Binti akisema amekufananisha na kaka yake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti akisema amekufananisha na kaka yake!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TANMO, Dec 19, 2010.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Wakuu kuna binti ameniambia huwa ananifananisha na kaka yake na nimeshindwa kabisa kumuelewa anamaanisha nini.

  Huyu binti tunafanya naye kazi sehemu moja na tuna mazoea ya kawaida kabisa ya kikazi zaidi. Kwa kweli ni binti mzuri na yuko singo. Binafsi sijawahi kumuonesha interest yeyote ingawa wakati mwingine huwa tunakuwa na matani ya hapa na pale (mara nyingine kuhusu mapenzi na maisha). Siku moja nikiwa nataniana naye mara ghafla akabadilisha topiki na kwa sauti ya msisitizo kabisa akaniambia kuwa huwa ananifananisha na kaka yake, nilivyomuuliza kwa nini akasema hata yeye mwenyewe hajui. Sikutaka kuendelea zaidi manake hata mimi nilipigwa na butwaa (kutokana na jinsi alivyosema kimsisitizo), tukaendelea na maongezi mengine.

  Baada ya lile tukio huwa mara kwa mara najiuliza kuwa yule binti alikusudia nini, hasa ukizingatia kuwa sikuwahi kutegemea kwamba itafika siku ataniambia maneno hayo (tena kwa jinsi alivyoonesha kumaanisha anachokisema). Kama ameniambia kujilinda zaidi najiuliza kwa nini? wakati sijawahi kuonesha kumtaka? Au matani yangu yanamfanya adhani kuwa namtaka? Kama hakukusudia kujilinda ina maana ndo nimepewa taarifa kuwa milango ipo wazi?

  Msaada wandugu!!!
   
 2. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  na wewe mwambie unamfananisha na dada yako
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Great thinker, Unadhani nikimwambia hivyo ndiyo nitapata jibu la fumbo alilonifumbia?
   
 4. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kwa kukufananisha ina maana ameshakurahisishia kazi ya kuwa karibu naye. Kazi kwako.
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu hudhani kuwa inaweza pia ikawa kinyume chake?
  Kuhusu kuwa karibu naye naweza kusema tupo karibu vya kutosha manake huwa tunazungumza mara kwa mara.
   
 6. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Je mlishawahi ku out pamoja?
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Unaweza ukawa unasoma zaidi ya kile kilichopo. Ningekuwa wewe ningeyaachia hayo maneno yake kama yalivyo.

  Kama kweli anakutaka basi ataendelea kukudondoshea vidokezo vya mafumbo na hata vya waziwazi.

  Kwa sasa tulizana tuli kama maji ya mtungi.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unafikiri kwamba hajakufananisha na kaka yake kweli ?

  Kuna binti mmoja kwenye elevator alinikazania sana kuniuliza kama nimesoma chuo alichosoma yeye, akinifananisha na mtu ambaye kashamuona chuoni hapo, nkamwambia tu kwamba mimi sikusoma hapo, na wala sikufikiria chochote zaidi, kwa sababu mimi mwenyewe nakutana na watu ninaowafananisha na watu niliowajua Tanzania ambao hawapo hapa nilipo.

  Waswahili wanasema duniani wawili, wawili.

  La kama kuna jengine zaidi umeliona utueleze.
   
 9. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  kwa hiyo we unafikiri nini? mbona jambo la kawaida kufananishwa?
  usiniambie tu mawazo yako yameenda kwenye malavi davi......
  manake wabongo tulivyo fasta....
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Binti mzuri yuko single. Je wewe uko single Teh Teh

  Huyu binti wewe ndiye umempenda na yeye kagundua sasa anakupa hizo story kukuwe kakarbu zaid iili uwe free. Hajasema wewe ni kaka yake kakufananisha tu . Haya hiyo ni dalili ya ni green light fanya unachotaka kufanya .

  Inawezekana una tatizo kama langu la Nimuazeje anzeje

  teh Teh teh . Utatupasha series inavyoendelea
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Labda huwa mnazungumzia masuala ya simba na yanga
  Vunja ukimya tamka unamtaka kimapenzi
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Welcome to Women Trix 101

  My take: Hapo huyo mdada anataka kuwa karibu na wewe for protection, lakini (msisitizo) hakuna kuchakachuana ndio tafsiri ya 'kaka'. Manake anataka uwe wingman,bodyguard,financial/emotional sponge au mshika pembe..Sasa its up to you kuamua unafanyaje.
   
 13. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sijawahi kwenda naye out zaidi ya kutoka kula pamoja tukiwa mzigoni (tena huwa inatokea kama coincidence, siyo kitu tunapanga naye)..
  Dah! mkuu si unajua hawa viumbe hawatabiriki, manake naweza sema nikae kimya kumbe bahati ndo inanipita hivyo.
  Nashukuru kwa ushauri..

  Mkuu kitu kinachonifanya nijiulize sana ni jinsi alivyowasilisha ile kauli, manake tulikuwa kwenye maongezi halafu out of no where akaniambia hivyo. Ni mtu ambaye tumefahamiana kwa miezi kama saba sasa,, muda wote huo hakuwahi kunifananisha na kaka yake aje anifananishe leo? Ina maana mwanzoni nilikuwa sifanani naye au?

  Umenifanya nicheke mkuu, ile taarifa haikuwa ya kawaida kwangu ndiyo maana nahisi kuwa kuna siri imejificha mahali...
  Yaani kipindi chote tulichojuana ghafla leo ndiyo nifanane na kaka yake?
  Ni kweli mawazo yapo kwenye malavi davi ila ndo nipo njia panda kuwa hayo malavidavi in positive or negative way...

  Nifanye ninachotaka kufanya? Hehehe!!! Hakuna ninachotaka kufanya mkuu, ingawa sitamtendea haki iwapo nitagundua kuwa lengo lake ni malavidavi halafu mimi nikatae. Ila ndo maana inabidi nilichukulie hili suala kwa uangalifu manake hawa wadada zetu huwa hawatabiriki. Anaweza kusema mimi Yanga kumbe anamaanisha Simba.. Sasa mkuu wewe ulishapata ufumbuzi wa lile tatizo lako la Umuanzeje anzeje?

  Simba na Yanga kiaje kaka?
  Huwa tunazungumzia mambo mengi tu kuhusu maisha na huwa namchukulia kawaida kabisa, sijawahi kudhani kuwa tutafika huku.
  Kama kweli ananitaka basi nitashawishika kusema kuwa wanawake ndiyo hawana uwezo wa ku-keep a man as just a friend, manake hii itakuwa kesi ya tatu kunitokea (mwanzo huwa nawachukilia kama rafiki ila baadaye mambo wanayageuza wenyewe)...

  Dah! Mkuu hayo yote uliyoorodhesha huwa nipo makini kweli yasinitokee manake inakera Bana kumshikia pembe mtu mwingine halafu hamna kitu unapata. Ila kwa kesi ya huyu Binti naweza kusema mimi siyo mtu wake wa karibu kuliko wafanyakazi wengine kwa maana wapo wafanyakazi ambao yupo nao karibu zaidi yangu. ila ni pale inapotokea tukiwa pamoja ndo mazungumzo ya hapa na pale na matani. Kwa hiyo ina maana out of wenzangu wote basi ameniona kuwa nafaa sana kukamata pembe nini? Mungu aepushie mbali......
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Inatokea ila mara nyingi wanataka kuchakachuliwa,uyo mdada anatafuta password yako. Mfano enzi mi nasoma chuo kuna mrembo alikuwa ivo ivo. Yeye anatokea kusini ambako mi sijawahi ata kufika ila alinilazimisha kuwa kakae,mara nyingi alifika kwangu kunililia shida zake,mfano nsipomsaidia analalama eti namfanyia roho mbaya,nataka ateseke yan maneno kibao. Alifika hatua anakuja kwangu asubuhi na kuondoka kama sa5 au sa6 usiku alaf anadai ela ya nauli au tax eti kachelewa kurudi hostel wakati mda wote anaangalia movie ndani kwangu. Pia alielewa fika kuwa mi nko single. Usipokuwa makni kwishnei!anaamia. Mwishowe nilipokuja kugundua eti marafik zake aliwaambia mi ndo mtarajiwa,yan hawa watu wanashindwa kujieleza. Kaka hapo angalia kama unaitaji poa,kama utaki mpotezee!
   
 15. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama mambo ya hivyoo mi pia nimepatikana wallah kuna mtu humu jf nilimwambia kafanana na kaka angu kimazungumzo,,,,na xpaster WA HUMU HUMU alinambia kanifananisha na mtu fulani kimatamko,,,,,BUT ,,,,,hakuna kilichoendelea wala kilichojificha, sasa ndugu mpenzi toa mawazo yasiyo aminifu kichwani mwako,,,,and every thing have it's time to come,,,,so if she loves you wallah i'm telling u she will tell u,,,bcouse girl's first day's THEY dont want to show exatly what we need from u,,,so THEY start taratibu taratibu with love gift,daily appointment,daily sms:A S-alert1:,and so manything's sooo WAIT,,,,
   
 16. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nashukuru kwa ushauri mkuu, kwa hiyo wewe ulimpotezea au?
  Mimi huyu hajawahi kunililia shida so far na wala hatujawahi kualikana makwetu zaidi ya kukutana kazini labda na mtaani sometimes.
  Ila nimependa penye red na nitaufanyia kazi ushauri wako kaka....
   
 17. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  HAPO ni kumuweka awe karibu then kunasiku atasema anapenda kuwa nawe na huo ukaka utaendelea kuwepo huku unachakachua. lakini usije ukawa married tukakushauri ujinga!
   
 18. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Asante Nilham kwa ushauri wako, nimeshindwa tu kukugongea Senks (Ok, nimefanikiwa tayari)..
  Ila sasa dada yangu huoni kuwa nimetegwa kwa binti kuniambia ananifananisha na kaka yake na nilipouliza kwa nini akasema hajui?
  Wewe unaweza kumfananisha mtu na memba wa family yako halafu ukawa hujui kwa nini umemfananisha?
   
 19. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Noted!!
  Nashukuru mkuu kwa ushauri..
  Hivi kwenye red ulikusudia kumaanisha nini vile?
   
 20. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #20
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  subhana llah,,,,,wallah ndugu yangu umeniziba hata mdomo siwezi tena kukujibu,,,labda ulikuwa wacheka kama kaka ake ndo akakufananisha jamani mbona watufanyia hivii tanmo vibaya hivyoo,,,
   
Loading...