Binamu Bananga: CHADEMA tunakutana kujadili mahojiano ya Rais Samia na BBC ili kujibu nini? Nasisitiza tusikurupuke

kwa hiyo mnataka akubaliane na ile kauli ya yule jamaa aliyeko Canada watu wasusie bidhaa na huduma eti serikali ikose mapato..

Hilo la Lema linatosha kabisa kuona upumbavu mwingi kwa watu eti tunawategemea ni chama mbadala na tuwape dola...
M-Canada alitakiwa awe waziri wa mambo ya ndani Lissu angeshinda
 
Ukweli upi hapo umetuambia? Chama kife kivipi kwa mawazo yako chama kitakufa? Swali kwako ebu ni tuelezi watu ambao tayari wamehukumiwa kwa hiyo kesi ya ugaidi maana Samia kasema tayari wengine wamehukumiwa wataje waliohukumiwa kwanza, tuanzie hapo
Ukweli upo.
Jaribu kufikiri WAZO la kugomea huduma serkali ikose mapato.
Yaani ugome kupanda gari
Ugome kunywa maji
Ugome kutumia Umeme
Ugome kunywa dawa za hosp
Ugome kununua nguo
Ugome kununua chakula
Je zoezi hili linawezekana kwa Tz? Wazo la KIJINGA ambalo haliwezi kutekelezeka

Vijiwe vya Twiter, sio zamani kulikuwa na michango , angalau kuweka mawakili sio mijadala tu.

Kumbe CDM ni Mbowe ndio maana anakuwa mwenyekiti wa maisha wengine wote hawana vision yoyote.

Kupoteza muda kujadili mazungumzo ya BBC na Rais, yataleta impact gani?
 
Namhurumia sana Shemeji yangu Hawa kwa kuwa na mtu kama huyu. Kwakuwa Shemeji yetu Hawa ndio kila kitu kwenye familia basi naamini ipo siku atapata mwanaume wa kweli mwenye heshima na anayejua kutafuta.

Bananga siku ukiachwa ndio utajua mwanaume sio kuvaa suruali bali ni kupambana
 
Hii sio mada ya hapa. Peleka kwenye uzi wake au kafungulie uzi wake huko tutakuja kujadili.

Hata maofisini ndio mnaharibu kazi hivi hivi, file la huku mnapeleka kule halafu kazi zinachelewa kutekelezwa.
Swali likijibiwa kwa jibu mambo uwa shwali.
Bananga anatakiwa kujibu swali langu linalotokana na uzi wake wa kufikirika / Kusadikika. Ref Shabaan Robert
 
- Chadema wanashinikiza mama aingilie mahakama kivipi wakati kwa ile kauli yake ya jana ni kama ameshaingilia huo uhuru wa mahakama?

- Bananga anataka kusema yale aliyozungumza Samia jana yalikuwa na ukweli? kwanini hataki Chadema imjibu? uelewa wake mdogo anataka kuwaambukiza na wengine sio, Samia alisema Mbowe alijificha Nairobi, Bananga anakubaliana na hiyo kauli?

- Uhuru wa habari aliosema Samia na Bananga anaupigia mstari ni upi? ule wa kufungulia blogs na vingine kama magazeti (Mwanahalisi, Tanzania Daima) kuendelea kubaki kifungoni?

- Anazungumzia "think tanks", kwa hili andiko lake nae anajiona ni "think tank" wa Chadema licha ya kasoro zote zilizomo, hao "think tanks" huwa hawajisemi ni maneno yao ndio yanawashawishi wengine kuwafahamu pale wanapoongea, huyu jamaa anadhani "think tanks" ni malaika kutoka mbinguni, hajui kuna wakati nao hukosea.

Huyu Bananga sasa namuona anataka kuitumia Chadema kama ngazi ya kupata teuzi CCM, anaropoka hivi kujitengenezea mazingira siku akichepuka wampokee wampe na cheo, hope rafiki zake kina Msando na wengine watamuwezesha kupata atakacho huko CCM.
Aisee
 
Back
Top Bottom