Binti aandika barua kuacha shule, auza sare na madaftari

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,043
Mzee Salum Bakari amesikitishwa na kitendo cha binti yake kuandika barua ya kuacha shule na kuuza sare zake kisha kutoroka nyumbani.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake amesema kuwa siku ya tukio aliitwa shuleni na Mkuu wa shule ambayo anasoma binti ake kidato cha kwanza.

“Kwanza alianza kuchelewa kurudi shule, anarudi muda ambao wengine wamesharudi, tukifuatilia tunagundua kuwa shuleni hajaenda na nyumbani hayupo ina maana yuko katikati ameenda wapi? Ilifikia wakati nikawa na mawasiliano ya mwanafunzi wenzie nijue maendeleo yake,” amesimulia.

“Kwakweli sikupata taarifa ya kuwa mwanangu ameandika barua, lakini niliitwa shuleni na nikapewa barua ya mtoto aliyoandika ya kutaka kuacha shule. Mtoto aliandika kuwa haelelewi anachofundishwa kwakuwa anaona kama anawasindikiza wengine lakini,” amesema.

“Alipokubali kwenda shule kazi ilikuwa kupata sare za shule kwakuwa alikuwa ameuziuza na daftari pia. Nililazimika kutatufuta sare kwa watoto waliomaliza shule hiyo, nilipomwambia akafuate akasema sawa, na ilipofika saa 8 mchana alitoroka nyumbani mapaka sasa hajarudi,” amesema baba yake mzazi.

“Siku za nyuma nimewahi kumkamata akiwa anatembea na wanaume tofauti tofauti jambo lile sikulipenda kwakuwa niliona kuwa ni mtoto mdogo na hata nilipojaribu kufuatilia ili kujua alipo bado kwangu ni kitendawili kwakuwa nyumbani hayupo,” amesimulia.

Ofisa Elimu Kata Naliendele. Benjamin Ndossi amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na vidato vya juu katika Shule ya Sekondari Naliendele wanaacha shule kwa kuandika barua.

“Yaani mzazi anakuja na mtoto shuleni wakiwa wameongozana tayari ameshaandika barua ya kukataa shule kisa haelewi lugha, kibaya zaidi mzazi akiulizwa na mwalimu anasema kuwa nitafanyaje kama mtoto ameamua mwenyewe kukataa shule,” amesema.

Diwani Kata ya Naliende, Masoud Dali alisema kuwa sisi kama viongozi jukumu letu kubwa ni kuhakikisha kuwa watoto wanarejea shuleni na kuendelea na masomo.

“Hii tabia ya kuwaacha na kuridhika na maamuzi ya watoto haifai na tunaikemea kwa nguvu zote inawezekanaje mzazi unakubaliana na mtoto kuwa aache shule wakati serikali imeweka mikakati ya kuhakiksiha kuwa tunatengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi hatuwezi kukubali watoto wachukue maamuzi yenye madhara kwao kwa siku zijazo,” amesema Dali.

MWANANCHI
 
Ingekuwa Kagera ... !

FnumT0wWAAA__sM.jpeg
 
Haelewi lugha okei

Case ni ngumu hii ila arudi shule apambane vitu havijawa rahisi we are all set to conquer them

Head up girl child
 
Wametisha Sana wanafunzi WA huko,hawataki longo longo ni kuandika Barua na kusepa
 
Hao wanaanzia mambo hayo tangu darasa la nne. Hapo alipo hata kusoma vzr Kiswahili hawezi au pengine hajui kabisa kusoma.
Shida ya Pwani hiyo, wanawacheza watoto wakiwa wadogo.
Wanawafundisha tabia mbaya
 
.... na ndio matatizo ya walimu wetu wa siki hizi, kaishiwa mbinu anaropokea mtoto "kama hutaki shule andika barua usitusumbue" sababu hakuna mtoto anayeweza kuwa na akili hiyo bila kuropokewa... hata kama aliiga kwa mwenzie, wa kwanza kuandika na walimu wakachukulia poa wakatua mzigo ndipo kosa lilipoanzia...Enzi nipo shule, barua hiyo inaletwa inasomwa mstarini asubuhi (Assemble) Mwalimu mkuu akiwepo mbele ya wanafunzi wote wanaisikia kisha inachanwa chanwa na unacharazwa viboko 100 mbele ya wanafunzi wenzio unaambiwa beba daftari darasani hakuna mwingine kesho ataandika barua ya upuuzi huo.
 
Vijana wetu hususani walio shuleni wanasumbuliwa na hofu,
Anahofu kuzungumza Kiingereza,kunakopelekea kujichukia na zaidi kuchukia Kila hatua anayopitia.

Kuna haja ya jamii kushirikiana na hawa vijana.

Mzazi ana nafasi,lakini mwalimu nae awe tayari kutafuta mbinu wezeshi za kumsaidia kijana kujenga hali ya kujiamini.

Kabla ya mtoto kufundishwa mambo makubwa kwa mujibu wa masomo ya kidato chake,apewe mbinu za kujiamini ikiwemo kufundishwa vitu vya msingi katika lugha ya kuzungumza kama vile salamu,kuhesabu namba kwa kiingereza.na pia kutafuta na kuandika misamiati myepesi katika mazingira yanayomzunguka.

Mtoto aaminishwe kuwa,kukosea ni sehemu ya kujifunza.

Aambiwe kuchekwa ni njia itakayomsaidia kujifunza ,hvyo asiwape muda wale watakaoonesha kumcheka,kumdhihaki kwa kutokujua kwake.

Mtoto afundishwe kujipongeza kwa hatua yeyote anayoipiga Kila siku,haijalishi ni ndogo kiasi gani ,hata kama ni kurudia kuandika neno lile lile la Kiingereza .

Na pia shuleni,tuwe na kawaida ya kuwaalika watu wenye uelewa na masuala ya Saikolojia kuzungumza na watoto wetu

Kwa mtoto wa kike,kuacha shule kunaeza changiwa hata na kukosa kujiamini kunakosababishwa na kuingia hedhi.

Anakuwa na maudhi mengi yanayoweza sababishwa na maumivu ya mwili na mabadiliko yanayompata kipind hicho,anapokosa mtu sahihi wa kuzungumza nae ,hofu inamtawala na lazima kuacha anaona ni suluhisho la kwanza ili kuepuka adha ya anayoyapitia.

Bado hatujachelewa wakuu.
 
Diwani Kata ya Naliende, Masoud Dali alisema kuwa sisi kama viongozi jukumu letu kubwa ni kuhakikisha kuwa watoto wanarejea shuleni na kuendelea na masomo.
Wanaendelea na masomo wasioyaelewa... Wanakuwa ni wahanga wa long distance to and fro..njaa kali..na viboko vingi toka kwa walimu waliojaa misongo mbalimbali ya mawazo...

Dali acha majibu ya kisiasa..

Mamia ya watoto wanaacha shule kutokana na gape wanalokutana nalo sekondari. Kama tunataka wasaidia kweli tutoe gape hilo..
 
Mzazi ana nafasi,lakini mwalimu nae awe tayari kutafuta mbinu wezeshi za kumsaidia kijana kujenga hali ya kujiamini.
Nilikuwa naongea wa wanafunzi wangu wa form 1 juzi..weengi mnoo..

Wanasema wao wanaonekana vilaza kwa vile hawaelewi lugha wametoka kidumu na mfagio..waliotoka english medium ndo wanaonekana wana akili.
Wakasema, wao wawe na shule zao wafundishwe kwa Kiswahili masomo yote na waliotoka english medium wawe na shule zao wasome kiingereza.

Nikaona niHoja ya msingi na muhimu.
 
... mtoto kama amekiri mwenyewe haelewi anachofundishwa darasani apewe option nyingine; maisha sio darasani tu.

Ni wakati sahihi kile kifungu cha sheria "kwa ridhaa ya wazazi" kitumike. Waliokitunga sio wajinga.
 
Mzee Salum Bakari amesikitishwa na kitendo cha binti yake kuandika barua ya kuacha shule na kuuza sare zake kisha kutoroka nyumbani.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake amesema kuwa siku ya tukio aliitwa shuleni na Mkuu wa shule ambayo anasoma binti ake kidato cha kwanza.

“Kwanza alianza kuchelewa kurudi shule, anarudi muda ambao wengine wamesharudi, tukifuatilia tunagundua kuwa shuleni hajaenda na nyumbani hayupo ina maana yuko katikati ameenda wapi? Ilifikia wakati nikawa na mawasiliano ya mwanafunzi wenzie nijue maendeleo yake,” amesimulia.

“Kwakweli sikupata taarifa ya kuwa mwanangu ameandika barua, lakini niliitwa shuleni na nikapewa barua ya mtoto aliyoandika ya kutaka kuacha shule. Mtoto aliandika kuwa haelelewi anachofundishwa kwakuwa anaona kama anawasindikiza wengine lakini,” amesema.

“Alipokubali kwenda shule kazi ilikuwa kupata sare za shule kwakuwa alikuwa ameuziuza na daftari pia. Nililazimika kutatufuta sare kwa watoto waliomaliza shule hiyo, nilipomwambia akafuate akasema sawa, na ilipofika saa 8 mchana alitoroka nyumbani mapaka sasa hajarudi,” amesema baba yake mzazi.

“Siku za nyuma nimewahi kumkamata akiwa anatembea na wanaume tofauti tofauti jambo lile sikulipenda kwakuwa niliona kuwa ni mtoto mdogo na hata nilipojaribu kufuatilia ili kujua alipo bado kwangu ni kitendawili kwakuwa nyumbani hayupo,” amesimulia.

Ofisa Elimu Kata Naliendele. Benjamin Ndossi amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na vidato vya juu katika Shule ya Sekondari Naliendele wanaacha shule kwa kuandika barua.

“Yaani mzazi anakuja na mtoto shuleni wakiwa wameongozana tayari ameshaandika barua ya kukataa shule kisa haelewi lugha, kibaya zaidi mzazi akiulizwa na mwalimu anasema kuwa nitafanyaje kama mtoto ameamua mwenyewe kukataa shule,” amesema.

Diwani Kata ya Naliende, Masoud Dali alisema kuwa sisi kama viongozi jukumu letu kubwa ni kuhakikisha kuwa watoto wanarejea shuleni na kuendelea na masomo.

“Hii tabia ya kuwaacha na kuridhika na maamuzi ya watoto haifai na tunaikemea kwa nguvu zote inawezekanaje mzazi unakubaliana na mtoto kuwa aache shule wakati serikali imeweka mikakati ya kuhakiksiha kuwa tunatengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi hatuwezi kukubali watoto wachukue maamuzi yenye madhara kwao kwa siku zijazo,” amesema Dali.

MWANANCHI
afadhari ya mtoto anaesema kweli kuliko anae teketeza pesa ya wazazi wake kama ataki shule aulizwe anataka nn kama kuolewa aozeshwe kama ufundi upelekwe akajifunze kama biashara apewe mtaji
 
Shida ya Pwani hiyo, wanawacheza watoto wakiwa wadogo.
Wanawafundisha tabia mbaya
kila siku wanawaona wazazi wao wakicheza vigodolo wakiwa watupu huku nyumba vijana wakiwaigizia serikali kupiga marufuku vigodolo inaogopa kupoteza kura
 
Back
Top Bottom