Binti Huyu Hana Dogo Mmh!

MLALUKO JR

JF-Expert Member
May 3, 2015
962
305
Habarini ndugu zangu.

Poleni na hongereni kwa mapambano ya kuzisaka Seenti.

Kuna binti mmoja wa chuo kutokea pwani ni mpenzi au mchumba wa jamaa yangu ya karibu.

Kitu kinachoshangaza ni kuwa baada ya kuwa pamoja ktk mahusiano takribani mwaka mmoja sasa,huku wakiwa wameshadokezana kwa wazazi wao.
Japo waliweka miadi ya kuishi kama mume na mke,Binti bila haya wala aibu ameanza kutangazia watu wake wa karibu kuwa ndoa yake ipo karibu hapo mwakani japo rafiki yangu hajashirikishwa ktk hilo.

Napenda kuuliza je,ni sahihi kwa binti kuanza kujitangazia ndoa ingali bado hawajapanga Situation kamili??je,ni mshawasha wa kuolewa au ni tambo kwa wenzake wajue nae ataolewa??
Mabinti,jaribuni kuwa Na Subra!!!
Nawasilisha kwenu wadau!!
 
Jamaa Ako = Wewe Mwenyewe

USHAURI: Utaoa "Mamlaka Ya Utabiri Wa Hali Ya Hewa" kabla haijanyesha keshatangaza itanyesha.

Raha ni kwamba pia kabla hajakusaliti atatangaza mapema so utajua mapema na kujiandaa kisaikolojia kuwa utasalitiwa mapema mwakani. Hupunguza maumivu.

Hilo ni chaka, Toka huko
 
Labda ameshaahidiwa hivyo wakati wana "kwinchi kwinchi"
So ukweli wanao wahusika.
Labda aje rafiki yako kuomba ushauri.....
 
Habarini ndugu zangu.

Poleni na hongereni kwa mapambano ya kuzisaka Seenti.

Kuna binti mmoja wa chuo kutokea pwani ni mpenzi au mchumba wa jamaa yangu ya karibu.

Kitu kinachoshangaza ni kuwa baada ya kuwa pamoja ktk mahusiano takribani mwaka mmoja sasa,huku wakiwa wameshadokezana kwa wazazi wao.
Japo waliweka miadi ya kuishi kama mume na mke,Binti bila haya wala aibu ameanza kutangazia watu wake wa karibu kuwa ndoa yake ipo karibu hapo mwakani japo rafiki yangu hajashirikishwa ktk hilo.
Napenda kuuliza je,ni sahihi kwa binti kuanza kujitangazia ndoa ingali bado hawajapanga Situation kamili??je,ni mshawasha wa kuolewa au ni tambo kwa wenzake wajue nae ataolewa??
Mabinti,jaribuni kuwa Na Subra!!!
Nawasilisha kwenu wadau!!
Wewe nawe hueleweki, unatabia ya wivu usio na maana na unadharau sana.
1. Unasema hao wachumba walikubaliana kuishi pamoja kama mke na mume. Halafu unasema mume hajashirikishwa kivipi? Umejuaje? Walikubalianaje kama hawakujafiliana na kukubaliana?
2. Wenzako wanatambulishana kwa wazazi wao, wewe unadunisha hatua hiyo muhimu kwa kuiita "kudokezana". Sijui unamaana gani! Ndugu, hiyo ni hatua muhimu sana kuelekea kwenye ndoa na ni heshima mkubwa kwa wachumba, wazazi wao na jamii kiujumla wake. Acha wivu!
3. Binti anawajulisha ndugu zake wa karibu ili waanze kujiandaa na waweze kumfahamu huyo mtu wake na kumpa heshima anayostahili kijamii. Wewe unasema "bila aibu anawatangazia watu"! We vipi? Hao ni ndugu wa karibu, wadau muhimu. Aibu ya nini hapo? Inaonekana wewe unapenda sana mambo ya kufanyika gizani, au siyo?
4. Eti tambo na "mshawasha wa kuolewa". Mbona unaonekana kuumia sana? Wacha kumbeza binti wa watu, mchumba wa mtu! Kama na wewe unampenda basi pole sana jaribu mwingine maana huyo ameshawahiwa.

Mwisho, kuwa makini sana na uchaguzi wa maneno. Wafuatiliaji wengi wanaweza kuungana na mimi kuwa maneno yako mengi yamejaa wivu, dharau na chuki. Inaonekana wazi kuwa ilikuwa unammezea mate huyo binti! Nimeona nikudunge tu sindano upone. Pole lakini!
 
Jambo rahisi sana hili kwa wazoefu, ukweli ni kuwa huyo binti kaahidiwa ndoa ila tatizo ni huyo jamaa asiyeelewa kuwa mwanamke hataniwi kuhusu kuolewa!!!
 
Sio lazima awe ameahidiwa na huyo jamaa yako mkuu,inawezekana yupo mwingine aliyeongea nae na ana uhakika na ndoa ndio maana jamaa yako hajui kwasababu sio muhusika.
 
Kwa Mujibu wa Hadithi ya Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) Rehema na Amani ziwe Juu yake Amesema:-

Ficheni posa zenu na dhihirisheni harusi zenu.
Mwisho wa kunukuuu.

Maana yake usitangaze mambo ya uchumba wa posa kwa wasiohusika na harusi ndio mutangaze
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom