Binti Huyu Hana Dogo Mmh!

Jamaa Ako = Wewe Mwenyewe

USHAURI: Utaoa "Mamlaka Ya Utabiri Wa Hali Ya Hewa" kabla haijanyesha keshatangaza itanyesha.

Raha ni kwamba pia kabla hajakusaliti atatangaza mapema so utajua mapema na kujiandaa kisaikolojia kuwa utasalitiwa mapema mwakani. Hupunguza maumivu.


Hilo ni chaka, Toka huko
Sawa mkuu
 
Labda ameshaahidiwa hivyo wakati wana "kwinchi kwinchi"
So ukweli wanao wahusika.
Labda aje rafiki yako kuomba ushauri.....
Nipo kama Wakili ,ameshanmbia ukweli jamaa yangu Huyo.
Kuhusu kuahidiana,Ndio!waliahidiana
 
Wewe nawe hueleweki, unatabia ya wivu usio na maana na unadharau sana.
1. Unasema hao wachumba walikubaliana kuishi pamoja kama mke na mume. Halafu unasema mume hajashirikishwa kivipi? Umejuaje? Walikubalianaje kama hawakujafiliana na kukubaliana?
2. Wenzako wanatambulishana kwa wazazi wao, wewe unadunisha hatua hiyo muhimu kwa kuiita "kudokezana". Sijui unamaana gani! Ndugu, hiyo ni hatua muhimu sana kuelekea kwenye ndoa na ni heshima mkubwa kwa wachumba, wazazi wao na jamii kiujumla wake. Acha wivu!
3. Binti anawajulisha ndugu zake wa karibu ili waanze kujiandaa na waweze kumfahamu huyo mtu wake na kumpa heshima anayostahili kijamii. Wewe unasema "bila aibu anawatangazia watu"! We vipi? Hao ni ndugu wa karibu, wadau muhimu. Aibu ya nini hapo? Inaonekana wewe unapenda sana mambo ya kufanyika gizani, au siyo?
4. Eti tambo na "mshawasha wa kuolewa". Mbona unaonekana kuumia sana? Wacha kumbeza binti wa watu, mchumba wa mtu! Kama na wewe unampenda basi pole sana jaribu mwingine maana huyo ameshawahiwa.

Mwisho, kuwa makini sana na uchaguzi wa maneno. Wafuatiliaji wengi wanaweza kuungana na mimi kuwa maneno yako mengi yamejaa wivu, dharau na chuki. Inaonekana wazi kuwa ilikuwa unammezea mate huyo binti! Nimeona nikudunge tu sindano upone. Pole lakini!
Hapana mkuu sipo hivo asee!umenielewa vibaya!
 
Kwa Mujibu wa Hadithi ya Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) Rehema na Amani ziwe Juu yake Amesema:-

Ficheni posa zenu na dhihirisheni harusi zenu.
Mwisho wa kunukuuu.

Maana yake usitangaze mambo ya uchumba wa posa kwa wasiohusika na harusi ndio mutangaze
Hivo ndivyo ninavyojua Maalim
 
Back
Top Bottom