Binti alimaliza form 4 mwaka 2018 na kapewa mimba mwaka huu na kudai anasubiri kuendelea shule, je ni kosa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Wanasheria hebu tusaidiane hapa.

Mfano binti alipata divisheni 3 mwaka 2018 na akawa mtaani sasa kapata mimba, yeye anasema bado ni mwanafunzi anasubiri kwenda form 5.

Je, hii ni kesi ya kumpa mimba mwanafunzi?
 
Usidanganyike. Huwa tunasema ni mwanafunzi akiwa katika continuity au mwendelezo wa kusoma. Mfano tunajua watu wakihitimu form mwezi oktoba na anajiunga kidato cha tano mwaka unaofuata.

Kwa hiyo kwa suala lako labda huyo binti angekua alijisajiri kuanza kidato cha kwanza kisha akapatwa na dharula iliyomfanya asiwe shuleni kama vile ugonjwa, basi hapotutamuweka kundi la wanafunzi kwa sababu atakua anasubiri apone kisha akaendelee na masomo. Mbali na huo uhalisia basi hakuna ubakaji hapo kwa sababu ya unafunzi.

Suala la pili linaloweza kukubana ni umri wake, endapo ana umri chini ya miaka 18 hata kama sio mwanafunzi jua imekula kwako mzee maana kumpa mimba binti wa miaka 18 ni UBAKAJI hata kama mlikubaliana.

Na katika kipengele hiki wakiamua kukunyoosha ujue kuwa hauna pa kutokea maana mama yake ndiye shahidi namba moja wa kusema umri wa mwanae hata kama cheti cha kuzaliwa kipo kinasema huyu ni over 18.

Kila la kheri.
 
Usidanganyike. Huwa tunasema ni mwanafunzi akiwa katika continuity au mwendelezo wa kusoma. Mfano tunajua watu wakihitimu form mwezi oktoba na anajiunga kidato cha tano mwaka unaofuata...
Apparent age not real age
 
Back
Top Bottom