Binti amlalamikia mpenzi wake kwa kumvalisha pete ya shilingi elfu 23,000

Mi nilimvalisha ya buku jero, nilinunua Mwenge kwa muuza urembo. Alifurahi sana, kwani aliamini amepata mpenzi wa kweli atakayefanya naye maisha.

Hakuhitaji thamani ya pesa kwenye Pete. Alihitaji thamani ya pendo langu kwenye maisha yetu
Mi wangu alinishauri kununua hizo za buku jero, japo nilitoa pesa mimi lakini alienda kuinunua mwenyewe, siku ya tukio kamkabidhi rafiki yake kaileta nikamvisha. Ikichubuka anaenda tena kariokoo ananunua nyingine analeta namvalisha upya. Maisha yansonga.
 
Mi wangu alinishauri kununua hizo za buku jero, japo nilitoa pesa mimi lakini alienda kuinunua mwenyewe, siku ya tukio kamkabidhi rafiki yake kaileta nikamvisha. Ikichubuka anaenda tena kariokoo ananunua nyingine analeta namvalisha upya. Maisha yansonga.
Mwanamke mpumbavu huivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Wako ni mke mwerevu mno
 
Kinachosikitisha Ni kwamba 95% ya Wana wake hawawezi kujua ili original ipi feki..so hata ukinunua ya 23000 MWAMBIE Ni 80000 na bado hawezi kuelewa chochote.
 
Inshu ni kwamba huyo dem hampendi mshikaji hata kidogo kwasababu sikuzote watu wakipendana Kasoro ndogo ndogo kama hzo hazionekanagi kabisa, Just imagine eti Pete ya uchumba ambayo ni ya mda tu dem anaMind kwamba ni mbaya hio inaonesha hata ukija kumuoa siku mkila daga wa bila nyanya jamaa hata lala ndani kwa mabango afu istoshe Madem kuweni makini saa nyingine unaweza pata Bwana anapesa kishenzi lakini kwa mitego midogo midogo kama hiyo ukashindwa ukaachika kisa jamaa kaConclude kwamba we sio wife material So kuweni makini
 
Wa kwangu ya uchumba na ndoa zote buku tano zote zilikua zenye rangi ya dhahabu GGM kwa Sasa zimechubuka vizuri zimebadilika rangi na kua za silver ...apa nawaza zikiendelea kuchubuka zitaleta rangi gani
 
Nacheka kama mazuri vile kmmmmmk

Kuna demu wangu mmoja hivi hapo mjini TIA alinambia yeye siku ya Graduation yake anataka Gauni la kushonwa kwa nani sijui vile(wadada wa mjini mtakuwa mnajua na bei zao) gharama yake ni laki 3. Nikamwambia sawa, nasubiri hiyo siku ya kuambiwa nitoe hiyo pesa mtu akashone gauni
manyoyaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachosikitisha Ni kwamba 95% ya Wana wake hawawezi kujua ili original ipi feki..so hata ukinunua ya 23000 MWAMBIE Ni 80000 na bado hawezi kuelewa chochote.
sasa hicho kinasikitisha au kinafurahisha..
 
Kuamini Pete ni kiashiria sahihi cha Ndoa(tukiweka mahusiano/uchumba pembeni) sidhani kama ni sahihi.

Mnaoamini Pete ndio kiashiria sahihi huwa nashindwa kuwaelewa.

Nilipooa baadhi ya watu wakawa wananiuliza Pete iko wapi, nikawajibu haina haja yoyote, hilo ni pambo tu kama mapambo mengine ni hiari ya mtu kulitumia.
 
Binafsi mbona nataka mixture ya diamonds na tanzanite?

And... yes. Me nimeona ni dharau. Ingemgharimu nini jamaa kucommunicate? Mahusiano mengi hufa kwasababu ya kukosekana mawasiliano. Napenda sana mawasiliano. Angemweleza tu. Na kulikua na haja gani ya kumvisha mabati kama ingine ilikua yaja?

Kwa upande mwingine hapo jamaa hana mke. Kibinti hakina akili. Kinapenda maisha ambayo hakina uhalisia nayo. Anadai kufanyiwa graduation part tena kwa demand order as if jamaa ni babake? Tena ananung'unika kabisa? Kmmk. Ndo ana zile mambo za kuleta na mashost ktk outings ambazo wanahitaji privacy na mpenziwe? Bogus kweli. Tumesoma mjini hapo ila huo ujinga hatujafanya. Hakina akili za maisha hiko kitakusumbua. Kama unamuacha muache kwa hizi tabia zake za kishamba akiamini anastahili kila treatment kutoka kwako as if ni babake. Kinaona kinemaliza dunia yote. Piga spana.
 
Back
Top Bottom