Binti Chongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti Chongo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by X-PASTER, Jun 16, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Alikuwa akimchukia sana mamake, kisa alikuwa ana chongo…
  Mama yake alikuwa anafanya kazi ya uwalimu na kufanya biashara ya kupika kwenye maharusi, ili kuweza kumtunza mtoto wake pekee. Mtoto ambaye alikuwa akimsomesha shule ya bweni kule Tabora. Mama huyu alikuwa mjane, mumewe alifariki kwenye ajali ya gari, miaka mingi nyuma....

  Siku moja alifunga safari kwenda kumtembelea mtoto wake kule shuleni. Mtoto wake hakufurahia ujio wa mama yake, na chuki yake ilionekana dhahiri kuwa amechukia.

  "Kwanini huyu mwanamke anapenda kuja kuniaibisha kila mara," alijisemea moyoni, dharau zake kwa mama yake na kutojali kwake kulionekana wazi wazi usoni kwake.

  Siku ya pili yake mwanafunzi mwenzake darasani alimuuliza… “kumbe wewe mama yako anajicho moja?” kijana yule akamjibu yule si mama yangu, ni jirani yetu kule nyumbani...

  Kwa kweli hakumpenda mama yake... alitamani apotelee mbali asimuone tena...
  Au afe hasiwepo tena duniani...

  Mama yake hakumchukia na wala hakuonyesha kisirani kwa mtoto wake…
  Kijana yule halisoma kwa bidii sana ili aweze kupata scholarship, ili atakapo rudi masomoni awe mbali na mama yake…
  Kwa bidii zake alifanikiwa kwenda kusoma nje ya nchi kwa miaka mitatu…

  Kwa miaka yote hiyo hakuwahi kuwasiliana na mama yake, na watu wakimuuliza kuhusu wazazi wake uwajibu kuwa walishafariki siku nyingi…

  Baada ya kumaliza masomo nje ya nchi, alirejea nchini na kununua nyumba, akaoa na baada ya miaka michache akapata watoto wawili…
  Akawa ni mtu mwenye furaha na maisha yake na familia yake…

  Siku moja mama yake ambaye sasa ashakuwa mzee sana, akaja kumtembelea, baada ya kuitafuta nyumba yake kwa takribani siku nne...
  Mama yake alikuwa ametamani kumuona mwanaye kabla M’Mungu ajamchukuwa…

  Na pia alitamani kuwaona wajukuu zake…

  Alipokuwa akigonga mlango, wakatoka wajukuu zake… walipomuona kibibi kizee chenye jicho moja wakacheka na kumwambia baba yao… kuna omba omba kaja anaonekana ana njaa sana huku wakicheka…

  Mwanaye alipotoka kumuona huyo omba omba, akagunduwa kuwa si omba omba bali ni mama yake mzazi…

  Alimwangalia kwa jicho kali na dharau na huku akimkaripia… hivi wewe kizee ujafa tuu…. Na umekuja kufanya nini hapa unatisha watoto zangu…
  Toka nisikuone hapa hatuna chakula wala pesa za kukupa….

  Yule mama akajibu kwa upole... “samahani baba nimekosea nyumba nilifikiri hapa anaishi mtoto wangu Fulani…!!
  Kijana akajibu huna mtoto nyumba hii huna haya weee mwanamke…!!

  Yule mama huku akilia ndani ya nafsi yake akajiondokea taratibu huku akijikongoja kwa uzee…

  Wiki chake kupita, kijana akaletewa barua kutoka kwa wakili wa serikali. Wakili akamtaka aende ofisini kwake. Alipofika na kujitambulisha, wakili akamfahamisha kuwa mama yake ambaye alikuwa analelewa nyumba ya wazee amefariki siku tatu nyuma. Akampatia na barua kutoka kwa mama yake. Wakili akashangaa kwani kijana hakuonyesha hata kusikitika…!!

  Habari ya kufiwa haikumuuzunisha hata chembe…
  Aliporudi nyumbani akajifungia ndani peke yake na kuisoma barua hile...

  Kwa mwanangu mpendwa... siku zote nilikuwa nakufikiria na kukuombea dua ufanikiwe...
  Nakutaka msamaha sana kwa kuja nyumbani kwako na kusababisha kutishika kwa watoto zako, kwa kuwa mimi nilikuwa chongo...!!

  Na pia nakutaka msamaha kwa vijana wote waliokuwa wakikutania kwa kuwa na mama ambaye ni chongo...

  Mwanangu mpendwa... Tangia siku ile nilipokuja kwako, nilipata maradhi na sikuweza tena kutoka nje...!!

  Nawashukuru sana hawa vijana wanao tutunza hapa kwenye nyumba ya wazee...!! kwa kuweza kututunza vyema...

  Mwanagu mpendwa... kuna jambo moja ambalo nililificha miaka yote hii na leo nimeona nikuandikie hii barua kukufahamisha kile kilicho kuwa ni siri yangu...!!

  Japokuwa utapokuwa ukiisoma barua hii... nitakuwa nimeshatangulia kwa Mola wangu...

  Ulipokuwa mdogo ulipata ajali mwanangu.... wewe na baba yako. Baba yako alipoteza maisha kwenye ajali hiyo, na wewe ukapoteza jicho lako moja...

  Mimi nikiwa ni mama yako sikufurahia kukuona ukiwa na jicho moja...
  Lakini sikuwa najinsi ya kufanya...

  Lakini nilijitahidi kutafuta pesa na nikachukuwa mkopo serikalini nikakupeleka nje ya nchi kufanyiwa operesheni ya jicho...!! Nikakubali kutolewa jicho langu moja kukupa wewe mwanangu ili uione dunia kwa macho mawili… huwe ni mwenye furaha duniani na kukuepusha kuchekwa na watoto wenzio....

  Wenzangu walishangaa sana kusikia kuwa nimetoa jicho langu kwa ajili yako mwanangu... lakini najivunia tendo langu hilo kwani ni tendo ambalo limenipa furaha ktk maisha yangu....

  I was so proud of my son who was seeing a whole new world for me, in my place, with that eye.…

  With my love to you… huo ni urithi pekee nilio weza kukupatia…

  Ndimi mama yako….

  Binti Chongo
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nafikiri alipaswa kumuambia yote haya akiwa bado mzima ili mtoto ajione alivyo mjinga. Haya mambo ya kutokuwa muwazi hadi dakika za majeruhi yanatukosesha mengi!!
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  huyo mtoto ni nanga! Huwezi hata siku moja ukamchukia mzazi wako. Whether u like or not, mna bond tayari. Huyu alikuwa hana hekima, kwa bahati mbaya hii haipatikani shule.
   
 4. s

  sinani Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  huyu jamaa hana akili hata kama ni profesa,kitendo cha mama yake kumleta duniani ni heshima tosha achilia mbali awe kilema wa kariba yoyote...mama ni mama
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Jun 17, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Duh masikini Binti Chongo. Inasikitisha sana hadithi hii.

  Licha ya jicho hata malezi unayopewa na mzazi wako inakupasa ushukuru ni wangapi wanatupwa majalalani?

  Ulale mahali pema Binti Chongo
   
 6. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,493
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Hii habari nimeishawahi kuiskia mahali, inasikitisha sana na nikiisoma kwa makini na utulivu huwa inanitoa machozi kabisa!
  Inawezekana si ya kweli, kwani mtu hawezi kumfanyia mama yake kitu kama hicho lakini inabeba ujumbe mzito kwetu kama wanadamu kuwa upendo wa mama/ mzazi kwa mtoto ni wahali ya juu mno kiasi kwamba mzazi anaweza kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtoto au tu kuhakikisha mtoto anakuwa na furaha maishani kama wenzie.
  Hapo ulipo nakupenda mama yangu, Mungu mbariki mama na Kinamama woote ulimwenguni kwa upendo wao wa ajabu kwetu!.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sio akina mama wote wenye upendo kihivyo..wengine wanatoa mimba sasa ivi...
   
 8. a

  agika JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yes hata mimi nishawahi kuisoma kitambo kidogo na ilikuwa kwenye Version ya Kiingereza na ilikuwa sio africa but all in all mzizi wa mmbuyu binadamu tumeumbwa tofauti wapo hao watu wanaona mama zao hivyo may be sio chongo but nakumbuka shule ya secondary kulikuwa na watu wanaona aibu mama zao wakija shuleni for any reason kisa eti ana muonekano wa kimasikini, hajavaa kupendeza,kilema en all that sasa fikiria huyu wa hivi si ndo anakuwa kama huyo kaka wa kumkataa mama yake? Mungu katuumba tofauti ile mbaya tuko binadamu ambao hatuna tofauti na shetani, maana hata wanyama wana upendo na mama zao
   
 9. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Zipo version nyingi za hiyo hadithi. Iliyo mashuhuri ni ile ambayo mama alikuwa na makovu ya kutisha ambayo yalimfanya mwanawe asimpende hadi siku alipotambua kuwa makovu hayo yalitokana na moto uliomuunguza mama yake aliporudi ndani ya nyumba inayowaka moto ili kumuokoa yeye Mtoto!
   
Loading...