Bingwa wa kusilimisha Wakristo ameingia Qatar Wakristo wengi wahofiwa kusilimu. Eneo la FIFA lapambwa kwa maneno ya Mtume Muhammad S.A.W

Bakiif Media

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
346
1,183
Qatar, imemualika mhubiri mkali zaidi duniani, ambaye kwa maneno yake amefanikiwa kusilimisha mamilioni ya Wakristo duniani. Huyu ni bingwa Zakir Naik

Zakir Naik tayari amefika Doha nchini Qatar kabla ya Kombe la Dunia la FIFA 2022, na atatoa mihadhara ya kidini katika muda wote wa mashindano nchini humo. Mamilioni ya Wakristo wahofiwa kusilimu.

1668945016788.png

Wakati Kombe la Dunia la FIFA la 2022 linaanza saa moja jioni ya leo nchini Qatar, mhubiri maarufu wa Kiislamu mwenye Zakir Naik, tayari amewasili Doha nchini Qatar kabla ya Kombe la Dunia la FIFA 2022, na atatoa mihadhara ya kidini katika muda wote wa michuano hiyo nchini humo.

"Mhubiri Sheikh Zakir Naik yuko Qatar wakati wa Kombe la Dunia na atatoa mihadhara mingi ya kidini wakati wote wa Kombe la Dunia" ndani na nje ya viwanja.

1668945166940.png

.................

Wakati huo huo Qatar Yaonyesha Hadithi za Mtume Muhammad (s.sa.w) Katika Maeneo ya Kombe la Dunia la FIFA 2022

1668945353670.png

Wenyeji wa Kombe la Dunia la 2022 Qatar wamepamba kukaribisha ujio wa mashabiki wa soka. Mmoja wao anaonyesha dondoo za hadithi kutoka kwa Mtume Muhammad SAWW kwenye kona tofauti za barabara katika nchi ya Ghuba.

Kulingana na vyombo vya habari kadhaa vya humu nchini, michoro inayoonyeshwa inalenga kuutambulisha Uislamu kwa mashabiki wa soka ambao watakuja kutazama mashindano ya soka yanayofanyika kila baada ya miaka minne.

1668945420460.png

Nukuu za hadith za Mtume (s.a.w.w.) ina maandishi ya kiarabyu na tafsiri ya Kiingereza. Michoro hiyo ina hadithi kuhusu huruma, hisani, na motisha ambazo zinawahimiza watu daima kufanya mema.

Baadhi ya hadithi ni pamoja na, “Kila jema ni sadaka”, “Asiyekuwa na huruma kwa wengine, hatatendewa huruma”, na “Jilindeni na Moto wa Jahannam”.

Qatar inaonekana kuchukua fursa ya Kombe la Dunia la 2022 kama msukumo wa kushiriki utamaduni na maadili yake na wageni wanaokuja kutoka kote ulimwenguni.

1668945534300.png

Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar limebakiwa na masaa machache tu, limeratibiwa kuanza Novemba 20 hadi Desemba 18.

Toleo la mwaka huu litakuwa ni mashindano ya kwanza kuandaliwa Mashariki ya Kati, ya kwanza katika nchi yenye Waislamu wengi, na ya kwanza kufanyika mwishoni mwa mwaka wa kalenda, mwezi Novemba na Desemba.
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
10,552
11,353
Watu wanaenda kuangalia mashindano ya kombe la dunia yeye analeta mambo ya mhadhara wa kidini, sio pahala pake.

Na kwenda mbinguni hakuhusiani katu na mambo ya kuslimu, hayo mambo ya kuslimu yanabaki hapa hapa duniani, hizo ni siasa tu religious politics.
 
Bakiif Media

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
346
1,183
Watu wanaenda kuangalia mashindano ya kombe la dunia yeye analeta mambo ya mhadhara wa kidini, sio pahala pake.

Na kwenda mbinguni hakuhusiani katu na mambo ya kuslimu, hayo mambo ya kuslimu yanabaki hapa hapa duniani, hizo ni siasa tu religious politics.
Michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar Huenda ikawa michuano ya soka yenye utata zaidi katika historia ya FIFA.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
17,703
26,421
Qatar, imemualika mhubiri mkali zaidi duniani, ambaye kwa maneno yake amefanikiwa kusilimisha mamilioni ya Wakristo duniani. Huyu ni bingwa Zakir Naik

Zakir Naik tayari amefika Doha nchini Qatar kabla ya Kombe la Dunia la FIFA 2022, na atatoa mihadhara ya kidini katika muda wote wa mashindano nchini humo. Mamilioni ya Wakristo wahofiwa kusilimu.

View attachment 2422130

Wakati Kombe la Dunia la FIFA la 2022 linaanza saa moja jioni ya leo nchini Qatar, mhubiri maarufu wa Kiislamu mwenye Zakir Naik, tayari amewasili Doha nchini Qatar kabla ya Kombe la Dunia la FIFA 2022, na atatoa mihadhara ya kidini katika muda wote wa michuano hiyo nchini humo.

"Mhubiri Sheikh Zakir Naik yuko Qatar wakati wa Kombe la Dunia na atatoa mihadhara mingi ya kidini wakati wote wa Kombe la Dunia" ndani na nje ya viwanja.

View attachment 2422132
.................

Wakati huo huo Qatar Yaonyesha Hadithi za Mtume Muhammad (s.sa.w) Katika Maeneo ya Kombe la Dunia la FIFA 2022

View attachment 2422135

Wenyeji wa Kombe la Dunia la 2022 Qatar wamepamba kukaribisha ujio wa mashabiki wa soka. Mmoja wao anaonyesha dondoo za hadithi kutoka kwa Mtume Muhammad SAWW kwenye kona tofauti za barabara katika nchi ya Ghuba.

Kulingana na vyombo vya habari kadhaa vya humu nchini, michoro inayoonyeshwa inalenga kuutambulisha Uislamu kwa mashabiki wa soka ambao watakuja kutazama mashindano ya soka yanayofanyika kila baada ya miaka minne.

View attachment 2422136

Nukuu za hadith za Mtume (s.a.w.w.) ina maandishi ya kiarabyu na tafsiri ya Kiingereza. Michoro hiyo ina hadithi kuhusu huruma, hisani, na motisha ambazo zinawahimiza watu daima kufanya mema.

Baadhi ya hadithi ni pamoja na, “Kila jema ni sadaka”, “Asiyekuwa na huruma kwa wengine, hatatendewa huruma”, na “Jilindeni na Moto wa Jahannam”.

Qatar inaonekana kuchukua fursa ya Kombe la Dunia la 2022 kama msukumo wa kushiriki utamaduni na maadili yake na wageni wanaokuja kutoka kote ulimwenguni.

View attachment 2422138

Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar limebakiwa na masaa machache tu, limeratibiwa kuanza Novemba 20 hadi Desemba 18.

Toleo la mwaka huu litakuwa ni mashindano ya kwanza kuandaliwa Mashariki ya Kati, ya kwanza katika nchi yenye Waislamu wengi, na ya kwanza kufanyika mwishoni mwa mwaka wa kalenda, mwezi Novemba na Desemba.
JESUS CHRIST! KING OF KINGS!!
 
Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
68,953
135,585
Mtangazaji atakuwa anatangaza na shehe Zakir Naik atakuwa anatoa mihadhara. Jamani si zitakuwa kelele hizo?
Halafu mtu umefunga safari kutoka kwenu hadi Doha kwa ajili ya kwenda kuangalia soka, hiyo mihadhara unaenda kuisikiliza ili upate nini? Wanawake 72 mabikira?
"Mhubiri Sheikh Zakir Naik yuko Qatar wakati wa Kombe la Dunia na atatoa mihadhara mingi ya kidini wakati wote wa Kombe la Dunia" ndani na nje ya viwanja.
 
Bakiif Media

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
346
1,183
Mtangazaji atakuwa anatangaza na shehe Zakir Naik atakuwa anatoa mihadhara. Jamani si zitakuwa kelele hizo?
Halafu mtu umefunga safari kutoka kwenu hadi Doha kwa ajili ya kwenda kuangalia soka, hiyo mihadhara unaenda kuisikiliza ili upate nini? Wanawake 72 mabikira?
Hakika, watu watakuwa radhi kusikiliza hoja za Dr Zakir Naik kuliko kuangalia mpira. Na huko ndiko kufaulu kwa dini. Huyo ni Bingwa mwenye hoja matata. Usithubutu kuangalia Television yake nyumbani kwako. Nyote mtasilimu.
 
Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
68,953
135,585
Kusilimu kwa Seedorf kuwa Mwislamu kulipongezwa sana katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu. Na Issam Toutate Gwiji wa zamani wa soka wa Uholanzi na klabu ya AC Milan Clarence Seedorf ametangaza kuwa amesilimu. Je hao ndio wakristo wa mchongo?
Seedorf hajawahi kujazwa na Roho Mtakatifu. Seerdorf alikuwa Mkristo wa mchongo. Angesilimishwa Kaka tungeamini kwamba mmemsilimisha Mkristo
 
16 Reactions
Reply
Top Bottom