Binti wa Form 3 alibakwa mwaka 2008 shule moja wilayani Chato. Huyu Binti aliumia sana kisaikolojia kwa lile tendo la kubakwa. Ingawa alikuwa na uwezo mkubwa darasni, ilibidi ahache shule, kutokana na familia yake kuwa na uwezo mdogo. Lakini kwa bahati nzuri, Shangazi yake ambaye ni mwalimu, aliamua kumfadhili huyu Binti ili aendeleze ndoto yake ya kuwa daktari.
Binti alitafutiwa shule tofauti jijini Mwanza mwaka uliofuatia huku akimwacha nyuma mtoto mchanga na mama yake mzazi, na kwa bahati nzuri binti alijitahidi sana akaja kufaulu vizuri sana kidato cha 4 mwaka 2010, Alipata Division 1. Form 6 pia alipata Division 1. Na Kujiunga na chuo kikuu Muhimbili. Tunavyoongea yule Binti alishamaliza degree yake ya MD, na sasa hivi yuko nchini Norway anasoma PhD ya brain Surgery.
Swali fikirishi, huyu binti alipata adhabu kubwa sana ya kubakwa. Matokeo yake kapambana na kufikia malengo yake ingawa jamii pia ilimuadhibu kwa kubakwa. Je tunakuwa taifa la aina gani tunawaadhibu mabinti wa aina hii, badala ya kuwafariji?
Mbaya zaidi hadi watetezi (Wabunge) wanashabikia waliobakwa kufukuzwa shule?