyesha juu ya hili
  2. Serikali ya Muungano itoe tamko juu ya hili kabla ya kuongeza mpasuko juu ya muungano wetu
  3. Watanzania wanaotoka znz wasusie, huduma, matukio, na misaada yoyote itokayo vodacom hadi pale watakapoomba radhi kwa dharau waliyoonyesha kwao!
  Nawasilisha
   
 2. i

  ikhwan safaa Senior Member

  #2
  Sep 14, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umemsahau MANGE KIMAMBI hapo
   
 3. tatizomuda

  tatizomuda Member

  #3
  Sep 14, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hiyo ni biashara ya watu sasa wangesitisha wangepata hasara hakuna uzalendo tena na hilo shindano ni la watu fulani walioanzisha wenye maslahi nalo sio taifa kama linavyotamkwa ndo maana kuna kipindi Lundenga alianzishiwa zengwe ajitoe kuandaa miss TANZANIA kutokana na kufanya vibaya ktk mashindano ya dunia akasema hawezi kujitoa wala kumuachia mtu sababu yy ndo mwenye hilo shindano.

  So hakuna utaifa hapo mkuu na ile kasumba inazidi kutuingia mioyoni ya kuwa kila mtu anajali maslahi yake na familia yake kama mafisadi wanavyoiba mali za umma kwa maslahi yao na familia zao, uzalendo kwishne babu!
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Issue nini hasa? Au ni Makamba?
   
 5. M

  Mwera JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa tu mkuu wazanzibari na watanzania walioguswa na msiba ule tayari wameshaisusia vodacom wengi wameacha kutumia huduma za voda na baada kama ya mwezi 1 hao voda wataipata nawatajua kua wanapoteza wateja,na hata smz wamekataa kupokea msaada wa vodacom ambao walitaka kujikosha baada yakufanya unyama mkubwa nadharau ile walioifanya.yetu macho na masikio ila voda naweza kusema wamejambia mtoni.
   
 6. n

  nndondo JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Tukitaka kujua upumbavu wa watanzania soma hao wanaojidai kuwa hakuha mahusiano kati ya biashara kichaa kama za voda za kushamiri kwa wizi wa kodi na maisha ya wazanzibar.

  Huo ndio ushamba wa watanzania, kuna siku mtafiwa na Rais wa nchi nao wataendelea na biashara zao, yaani kama nyie watanzania wenyewe mnaona hasara za miss tanzania kuahirishwa ni kubwa kuiliko maisha ya watanzania wenzetu ambao hata idadi yao mpaka sasa haijajulikana japo tunajua ni zaidi ya watu 1000, mtashangaa nini kesho mkiitwa panya nchi kwenu, nataka tu niwatoe ushamba kama hii swal ingekua south africa, hawa mbwa wasingefanya hilo tukio, hapa kwa kuwa wanaotakiwa kutoa ushauri ni wakina lundenga mkorogo na mwamvita bibi y dicloaf, tunaonekan tunaosema tuna wivu.

  Kitakachoendelea kuitafuna nchi yetu ni ushamba wa hawa wanaopata vyeo, na ndio ile conclusion yangu kuwa haisaidii kuwapa vyeo watanzania wasio na uzalendo maana wataishia kushibisha matumbo yao kwa kutoa sponsorship kwa ccm na matukio anayoshiriki kaka, tu na sio kubadilisha maisha ya watanzania kwa ujumla. Hili ndio tatizo, tazama wakina mafuru hivi wanaweza kuonyesha nini mchango wao pale pamoja na kupata cheo aliishia kupalilia iniative za dick omondi, alizozokuta mpaka leo wakenya wanapeta pale miaka zaidi ya mitatu tangu dick aondoke, wakina willliam kalombo wanafanya nini ambacho watanzania hawawezi kukifanya?

  Hili ndi tatizo letu umaskini wa akili na mawazo shenzi kabisa mbwa hawa wasiojali watu wao lakini eti watu wangepata hasara, jamani ungeumia tu kama baba yako angefia huko wale vichanga wewe huna habari nao
   
 7. a

  arigold JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  Atakaye warudisha VODA kwenye chati ZNZ huyu hapa....inasemekana yuko bize ana lobby SMZ iwasamehe Voda, lakini baada ya kauli ya Lundenga jana sidhani kama kutakuwa na ahueni kwa binti Makamba

  [​IMG]
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu mwenyewe tangia j2 nimehamia airtel na sidhani kama nitarudi voda na hii kampeni ya kutotumia voda iwe endelevu
   
 9. S

  Simcaesor Senior Member

  #9
  Sep 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania ni walewale, Uzalendo haulazimishwi.

  Hivi kuna mambo mangapi yanatokea hapa nchini kwetu mnapigakelele siku mbili then mnasahau na kukaa kimya moja kwa moja, mfano suala la mgao wa umeme sasa tumelizoea wakati ni suala nyeti na pia inatakiwa kuwa serious nalo, mawazili hawatendi kazi zao ipasavyo kama vile upishano wa waziri wa mambo ya nje na waziri wa wanyama, sasa tusiwe tunaondea tu bila kufuatilia na baada ya mda kusahau huo ni upungufu wa akili....

  Kuhama mtandao siyo solution waombe radhi kama mnavyotaka ili kutoa fundisho wa wengine then watoe huduma kama kawaida, bora hawa vodacom wanasaidia na msaada wao tunauona yapo makampuni kibao yako tu kimya. watanzania tusiwe na roho za kinafiki na maono ya sekunde.....
   
 10. Nkwesa Makambo

  Nkwesa Makambo JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 4,765
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  JAMANI HIVI MAJANGA NI SWALA LA MUUNGANO ? Wakati mwingine ukweli usemwe bila kumung'unyamun'nya maneno,hawa wenzetu muungano ni kitu muhimu sana na ndiyo sababu hata SUMATRA hawawezi kusimamia meli za Zanzibar.Kama wadhibiti wa usafiri wa meli hawana ruhusa kudhibiti vyombo vya majini Zenj, Kwanini ajali ifanywe jambo la Muungano.
  Pole kwa wale wataokwaza na hili swali,nami naomboleza Zanzibar,kenya na DRC
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kidoogo umenena
  kwa sababu kama ni kulaumu vodacom, basi
  bendi za dansi zilaumiwe kwa kusherehesha usiku ule na
  pia pambano la yanga na polisi tff ilaumiwe tuacheni siasa
  hili ni janga la wazanzibar na sisi tunawasapoti tu kama kenya.
  kitu kingingine mbona salamu zote za rambirambi zinatumwa kwa serikali ya zanzibar
  na siyo ya muungano yaani TANZANIA????????? pitia michuzi blog uchukue hatua
   
 12. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mimi ndiye nılıkuwa wa kwanza kuulıza kuhusu tff,watu wa kakaa kımya.
   
 13. mdeki

  mdeki JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 3,303
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  makamba+vodcom+miss tz+muungano=politics
   
 14. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Binti Makamba kumbe anajua kuvaa nguo..!!!
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nitakuelewa kama hutoangalia tena TBC, Startv, ITV, hutoendelea kuwa wanachama wa CCM, hutoangalia soka la bongo,....
   
 16. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndugu usiwe mnafiki, peleka lawama zako kule Baraza la Wawakilishi walioondoa udhibiti na ukaguzi wa shughuli za usafiri huko Unguja na kuwa si suala la Muungano.

  Voda haikuwa inaendesha chombo kile wala haikuwa inadhibiti usalama wa abiria.

  Think straight buddy!!
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hata kama Vodacom na kamati ya miss TANZANIA WANGESITISHA TAMASHA SIJUI SHINDANO Hilo roho ngapi zingepona, je maiti zingeibuliwa zaidi , je ukweli ungebadilika kuwa meli ya mizigo ilibeba abiria, ama wakaguzi hawakukagua meli, ama nini kingeondoa ukweli kuwa meli ilizama kwa uzembe wa kujaza watu kupita kiasi, Voda sijui miss Tanzania ni mbinu chovu za kutafuta huruma kwa upuuzi wa kuzamisha meli kwa ujinga wa mamlaka za kiutawala na kiutendaji kule Znz.
   
 18. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hawa wote ni takataka
  -VODACOM
  -MAKAMBA
  -LUDENGA
  -NA WALIOINGIA ,NASIKIA HATA WAZIRI ALITUMA MWAKILISHI MAANA YAKE ALIKUBALI WAENDELEE
   
 19. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  Jamaa inasemekana kwa duru zangu za uchunguzi yumo humu jamvini anatumia moja ya majina yake matatu. Ila ana kazi nzito sana hapa Vodacom wamechemka vibaya sana. Naona bora Vodacom waombe radhi na PR department iwajibishwe pamoja na mkurugenzi wao Miss Makamba. Itaweza kupunguza hasira na munkari na hali ya hewa chafu iliyopo sasa. Kukaa kwao kimya kunaweza kuzidisha hasira na kuonyesha dharau watumie busara sana katika hili.
   
 20. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red nakuunga mkono kwa sehemu kubwa. Shamhuna and His Co. aliishupalia sana SUMATRA iondoke zanzibar.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...