TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,511
- 11,271
Wakuu kuna binti ameniambia huwa ananifananisha na kaka yake na nimeshindwa kabisa kumuelewa anamaanisha nini.
Huyu binti tunafanya naye kazi sehemu moja na tuna mazoea ya kawaida kabisa ya kikazi zaidi. Kwa kweli ni binti mzuri na yuko singo. Binafsi sijawahi kumuonesha interest yeyote ingawa wakati mwingine huwa tunakuwa na matani ya hapa na pale (mara nyingine kuhusu mapenzi na maisha). Siku moja nikiwa nataniana naye mara ghafla akabadilisha topiki na kwa sauti ya msisitizo kabisa akaniambia kuwa huwa ananifananisha na kaka yake, nilivyomuuliza kwa nini akasema hata yeye mwenyewe hajui. Sikutaka kuendelea zaidi manake hata mimi nilipigwa na butwaa (kutokana na jinsi alivyosema kimsisitizo), tukaendelea na maongezi mengine.
Baada ya lile tukio huwa mara kwa mara najiuliza kuwa yule binti alikusudia nini, hasa ukizingatia kuwa sikuwahi kutegemea kwamba itafika siku ataniambia maneno hayo (tena kwa jinsi alivyoonesha kumaanisha anachokisema). Kama ameniambia kujilinda zaidi najiuliza kwa nini? wakati sijawahi kuonesha kumtaka? Au matani yangu yanamfanya adhani kuwa namtaka? Kama hakukusudia kujilinda ina maana ndo nimepewa taarifa kuwa milango ipo wazi?
Msaada wandugu!!!